Serikali inamuogopa Hosea: Dk Slaa

Serikali inamuogopa Hosea: Dk Slaa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Dk Slaa asema serikali inamuogopa Dk Hosea

Mwandishi Wetu

Mwananchi

NAIBU kiongozi wa upinzani bungeni, Dk Willibrod Slaa amesema serikali inachelea kuchukua hatua dhidi ya mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea kwa sababu inamwogopa na inamlinda kwa maslahi binafsi.

Kauli hiyo imetolewa wakati serikali bado haijatangaza hatua dhidi ya Dk. Hosea pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika ambao wametajwa kwenye kashfa ya utoaji zabuni ya ufuaji wa umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development LLC na serikali kushauriwa kuwachukulia hatua.

Katika taarifa ya utekelezwaji wa mapendekezo ya Bunge, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema wawili hao wameshaandikiwa barua za kutakiwa kujieleza, lakini hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa na mamlaka husika dhidi yao.

Akizungumza na Mwananchi jana, Dk Slaa alisema ukimya wa serikali kuhusu hatua dhidi ya Dk Hosea, ambaye taasisi yake ilieleza kuwa hakukuwepo na rushwa katika utoaji wa zabuni hiyo kabla ya kamati teule ya Bunge kubaini kuwepo kwa mchezo mchafu, ni ishara ya kumwogopa na kumlinda kwa maslahi binafsi.

"Kutokana na nyaraka za bunge kupitia kamati ya (mbunge wa Kyela, Dk Harrison) Mwakyembe, huyu Dk Hosea anahusika. Kitendo cha kuisafisha Richmond tu kinastahili awajibishwe kwa kuchukuliwa hatua. Nashangaa kwa nini Kikwete hachukui hatua," alisema.

"Serikali hii ni ya ajabu. Ina macho na masikio makubwa, lakini haisikii. Inasema inamchunguza, inachunguza kwa miaka mingapi."

"Hii inaonyesha jinsi serikali ilivyokosa utawala bora.

"Utendaji wa Rais Kikwete na serikali yake una mtia shaka kutokana na kufumbia macho na kutochukua hatua katika masuala mengi yaliyo wazi na yenye maslahi kwa taifa na hivyo kuacha maswali kwa wananchi.

"Ni wazi hakuna utawala bora bali ni kulindana kwa maslahi binafsi, nimeshasema mara nyingi hilo lipo wazi.

"Naamini Kikwete alielezwa kuhusu Richmond, cha kushangaza ni kigugumizi alichonacho kumchukulia hatua Dk Hosea.

"Haikuwa rahisi zabuni kubwa kama ile kutolewa kwa Richmond, wala mitambo mikubwa ya kuzalisha umeme kuingia nchini bila yeye (Kikwete) kufahamu, najua anafahamu sasa kigugumizi cha kuchukua hatua kwa Hosea anayestahili kuwajibika kwa kuisafisha Richmond."

Kuhusu Mwanyika, ambaye pia serikali ilisema inamchunguza, Dk. Slaa alisema alishatoa kauli yake na kumtaja aliyehusika.

Katika taarifa yake kwa Bunge kuhusu kampuni ya Richmond, Takukuru ilieleza kuwa uchunguzi wao ulibaini hapakuwa na rushwa katika utoaji zabuni kwa kampuni hiyo, jambo ambalo ni tofauti na taarifa ya kamati teule ya bunge iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Dk Mwakyembe.

Kamati ya Dk Mwakyembe, pamoja na mambo mengine ilibaini kuwepo kwa mazingira ya rushwa katika utoaji zabuni hiyo na ripoti ya kamati hiyo ilisababisha Edward Lowasa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu kutokana na kutajwa kwenye kashfa hiyo.

Kuhusu kauli ya Dk. Hosea kuwanyooshea kidole wabunge kuwa wanachukua posho zaidi kuliko uhalisia wa kazi wanayoifanya kwa wananchi, Dk.Slaa alisema mkurugenzi huyo wa Takukuru asitumie nafasi hiyo kisiasa kulipa kisasi na kuwashambulia wabunge.

Alisema kimsingi hana ugomvi na Dk. Hosea na kwamba ni jambo baya kwa mkurugenzi huyo iwapo amefanya hivyo kwa lengo la kuwaumbua na kuwanyamazisha wabunge kwa malengo yake binafsi.

"Asitumie nafasi yake kulipa kisasi... kuwanyamazisha wabunge. Asitumie nafasi hiyo kisiasa kutaka kuwashambulia na hata kuwaumbua wabunge," alisema Dk Slaa.
 
Moja ya mapungufu makubwa kwenye utawala wa JK ni kushindwa kwake kuwawajibisha wale wanaotuhumiwa kwenye vitendo vya kifisadi kama hao waliotajwa na Dr Slaa. Tatizo kubwa hapa naamini ni kitendo chake cha kuhusisha urafiki kwenye kuteua viongozi jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa kwenye utendaji wa kila siku. Asipojitahidi kutenganisha uswahiba na uongozi tusitarajie mabadiliko yoyote hata akipewa miongo miwili au zaidi.
 
