Serikali imuondoe Paul Makonda haraka kabla mambo hayajaharibika. Tamko lijalo linaweza kuathiri nchi pakubwa

Ningelikuwa na kauwezo ile mi INVECO ningeitumbukiza baharini kwa sababu hawa jamaa wanaweza weka bolt na nut kumbe ni makamera yao ya kuwapelekea siri za jeshi letu. Siyaamini sana haya mabeberu. Hakuna msaada pale bali uchuro tu
Hakuna siri za Jeshi mkuu.
Jeshi ni international .
Siri ni uoande wa TISS na CID tuu.
Jeshi lina mpaka wachina,Warusi ,Wamarekani n.k.wanabadilishana uzoefu na Teknolojia na mbinu za kivita mana kuna wakati wanakua na operations za pamoja kama kule Kongo na kwingineko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati Waziri Kabudi alienda ziara Marekani.
Wakati wa mahojiano na waandishi wa habari, aliulizwa, " kwa nini Serikali ya Tanzania haijafanya uchunguzi na kutoa taarifa kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi"
Alijibu kwa kuwauliza swali. " Kwani nini hadi leo toka aliyekuwa Rais wa Marekani , John Kennedy kupigwa risasi na kufa miaka mingi iliyopita hadi leo hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mauaji hayo"
Kiuhalisia aliuliza vizuri.
Lakini wanafalsafa hunena , The boss is always right.
Mkubwa huwa hachelewi ila anakawia kufika.
Kwa waswahili mzee akiharibu hali ya hewa, humsingizia mto to aliye akaribu naye.
Inchi kama Tanzania hatuwezi kujilinganisha na Inchi ya Marekani.
Katika maamuzi magumu ya Ki dunia Marekani ana veto power.
Kwa hiyo katika swala hili kubishana na Marekani ni sawa na kugombana na hakimu mahakamani au raia wa kawaida kugombana au kubishana na Rais Makufuli.
Tuwe wapole na tutafakari na tukubali yaishe kwa maslahi ya Taifa letu.
At least kule Marekani kuna watu walikamatwa na kuhojiwa.
Kuna misako ilifanyika.

Kulinganisha na Lisu ni jambo la hovyo.
Lisu ushahidi unaweza kupatikana kwa wepesi mana alikua anatishiwa na watu wanaojulikana na simu zao zingeweza kufuatiliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umekosa kazi ya kufanya?

Mwaka wa ngapi huu unapiga chapuo RC atolewe?
 
Ndugu wana JF, kila mmoja amesoma tamko la hasira la Marekani juu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul Makonda.

Kwa desturi za USA, mlengwa mkuu hapo ni Rais Magufuli na serikali yake, walichofanya ni kuipima serikali yetu itamfanya nini Makonda baada ya wao kutangazia Dunia kuwa hawataki akanyage Marekani.

Makonda asipoondolewa, tujiandae kususiwa na Dunia nzima, maana Marekani ndio taifa lenye nguvu za kila aina Duniani.

Hata mataifa yanayojitegemea Kiuchumi yana ufyata kwa Marekani, sembuse sisi tunaojitegemea kwa asilimia 56%? Huku 44% tukitegemea kusaidiwa na Mabeberu?

Kama unajua trend reading, Ubalozi Marekani walikuwa wanatoa taarifa inayofanana na balozi nyingine kama ubalozi wa Ulaya, Uingereza nk.

Usishangae ndani ya siku chache ukawasikia washirika wa Marekani nao wakimpiga marufuku Makonda kukanyaga huko.

Kama serikali ikizembea kumfukuza Kazi Makonda ili kujisafisha, usishangae likatoka tamko la kuzuia misaada kwa Tanzania, halafu tuwekewe na vikwazo ikiwa ni pamoja na kuzuia watalii wasije Tanzania kwakuwa ni nchi hatari kiusalama.

Wazungu wanaweza kutukumia vyovyote, hambo la msingi na haraka ni kumuondoa Makonda ofisini na kuteua mtu mwingine atakaefanya tofauti.

