jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,530
- 9,550
Nianze kwa kusema habari wapendwa.
Nianze kwa kusema thread yangu nimeianza kwa mfumo wa swali hali ya kuwa ndani inamaelezo machache japo yenye kuendana na swali pia.
Sababu ya kuleta thread hii ni kwa sababu ya baba yangu mdogo ambae alikuwa akifanya kazi magereza kipindi cha miaka ya 80 na mpka sisi tunakuwa yeye alikuwa ni mtumishi wa serikali.
Alikuwa ni mtumishi wa magereza nasi sote kama watoto tulikuwa tunajua tu kama ni mtu anaelinda wafungwa na kazi zinginezo za ki askari magereza lakini alikuwa akiogopwa mno ndani ya familia na ukoo kiujumla.
Alifungua kampuni ya mbao na kuwa na maisha mazuri mno kipindi hicho lakini alikuwa ni mtu mwenye ujivuni na mengineyo mungu amsamehe juu ya hilo.
Maisha yalikwenda hivyo vizuri akiwa anafanya miradi yake ya kuchanja mbao ndani ya hyo kampuni baada ya kuacha kazj na kuendelea na tenda tofauti tofauti za serikali,lakini mungu taratibu akawa anaendelea kuuza kitu kimoja baada ya kimoja kiasi cha kwamba mpaka tunavyozungumza mda huu ni kwamba hana hata nyumba ya kuishi,maisha yake anatembea na mfuko kila anakoenda anakaa mpka jioni msipomuuliza analala yani hivyo.
Miaka mitatu nyuma hali yake ya akili ikaanza kubadilika kama akilala usiku anapiga tu makelele au kuongea hovyo,na wakati mwengine anaweza kuwa anaongea tu maneno yasiyoeleweka,aliyekuwa anavaa suti leo hii anavaa nguo mwezi na hataki kuivua tabia ya ubabe bado ipo hvyo kufnya ndugu kama kumtenga sabab ya kuleta ubabe popote aendapo plus uchiz.
Basi nikapata wasaa wa kuongea na bimkubwa na kumuuliza je alikuwa anafnya kazi gani magereza bimkubwa hakupindisha maelezo bali ni kwamba alikuwa kwenye kitengo maalum cha kunyonga wafungwa wenye hukumu za kifo,na ndo maana hata familia ilikuwa inamuogopa sana kutokana na ukatili wa kazi aliyokuwa anaifanya.
Nimerefer kisa hichi cha ndugu yangu kabisa,na kuna wengine wengi ambao wapo ndani ya majeshi yetu lakini baada ya kustaafu maisha yao yanakuwa ya ajabu na wengi kuishia kwenye uchizi au kujiua, je serikali huwa na utaratibu gani na wastafu hawa wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama?
Na pia nitoe ushauri kwa wengine ambao wamejiunga katika vyombo vyetu hivi vya ulinzi na usalama wenye umri kama wangu wa ujana kujitahidi kufanya kazi kwa weledi na haki maana kama ukiishi kwa kudhulumu na kudhulumu haki za watu huko mbeleni mambo huwa mazito mno juu yako,pia serikali ingetengenezo chombo cha counseling kwa hawa ndugu zetu hasa jinsi ya kuinteract na raia bila kusahau ushauri nasaha wa mara kwa mara.
ahsanteni