Serikali inaogopa nini kufanya lugha ya kufundishia iwe kingereza kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu?

Serikali inaogopa nini kufanya lugha ya kufundishia iwe kingereza kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu?

Lengo lao ni kufanya watoto wa kimasikini waendelee kuwa masikini na wao watoto wao waendelee kuwa juu

Hakuna waziri Wala mkulugenzi yoyote katika nchi hii ambaye hajui kuwa kingereza ni lugha muhimu

Kipindi Dar es salaam hakuna English medium za private wao walikuwa na English medium zao Olympio na Bunge na watoto wote wa viongizi unaowajua wewe wamesoma katika hizo shule

Alafu nyinyi mnambiwa watoto wenu wasome primary Kwa lugha ya kiswahili Ili kudumisha uzalendo

Mtoto wa kimasikini anatoka kayumba anapelekwa secondary ya kata akiwa anapambana na lugha hapo mtihani wa kidato Cha nne huo anamaliza hapo hata kuomba maji Kwa kingereza hajui

Hapo Sasa chichiem ndio wanajisikia Raha maana wajinga wanaongezeka mitaani na ndio mtaji wao katika uchaguzi
 
Halafu hii nchi ina ubaguzi sana kielimu

Wabunge ,maraisi ,mawaziri wakiwemo wa elimu,majaji,viongozi wa taasisi za umma ,maprofesa hadi wa kiswahili nk watoto wao wanasomesha English Medium halafu watoto wa maskini wanataka wasome shule za mitaala ya kiswahili

Asante Mungu kwa kuweka Jehanamu ili hawa roho mbaya wanafiki wasiotaka watoto wa maskini shule za umma shule zao zisiwe English medium wapelekwe huko siku wakifa
 
Usisahau kukuza ajira kimataifa za walimu wa kiswahili hiyo ni kukuza uchumi pia kwa kuleta pesa za kigeni kwa ku export walimu wa kiswahili

Sasa hivi kuna soko kubwa mno la walimu wa kiswahili kinataifa lakini nafasi zote zinachukuliwa na wakenya sababu walimu wetu wa kiswahili wabovu kwenye kingereza uwezo wao mwisho kufundisha kiswahili Tanzania tu

Serikali iache ujinga imebadilishe mitaala iwe shule zote English Medium kiswahili kibaki kama somo tu kama kenya na kibaki kuwa lugha ya taifa tu

Kenya kingereza wanakiweza ba kiswahili wanakiweza
Mkuu sidhani kama kiswahili kinaweza kutuingizia fedha za kigeni jinsi unavyoiweka
Ila kama kufundisha kiingereza kuanzia kindergarten basi hapo itabidi serikali ijipange haswa maana inahitaji waalimu wa English nchi nzima ambapo hatuna kabisa
Wakiajiri kutoka Kenya au Uganda ni gharama kubwa mno
Kila kitu kinawezekana ila na mfuko uwe umetuna

Nimeona waalimu wengi wa shule za bongo kwa lugha ya wazungu kwa kweli ni changamoto sana
Wapo wanaongea vizuri na wapo hawajui kabisa
 
Uongo

Nenda shule zote za English medium zikizoko Tanzania na mtaani kwako au kijijini kuanzia chekechea walimu wanaofundisha waswahili wamesoma vyuo vya ualimu vya hapa hapa nchini tena vya serikali sio nje ya nchi

Walimu wapo wa kutosha ni kubadili tu mtaala basi hatuhitaji ku import walimu

Masomo yote sekondari na vyuo vya ualimu kasoro kiswahili wamesoma kwa kingereza
 
Umesema private school na sio za serikali ama
Sasa kwani hakuna somo la kiingereza mashuleni?
Mbona kijana wa form 4 hawezi kuongea
Hapo tatizo ni nini wakati wapo waalimu wa masomo.hayo
 
Basi hizo shule zingefundisha Kiswahili mwanzo hadi mwisho. Sio ghafla bin vuu, sekondari mtoto anakutana na lugha asiyoifahamu.
Tatizo la elimu yetu siyo lugha ya Kiswahili wala Kiingereza. Shida kubwa iko hasa kwenye miundombinu, vifaa/nyenzo za kufundishia na walimu mahiri na mazingira bora na wezeshi kwa walimu na wanafunzi.
 
Tatizo la elimu yetu siyo lugha ya Kiswahili wala Kiingereza. Shida kubwa iko hasa kwenye miundombinu, vifaa/nyenzo za kufundishia na walimu mahiri.
Katika hayo matatizo uliyoyaorodhesha, lugha pia ni mojawapo hata usikwepe. Huo umahiri mtu anautoa wapi ikiwa lugha inayotumika kuimpact huo umahiri haimudu?
 
Umesema private school na sio za serikali ama
Sasa kwani hakuna somo la kiingereza mashuleni?
Mbona kijana wa form 4 hawezi kuongea
Hapo tatizo ni nini wakati wapo waalimu wa masomo.hayo
Kijana wa four kushindwa kingereza tatizo linakuwa Hana msingi mzuri wa kingereza chekechea na primary

Ukisikia elimu ya msingi ya mhimu mno

Mtoto huweza ku master lugha sana akiwa mtoto mdogo.Ndio maana huitwa elimu ya msingi.Nyumba kujenga msingi unatakiwa kuwa imara sana

Huwezi kuacha mtoto unamsomesha kiswahili mfululizo chekechea miaka miwili halafu miaka saba primary jumla miaka tisa kiswahili kitupu halafu unataka amudu lugha ya kingereza kwa miaka minne ya sekondari uongo na utapeli na kumuonea
 
Katika hayo matatizo uliyoyaorodhesha, lugha pia ni mojawapo hata usikwepe. Huo umahiri mtu anautoa wapi ikiwa lugha inayotumika kuimpact huo umahiri haimudu?
Umeshawahi kusikia Inglishi ya wale vipanga wa hisabati na fizikia? Unaweza kucheka hadi upasuke.

Lakini shughuli yao kwenye masomo si ya kitoto. Same applies kwenye masomo mengine.

Lugha is very important, but should never be overrated.
 
Kijana wa four kushindwa kingereza tatizo linakuwa Hana msingi mzuri wa kingereza chekechea na primary

Ukisikia elimu ya msingi ya mhimu mno

Mtoto huweza ku master lugha sana akiwa mtoto mdogo.Ndio maana huitwa elimu ya msingi.Nyumba kujenga msingi unatakiwa kuwa imara sana

Huwezi kuacha mtoto unamsomesha kiswahili mfululizo chekechea miaka miwili halafu miaka saba primary jumla miaka tisa kiswahili kitupu halafu unataka amudu lugha ya kingereza kwa miaka minne ya sekondari uongo na utapeli na kumuonea
Hapo ndio watoto wanaanza kukariri sasa na wanatoka watupu
Ni kweli ukimuuliza atafsiri alichosoma hawezi kuelewa
Nimekuelewa
 
Back
Top Bottom