Marekani imeamua kukusaidia kujitenga na Makonda. Marekani imekutega Rais na Mwenyekiti wangu Dr. John Pombe Magufuli. Imekusaidia na kukupa nafasi adhimu. Jitenge na Makonda kabla ya mambo mrama kwenda!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Sidhani kama utakuwa uamuzi wa busara kwa mwenyekiti kujitenga na Makonda kwa sasa,Kujitenga na Makonda ni kukubaliana na mawazo ya wamarekani, Kuna vitu lazima ujifunze kuviangalia kwa macho ya tatu, Mwalimu wangu wa Physics alikuwa anasema jaribu kuwa nje ya mada na uwe mwangaliaji kwa mbali ndio utaona uhalisia,
Nakukumbusha,
Mwana Mfalme wa Saud alipoamua kwa makusudi na maslahi yake na kwa uwazi kabisa kumuua Mwandishi wa Habari aliyekuwa anaandikia CNN Jamal Khashogi, Turkey alikuwa kiranja kuionyesha US Kuwa Mwanamfalme ni mkosaji, na ushaidi upo, lakini US Iliziba masikio,umeshajiuliza kwanini?
Maslahi, Trump alimtetea mwanamfalme waziwazi, na pia Pompeo alitumwa Turkey na baadaye SAUDIA Kuhakikisha kwamba mambo yanakaa sawa, hatimaye ERDOGAN alisalimu amri! Unajua sababu?
Nini nafasi ya maslahi ya US na magharibi katika serikali ya awamu ya 5. Toka Rais ameapishwa hajakanyaga US wala EU na kwingineko, Je maslahi ya US na washirika wake yaliyoimarishwa awamu ya 4 yanarindwaje? Ikiwa Kiongozi aliyeko madarakani hana muda nao!!!
Je nani ni wamiliki wa makampuni ya ACACIA na BARICK? Nini hatima ya maslahi ya Mataifa ya nje?
Embu jiulize unamfungia mtu ambaye hana umuhimu wa kuja nchini kwako si ujinga huo.
Suala la Makonda halihitaji Muhemuko, wala Siasa za Kipumbavu, Sababu zilizoongelewa ni za Kishabiki zaidi.