Chonde Chonde washauri wa Rais Magufuli, tunawapenda sana na tunaipenda serikali yetu, Makonda Mmoja asiingize nchi kwenye mgogoro wa Kidiplomasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamekuambia tamko lingine wanalitoa lini? Hii ni nchi huru. Hatuogopi mtu yeyote awe kibaraka au beberu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikitiko langu kubwa ni tuhuma aliooredheshewa ya kudhulumu uhai wa watu kadhaa (kukatisha uhai wa watu kabla ya wakati wao). Hili ni jambo ambalo serikali inapaswa ilitolee maelezo ni kwa namna gani vyombo vya usalama vya nje vifahamu pasipo na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali haiwezi kutolea maelezo upumbavu wewee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother wazee wetu walifanikiwa Sana kuliunganisha taifa hili, hadi tukaitwa kisiwa cha amani.
hebu jiulize tungali kisiwa cha amani? Na Kama bado tunakoenda tutaendelea kuwa kisiwa change amani?
Katibu mkuu CDM aliwahi Kukaa rumande huko kusini kwa wiki kadhaa kwa kosa la kufanya mkutano wa ndani kinyume na maagizo ya mkuu wa kaya hadi Leo baba wa watu anahudhuria kesi ndogo iliyodumu kwa miaka kadhaa bila kuhukumiwa, Ni ushahidi gani unatafutwa wakati alikamatwa akiwa kwenye kikao?
Je mwenezi wetu na Katibu mkuu wetu hawafanyi vikao mikoani? Nani kawashitaki au kuwanyima vibari? Kwa hiyo sheria inawahusu wale na hawa haiwahusu; huu so unyimi wa haki?
Kuhusu wasio julikana na wateka nyara hili unalijua, tatizo tunashindwa kuwabaini Hawa watu wanaositisha haki za watu kuishi najua unakumbuka kule baharini, beach zetu zilitapika wafu wote waliomezwa miaka dahari! tunashindwa kujitetea, tukatoa majibu lainiii!
Ujue mwizi akimwibia mlinzi,mtuhumiwa wa Kwanza ni mlinzi, hadi mlinzi atakapombainisha mwizi.
Wenzetu wameshaona tunakoenda siko wanataka kuturejesha kwenye njia sahihi, hata hao unaowajua wewe walianzia Huku huku.
Salaam,
Tanzania bado ni hazina na ni kisiwa cha Amani, Changamoto kubwa inayoendelea ni mgongano wa maslahi na tabaka la walionancho, wanaofaidika, wasionancho na wale wafaidika waliowekwa pembeni, sijui wewe unaangukia kundi gani hapa.
Kuhusu Mikutano, Baada ya uchaguzi kasi ya mikutano haiwi kubwa kwa kuwa sasa wateule na wachaguliwa watakuwa busy kushughulika na maendeleo na kero za waliwachagua. Mbunge ana nafasi kubwa ya kufanya vikao na wananchi wake bila kujali chama anachotoka, na katika hili sidhani kama kuna aliyezuiliwa.
Wasiojulikana? Ni dhana potofu, au ni hofu inayoenezwa kwa maslahi ya watu wachache.
Issue ya Bahari Beach? Kaka nikwambie kitu? Bahari ina tabia ya kusarisha takataka kuelekea Pwani, kwa Mimi ambaye nimekaa karibu na Bahari kwa muda mrefu ni kawaida sana kukuta mabaki pwani, aidha ya watu, boat au wakati mwingine hata samaki wakubwa.
Mtu ana thamani kubwa sana, hawawezi kupotea watu 5 halafu ndugu wasiwatafute, Nikuulize wewe binafsi umepotelewa na Jirani,Ndugu, Jamaa au rafiki wangapi? Unipe jibu kwa idadi na majina, kama huna utakuwa mzushi.
Kwa kuwa umesahahu naomba nikukumbushe yaliyojiri utawala uliopita ambao sasa hivi hamuachi kuusifia japo kwa wakati ule mlikuwa mnakesha mitandaoni kuukashifu:
Siku njema.
 
Chamsingi Mh akili makosa aliyo yatenda ndan ya nchi kwa maandishi then taarifa itumwe Marekan kwa bwana Pompeo former leader of CIA hapo nchi inaweza kuwa salama make hakuna mkamilifu chini ya jua.
 
Ndugu wana JF, kila mmoja amesoma tamko la hasira la Marekani juu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul Makonda.

Kwa desturi za USA, mlengwa mkuu hapo ni Rais Magufuli na serikali yake, walichofanya ni kuipima serikali yetu itamfanya nini Makonda baada ya wao kutangazia Dunia kuwa hawataki akanyage Marekani.

Makonda asipoondolewa, tujiandae kususiwa na Dunia nzima, maana Marekani ndio taifa lenye nguvu za kila aina Duniani.

Hata mataifa yanayojitegemea Kiuchumi yana ufyata kwa Marekani, sembuse sisi tunaojitegemea kwa asilimia 56%? Huku 44% tukitegemea kusaidiwa na Mabeberu?

Kama unajua trend reading, Ubalozi Marekani walikuwa wanatoa taarifa inayofanana na balozi nyingine kama ubalozi wa Ulaya, Uingereza nk.

Usishangae ndani ya siku chache ukawasikia washirika wa Marekani nao wakimpiga marufuku Makonda kukanyaga huko.

Kama serikali ikizembea kumfukuza Kazi Makonda ili kujisafisha, usishangae likatoka tamko la kuzuia misaada kwa Tanzania, halafu tuwekewe na vikwazo ikiwa ni pamoja na kuzuia watalii wasije Tanzania kwakuwa ni nchi hatari kiusalama.

