DOKEZO Serikali inapata hasara ya mabilioni kwa watumiaji wa mifumo ya TEHAMA kulipia huduma isiyoendana na kiasi cha fedha kilicholipwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kuna jambo nimelifanyia utafiti nimegundua makampuni na mashirika ya umma yanaiba fedha nyingi sana serikalini. Kuna fundi nilimtuma akalipe huduma ya kuunganisha maji. Nakumbuka jumla ya fedha zilizoletwa kama bill kwenda serikalini ilikuwa zaidi ya laki saba na sabini na nane.

Nilimpa moja wa mafundi wangu wakalipie kile kiasi na baadaye nikaletewa karatasi kama uthibitisho wa malipo. Mtu mmoja akaniambia hapo mkuu umepigwa kama laki nne hivi, nikamwambia mbona nimepewa risiti ya malipo? Akaniambia nichukue control number iliyoandikwa kwenye karatasi niingie kwenye mfumo wa malipo ya serikali nione hiyo namba imelipia nini na kiasi gani.

Nilichogundua ni kwamba; ile control numba siyo ya shirika la maji. Imelipia huduma nyingine kabisa, nikafanya ufuatiliaji bila kusema , nilipokwenda kwenye mamlaka husika nikakuta malipo yaliyofanyika ni 254300 tu na control number ya malipo haya siyo ile niliyopewa.

Nilijaribu kufuatilia ila nikagundua wale mabwana wenye ofisi ya maji wanaelewa ule mchezo na ndiyo maana wameweka utaratibu wa watumishi wengi wasio na ajira rasmi ili unapowashtukia wakiambiwa huyo aliyefanya hivyo siyo mwajiriwa wetu ni mtoto mwenye njaa anajitolea. Lakini najiuliza hizi risiti zinazotolewa kinyume cha huduma siyo uhujumu uchumii?

Baada ya kutokea ule mchezo nimekuwa nafanya utafiti kwa huduma nyingi za serikali; napenda kusema kwamba tatizo lipo kwenye malipo ya leseni za udereva, leseni za biashara, kodi mbalimbali, TANESCO kuunganisha umeme, huduma za afya nk

Jambo lililofanywa na viongozi wa utumishi wa umma ili wapate fedha wameondoa ujumbe mfupi wa malipo kwenda kwa mteja. Mifumo hii ya malipo ilikuwa imeunganishwa na namba za simu za mteja na lazima hiyo namba iwe imesajiliwa kwa kitambulisho cha NIDA.

Viongozi na watumishi wameweka huduma nyingi zisizotoa uthibitisho wa malipo wa mteja anayetaka huduma badala yake wameruhusu hata namba za vishoka ziweze kupewa huduma.

Mimi kwa mfano naitwa Shebe Lule Kitwingila na nina namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina langu, kwanini mifumo ikubali kuandikwa namba za vishoka kwenye malipo ya awali? Kwanini bili za maji na TANESCO au kodi ya ardhi zinakwenda kwa namba ya mteja ila malipo ya awali bili zitengenezwe kwa namba nyingine?

Juzi kati hapa mlisikia mfanyabiashara aliyekuwa analalamika kwa mkuu wa mkoa; aliomba mifumo iboreshwe lakini sidhani kama watarekebisha kwa sababu wanufaika ni hao hao.

Wizi wa kutumia wrong control number ni mkubwa sana nchini na endapo kila mkuu wa taasisi ataamua kufanya ufuatiliaji watagundua kuna uhalifu mkubwa sana unaendelea.

Mwisho, nitoe wito wa kila mwenye malipo ya serikali au shirika waingie kwenye mfumo wa malipo ya serikali wafanye verification kama malipo yaliyofanywa kwa namba za malipo alizopewa ni sahihi?

Viwanja vingi vya serikali sasa hivi vinauzwa kwa wrong control number na upo uwezekano huko mbeleni tuendako tukaenda ardhi tukakuta fedha zilizopo kwenye risiti siyo zilizopo ardhi.

Watanzania amkeni acheni kuwapa watu wakawafanyie malipo kwenye nyaraka serious kama kununua ardhi, kuunganisha maji, TANESCO, leseni nk.....atakuja Rais mwingine hapa tutaanza kukamatwa kwa uhujumu uchumi....na utakosa haki kwani walipkuhudumia watakuwa wamestaafu.

Mwisho, taasisi zote ambazo wanatoa huduma ya malipo na hakuna feedback kwamba umelipia huduma ni wezi
 
Mkuu Asante kwa taarifa. Ungetaja na Mkoa ulipo patia hiyo kadhia ingekuwa bora zaidi.
 
Hiyo ni mkoa upi?
 
Kama kuna control number feki tena basi ujue ni mabillion yamechepushwa
 
Ukimtuma mtu kukufanyia jambo hayo ndo matokeo yake. Inategemea na uaminifu wake. Sasa hapo umelizwa na watu wa kati. Mambo ya msingi uwe unafuatilia mwenyewe.

Kimsingi hapa serikali haibiwi kitu, maana fedha zote zinazo stahili kulipwa zinakuwa zinalipwa. Ila wewe mteja ndo unapigwa cha juu na watu wa kati.

Siku zote kagua control number kabla hujalipa kupitia app ya GePG. Kila kitu kiko wazi.
 
Hii ni balaa.
 
Hata TRA wanaiba sana kwenye VAT returns.

Wanawaibia wateja wasiokuwa makini
 
Kupambana na ufisadi sio jambo la kuchekacheka na kuweka jokers kama akina Mwigulu na Nape kwenye nafasi nyeti.
 
Kuishauri hii serikali ni kama kutupa akili zako chooni!
 
Hiyo michezo nimeiona shirika la posta!!!

Kila mwaka tunalipa bill kwa shirika kupitia control number ila mwaka Jana nimeenda kuomba bill ikaja na deni la miaka 5 nikabaki kushangaa tu.

Nilivamia ofisi kwao na receipt zote wakalalama ohoo mbona ukuja na receipt kabla ya bill kutoka so hawawezi kubadilisha chochote coz control number imeshatoka.

Mpaka Leo nabaki kujiuliza inamaana system ya posta Haina kumbukumbu za wateja wao wanaolopa bill?
 
Umeiweka vizuri sana; tunalipa tukiamini tumelipa serikalini kumbe tumewalipa watu.

Na ukienda ofisini na uthibitisho wa malipo ni rahisi sana wale wale wanaopiga hizi fedha kukuambia tayari wametengeneza bill hivyo lazima ulipe.

Ukitaka kupeleka mashtaka yako vyombo vya uchunguzi kama polisi unaambiwa utawafukuzisha watu kazi bora ulipe tu

Watanzania tuamke la sivyo huko tuendako tutapata shida sana. Kibaya zaidi sms za malipo si rahisi kuzihifadhi kwa miaka
 
Unashangaa nini wakati hata wanaohubiri uzalendo ni wezi.
 
Umechelewa sana kulitambua hilo, kwa kifupi ni kwamba kwenye mifumo ya serikali kumejaa wezi.
 
Weka control number yenye risiti tuone mkuu,,,,,i mean weka bill na receipt yake,,,how is possible upewe bill ya idara ya maji halafu malipo yawe taasis nyingine....sababu bill huwa inaandikwa pia sababu ya bill.....maybe tutakua tunajifunza zaid ukiweka ushahid
 
Ili mumjue ni nani muanze kumsumbua?
 
Naungana naye hii michezo michafu inaanzia juu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…