Serikali inapokosolewa kwa Constructive Criticism, je, Ifuate Ushauri? Hongera Bunge letu tukufu kufuata ushauri na kutuondolea ubatili huu

Kulikuwa na ulazima wa kuandika majina ya Katibu wa bunge na Katibu mkuu wa CCM kwenye hiyo barua?
Mimi binafsi sioni kwamba kulikuwa na haja ya kuandika majina ya katibu wa chama.

Hapo Wanataka kuendelea kutuhadaa kwa kutuaminisha haya;

1. Kwamba hawakuwa wamekosea toka mwanzo hivyo tuone kuwa hakukuwa na tatizo kubwa kivile,

2. Kwamba bado mihimili yote ikiwemo bunge ionekane haiwezi kuwa na sauti, nguvu au maana kwa wananchi bila uwepo wa ccm.

3. Kwamba bado tupo katika Zama za chama kushika hatamu/dola.
 
Uandishi wa habari ni kazi kama kazi nyingine zote, waandishi wanaomba kazi na wanaajiriwa na kulipwa mishahara kama wafanyakazi wengine wowote. Waandishi walioajiriwa wanaitwa Press Journalists or media Journalists.

Waandishi ambao hawajaajiriwa wanaitwa Freelance Journalists.
Kwenye kundi la Freelance Journalists, kuna makundi matatu
1. Media Freelance Journalists, ni waandishi wa kujitegemea lakini wanaandikia media fulani as correspondents, hawa wanalipwa na hizo media.
2. Independent media Freelances - hili ni kundi la waandishi wa kujitegemea ambao hawako chini ya chombo chochote cha habari, hawa wanapeleka habari zao chombo chochote cha habari na hicho chombo kinawalipa.
3. Independent Media Freelance Volunteers, hili ni kundi la waandishi wa kujitegemea kwa kujitolea, hawa hawalipwi na media yoyote. Hawa wana shughuli zao nyingine za kuendesha maisha yao, lakini wanafanya uandishi wa habari kwa mapenzi tuu, just for the love of it. Hawalipwi, wanaandika habari bure kwa kujitolea, wanazisambaza bure kwenye media. Mimi ndio niko kwenye kundi hili. Naandika bure, nasambaza habari zangu kwenye
1. Vituo 8 vya TV, Vituo 10 vya Radio, Magazeti 10, na mitandao ya jamii lukuki ikiwemo jf. Nafanya bure, silipwi na media yoyote, ni mapenzi tuu.
P
 
Umeisahau CCM?
 
Barua mpya mbona haijasema kama inafuta barua ya awali?

Maana ndio utaratibu
 
Hii nchi Nani analiharibu kwa kukubali uvunjifu wa katiba na taribu waziwazi hivi?
Ni wakati gani Wana habari mnatakiwa kuwabarisha jamii kuhusiana na uvunjifu wa katiba kama ilivyo Sasa?
Kuna watu wapo kwenye sekta muhimu na nyeti sana lakini hawajitambui tu, mojawapo ya hao watu ni waandisi wa habari...hapa Tanzania ni mabogus ziro kabisa.
Wanastahili kuuliwa na kilufutwa kabisa, jinga kwelikweli.
 
Barua mpya mbona haijasema kama inafuta barua ya awali?

Maana ndio utaratibu
Ushauri wangu ni kwa vile the original letter was never on public, hivyo nikashauri marekebisho yafanywe kimya kimya, kwa kunyofoa na kupachika kimya kimya, hivyo hata ile taarifa kwa media iliyosema barua imepelekwa CCM, imeisha nyofolewa kimya kimya from Bunge Website.
Mambo ni kimya kimya.
P
 
Duh yaani unatuombea kifo!.
Huku ni kutupigia ramli chonganishi!.
P
 
Hakuna bunge hapo hilo ni genge la wahuni tupu
 
Kwa bahati mzuri, huwa nasoma katiba mara kwa mara! Na hapa wala sina sababu ya kufungua katiba kukuambia HAKUNA PAHALA POPOTE KWENYE IBARA YA 149 (1) (C) ILIPOTAJA HABARI ZA BARUA!

Swahili version imetaja TAARIFA, na newest version ambayo ipo kwa lugha ya mabeberu imesema NOTICE of Resignation!! So, utakuwa sahihi endapo BARUA = TAARIFA=NOTICE!