Ndiyo maana hatufai kama Kiongozi hivyo hafai kugombea tena 2010. Rais muoga ni hatari sana kwa nchi yoyote ile ikiwemo Tanzania.
 
Mjomba kalamba sukari ya mafisadi sasa tawageukaje?
 
Hosea hawezi kuwajibishwa kwa vyovyote vile na serikali ya CCM -- anayo siri kubwa ya ufisadi wa wakubwa na yeye tu ndiye anayetakiwa kuwalinda. Amekuwa na tabia ya kuwakandamiza sisimizi wa rushwa akiwemo mwaandishi wa habari mmoja ambaye alimtegeshea mlungula wa laki mbili kwani alikuwa anafuatilia tuhuma moja ya rushwa dhidi yake (Hosea) wakati akiwa Deputy Director wa Takukuru. Alihakikisha kaenda jela miaka 3. Mwandishi huyo sasa katoka na karudi kazi yake ya uandishi.

Mapapa ya ufisadi yanayoiba mabilioni anayalinda -- sijui kwa Bwana Mungu wake atakwenda kusema nini kwa uonevu kama huu.
 
Slaa anaogopa nini kusema Wabunge ni kweli wanapata posho kama kuku wagonjwa kwani amesikika akiilalamikia feza inayolipwa wabunge ,sasa hapo angeliunganisha tu kuwa ni kweli na ameshalisemea kuliko kuonekana ana babaika.

Slaa alisikika akisema ..."Nchi hii wanasema ni masikini, fikiria kuna wabunge 320 walipwe posho wakiwa Dodoma 135,000 kwa siku, mwisho wa mwezi milioni saba ambazo ni kiasi kidogo tu kinakatwa kodi. Hili ni jambo la ajabu?Ebu tazama maisha ya Watanzania vijijini na wamuogope Mungu," alisema Dk Slaa.
Slaa hapo hana tofauti na kauli ya Horsea au mnaonaje ?
 
Mimi nina wasi na uongozi wote wa JK...na uoga wake,kuingia kwafedha kifisadi,hana ubavu kusema na kutenda....akiweza kumkamata RA na EL ataweza kumkamata na kumfukuza yeyote yule...ila kama hawezi kwa hao 2 Hosea atakaa pale hadi 2010.heri tumpe Magufuli maana ameonyesha angalau cheche kidogo tangu awe waziri...wengine wotemizigo tu...
 
Hosea atachukuliwa barua kwa mujibu wa taratibu, kwa sasa ngoja kwanza atekeleze wajibu aliopewa kwa na Rais Kikwete wa kuwashughulikia mafisadi. Ile ripoti ya kusafisha Richmond ilitoka kwa shinikizo. Sheria ya kudhibiti rushwa ili badilishwa baada ya hapo kumpa mamlaka zaidi na kumlinda dhidi ya mashinikizo. Sasa Hosea anachukua hatua

.............ndiyohiyo
 
Ndiyo maana hatufai kama Kiongozi hivyo hafai kugombea tena 2010. Rais muoga ni hatari sana kwa nchi yoyote ile ikiwemo Tanzania.

Wakuu wa CCM washajipanga kumpitisha kugombea kwa nguvu zote. hapa wananchi tunatakiwa tumpinge kwa nguvu zote pia ikiwemo kuandamana akichukua formu ya kugombea. Vinginevyo tuandike maumivu mpaka 2015
 
Hosea atachukuliwa barua kwa mujibu wa taratibu, kwa sasa ngoja kwanza atekeleze wajibu aliopewa kwa na Rais Kikwete wa kuwashughulikia mafisadi. Ile ripoti ya kusafisha Richmond ilitoka kwa shinikizo. Sheria ya kudhibiti rushwa ili badilishwa baada ya hapo kumpa mamlaka zaidi na kumlinda dhidi ya mashinikizo. Sasa Hosea anachukua hatua

.............ndiyohiyo
Mwenzetu tupo wote sayari hii hii?
 
Mimi nina wasi na uongozi wote wa JK...na uoga wake,kuingia kwafedha kifisadi,hana ubavu kusema na kutenda....akiweza kumkamata RA na EL ataweza kumkamata na kumfukuza yeyote yule...ila kama hawezi kwa hao 2 Hosea atakaa pale hadi 2010.heri tumpe Magufuli maana ameonyesha angalau cheche kidogo tangu awe waziri...wengine wotemizigo tu...

Hawezi kuwakamata hao maana alishirikiana nao katika dhambi walizozifanya ili kuhakikisha Kikwete anaibuka kama mgombea wa CCM.
 
Back
Top Bottom