Wazungu wanaweza kutukumia vyovyote, hambo la msingi na haraka ni kumuondoa Makonda ofisini na kuteua mtu mwingine atakaefanya tofauti.

Chonde Chonde washauri wa Rais Magufuli, tunawapenda sana na tunaipenda serikali yetu, Makonda Mmoja asiingize nchi kwenye mgogoro wa Kidiplomasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata ungekuwa wewe mtu anayekutafutia waganga unamuondoaje ?
 
Kimsingi makonda siyo msemaji wa serikali hivyo na wao wameonyesha udhaifu mkubwa Sana ۔makonda Ni mkuu wa mkoa huwezi kutoa tamko Kama hii kisa mkuu wa mkoa but kwa kuwa imetoke Ni vyema akachia ngazi pia pro kabudi apunguze majibu ya haraka haraka hata Dem ukimtongoza anajibu subiri kwanza nifikirie
Bro angalia kauli zako central cyo mbali ujue...😆😆😆😆😆
 
Salaam,
Tanzania bado ni hazina na ni kisiwa cha Amani, Changamoto kubwa inayoendelea ni mgongano wa maslahi na tabaka la walionancho, wanaofaidika, wasionancho na wale wafaidika waliowekwa pembeni, sijui wewe unaangukia kundi gani hapa.
Kuhusu Mikutano, Baada ya uchaguzi kasi ya mikutano haiwi kubwa kwa kuwa sasa wateule na wachaguliwa watakuwa busy kushughulika na maendeleo na kero za waliwachagua. Mbunge ana nafasi kubwa ya kufanya vikao na wananchi wake bila kujali chama anachotoka, na katika hili sidhani kama kuna aliyezuiliwa.
Wasiojulikana? Ni dhana potofu, au ni hofu inayoenezwa kwa maslahi ya watu wachache.
Issue ya Bahari Beach? Kaka nikwambie kitu? Bahari ina tabia ya kusarisha takataka kuelekea Pwani, kwa Mimi ambaye nimekaa karibu na Bahari kwa muda mrefu ni kawaida sana kukuta mabaki pwani, aidha ya watu, boat au wakati mwingine hata samaki wakubwa.
Mtu ana thamani kubwa sana, hawawezi kupotea watu 5 halafu ndugu wasiwatafute, Nikuulize wewe binafsi umepotelewa na Jirani,Ndugu, Jamaa au rafiki wangapi? Unipe jibu kwa idadi na majina, kama huna utakuwa mzushi.
Kwa kuwa umesahahu naomba nikukumbushe yaliyojiri utawala uliopita ambao sasa hivi hamuachi kuusifia japo kwa wakati ule mlikuwa mnakesha mitandaoni kuukashifu:
Siku njema.
duuh hivi ni kweli?!?, niliwahi kuona heche,matiko wanazuiliwa na polisi kufanya vikao vyao na waajiri wao, sijui sababu ilikuwa nini!!!!
 
Ndugu wana JF, kila mmoja amesoma tamko la hasira la Marekani juu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul Makonda.

Kwa desturi za USA, mlengwa mkuu hapo ni Rais Magufuli na serikali yake, walichofanya ni kuipima serikali yetu itamfanya nini Makonda baada ya wao kutangazia Dunia kuwa hawataki akanyage Marekani.

Makonda asipoondolewa, tujiandae kususiwa na Dunia nzima, maana Marekani ndio taifa lenye nguvu za kila aina Duniani.

Hata mataifa yanayojitegemea Kiuchumi yana ufyata kwa Marekani, sembuse sisi tunaojitegemea kwa asilimia 56%? Huku 44% tukitegemea kusaidiwa na Mabeberu?

Kama unajua trend reading, Ubalozi Marekani walikuwa wanatoa taarifa inayofanana na balozi nyingine kama ubalozi wa Ulaya, Uingereza nk.

Usishangae ndani ya siku chache ukawasikia washirika wa Marekani nao wakimpiga marufuku Makonda kukanyaga huko.

Kama serikali ikizembea kumfukuza Kazi Makonda ili kujisafisha, usishangae likatoka tamko la kuzuia misaada kwa Tanzania, halafu tuwekewe na vikwazo ikiwa ni pamoja na kuzuia watalii wasije Tanzania kwakuwa ni nchi hatari kiusalama.

Wazungu wanaweza kutukumia vyovyote, hambo la msingi na haraka ni kumuondoa Makonda ofisini na kuteua mtu mwingine atakaefanya tofauti.

Chonde Chonde washauri wa Rais Magufuli, tunawapenda sana na tunaipenda serikali yetu, Makonda Mmoja asiingize nchi kwenye mgogoro wa Kidiplomasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamekusikia
 
Back
Top Bottom