Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Video ya inayosambaa mitandaoni ya mwalimu wa madrasa huko Mbagala akiwapiga fimbo watoto wadogo ni mbaya sana. Hata hivyo ukisikiliza wanaochukua hiyo video wanasema siku nyingine huwa anawapiga mpaka hasira zake ziishe! Hii ni hatari kwa usalama wa hao watoto.
Kwa kumuangalia tu huyo mwalimu wa unaweza kuona ni kama mtu mwenye matatizo ya saikolojia lakini pia hana mbinu zozote za kufundisha watoto wadogo. Ni hatari sana kumuacha mtu wa aina hiyo na watoto wadogo.
Ni jambo lenye mashiko kwa serikali kuratibu mafunzo yoyote ya umma ya watoto wadogo kuanzia madrasa hadi madarasa ya kipaimara na komunyio. Serikali iweke vigezo vya msingi vya ujumla vya mtu kuwa mwalimu wa watoto wadogo ikiwemo kuwa na cheti cha mafunzo ya mbinu za kufundisha watoto wadogo kutoka vyuo vya ualimu.