EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,325
Muungano wa Makandarasi wa Kichina Tanzania wanaidai serikali sh 287.1 bn. Deni hili limeanza tokea mwaka 2009. Asilimia 65.5 ya barabara zinazojengwa nchini zinajengwa na makandarasi wa Kichina. Baadhi wa makandarasi wameamua kuhairisha projects zao baada ya kukosaa fedha na mikopo toka benki. Wamemwandikia mawaziri wa ujenzi na fedha na wameongelea hili suala na TANROADS lakini wanadai hakuna kilichofanyika. Wanataka serikali iheshimu mikataba iliyoingia.
Kwa, mfano kuna kampuni ya Kichina inaidai serikali sh 110bn na wamelipwa sh10 bn tuu mwaka huu wakati costs za ujenzi wa barabara husika ni sh 60bn. Kwa sababu hiyo, kampuni imeamua kuhairisha ujenzi wa barabara ya kilometa 132 toka Isaka hadi Ushirombo mkoani Shinyanga. Kampuni nyingine inayojenga barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni, Sumbawanga imeamua ku-slow down ujenzi wa barabara hiyo wakisubiri fedha toka serikalini. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Balozi Herbert Mrango alipoulizwa alisema kama hayo wakandarasi wana malalamiko wafuate taratibu za kulalamika