A
Anonymous
Guest
Ninaomba kufikisha kero yangu kwa Waziri wa Nishati. Serikali inahamasisha wananchi kutumia nishati safi kama gesi na umeme ili kupunguza matumizi ya mkaa na kulinda mazingira, lakini gharama za nishati hizi bado ni kubwa kwa wananchi wengi.
Gesi nayo imekuwa na bei ya juu, mtungi mdogo unafikia zaidi ya shilingi 26,000 na mtungi mkubwa zaidi ya shilingi 60,000. Kwa upande wa umeme, matumizi ya majiko ya umeme yanakuwa changamoto kutokana na gharama kubwa, ambapo uniti moja kufikia zaidi ya shilingi 350 ni mzigo mkubwa ukilinganisha na kipato cha Watanzania wengi.
Waziri naomba mliangalie suala hili kwa kina kwa sababu gharama hizi haziendani na hali halisi ya maisha ya wananchi wa kawaida. Kama tunataka watu waache matumizi ya mkaa, ni muhimu nishati mbadala iwe nafuu na iweze kumudu kwa wengi.

=======================================
Ninaomba kufikisha kero yangu kwa Waziri wa Nishati. Serikali inahamasisha wananchi kutumia nishati safi kama gesi na umeme ili kupunguza matumizi ya mkaa na kulinda mazingira, lakini gharama za nishati hizi bado ni kubwa kwa wananchi wengi.
Gesi nayo imekuwa na bei ya juu, mtungi mdogo unafikia zaidi ya shilingi 26,000 na mtungi mkubwa zaidi ya shilingi 60,000. Kwa upande wa umeme, matumizi ya majiko ya umeme yanakuwa changamoto kutokana na gharama kubwa, ambapo uniti moja kufikia zaidi ya shilingi 350 ni mzigo mkubwa ukilinganisha na kipato cha Watanzania wengi.
Waziri naomba...
Samahani mkuu 'AGK' wa TANESCO, ninavyoona mimi hujamsaidia chochote huyo mteja na sisi wengine tuliokuwa tunatarajia kupata jibu la kutosha kutoka kwenye kampuni yako.
Hayo majiko ya umeme yanayopendekezwa ni majiko ya aina gani, yapo sokoni hapa kwetu?
"Kutumia umeme kidogo" maana yake ni nini? Jiko kuwa 'energy efficient' tafsiri yake ni kutumia umeme kidogo?
Maoni yangu ni kwamba, mtaalam unapopata fursa nzuri kama hii ya kutoa elimu kwa wateja wako, unaitumia ipasavyo. Hapa hukutusaidia chochote na jibu lako hili.
Ukweli tunaoushuhudia wenyewe humu majumbani mwetu, na siyo...