Kutokana na hilo, mwanzoni kabisa wakati Ndugai anajiuzulu nilisema wazi sioni kama Ndugai amekosea. haidhuru hata kama majority walisema kujiuzulu kwako hakukufuata katib!!

Na nilisema wazi kwamba mchakato wa kumpata Spika kwa mtu ambae ni mbunge unaanzia kwenye chama! Na chama kikishapitisha jina, anayewasilisha jina kwa Katibu wa Bunge ni chama chake na sio Mgombea Mteule kama isemavyo Kanuni #7(3) ya Bunge kwamba:-
Na ndo maana nikasema, kwa mchakato kama huo, Uspika wa mtu upo mikononi mwa chama zaidi kuliko kwa Katibu wa Bunge! Chama kikimfukuza uanachama, Uspika unafia hapo hapo hata kama Katibu wa Bunge ni mjomba wako!

Ni kutokana na hilo ndo maana hata anapolazimika kujiuzulu, mwenye haki ya kupata BARUA ni Chama kwa sababu ndicho kilimtuma akagombee na sio Katibu wa Bunge!! Kama ataandika na nakala kwa Katibu wa Bunge, well and good, Ibara ya 149(1)(c) INAMLAZIMISHA kutoa TAARIFA (na sio barua) kwenye bunge!!

Lakini kwavile suala la Spika lina public interest, ndipo kupitia barua ya kujiuzulu, Chama kitautaarifu umma kwa kutoa TAARIFA kwamba XYZ amejiuzulu! Na Katibu wa Bunge nae kwavile atakuwa amearifiwa kuhusu kujiuzulu kwa Spika, awe alipewa nakala ya barua au taarifa, nae atakachofanya ni kutoa TAARIFA kwa umma kwamba XYZ amejiuzulu Uspika!!

Unaanzaje kwa mfano, kuanza kupeleka barua kwa Katibu wa Bunge, and assume Katibu wa Bunge anakubali kujiuzulu kwako wakati aliyekutuma ukagombee Uspika ni chama?!
 
Waheshimiwa wepi?.
Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, naandika just for the love of it, naandika bure kwa kujitolea bure bila kulipwa na yeyote.
P
Unaishauri serilaki kupita uchochoro na unafurahi kuwa ni sikivu haya mkuu we ni mwanahabari ngulin
 
Kwa hiyo Bunge/Serikali kwa kushirikiana na Ndugai waneandika barua juzi na kurudisha tarehe nyuma ionekane iliandikwa Jan 6? Je, hili si kosa kisheria? Mbatia afungue kesi nyingine.
Barua ya marekebisho bila Shaka iliandikwa baada ya wiki 2 kupita, lakini tarehe ikawa hiyo hiyo 6 January! Kwa maana hiyo, hiyo ni barua ya kughushi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwa ni sawa serikali kusema uongo mahakamani? Huoni kuwa ni hatari nchi kuongozwa na viongozi wanaokosa uadilifu kiasi cha "kutengeneza" barua ya uongo na kuipeleka mahakamani?
 
Mkuu Chige, kwanza asante sana kwa mchango wako huu elimishi, maana ni kupitia michango kama hii, hutoa fursa ya kuelimisha wengine walio wengi wasiojua, kama jinsi wewe na hata Mwanasheria Mkuu wa serikali, asivyojua!. Lugha ya Kiswahili, ina upungufu mkubwa wa vocabulary, hivyo kunapotokea utata wa neno lolote la katiba ya Kiswahili, tafsiri rasmi huchukuliwa kwenye katiba ya Kiingereza. Hivyo neno "taarifa" kwenye katiba ya Kiswahili, sio taarifa yoyote, maana kutoa taarifa hata kwa mdomo tuu, ni taarifa, neno "taarifa" tafsiri ya taarifa kutoka katiba ya Kiingereza ni "notice", hivyo notice has to be in black and white!, yaani lazima iwe ni kwa maandishi!. Hiyo taarifa ya maandishi, ndio barua ya kujizulu, hivyo kusoma kwako koote katiba, hujaona neno barua, ila umeona taarifa, hivyo darasa la kwanza kwako na wengine wa type yako, taarifa ndio barua!.
Hapa unazungumzia vitu viwili tofauti, hapa unazungumzia mchakato wa kumpata Spika, ndio unaoanzia kwenye chama, jukumu la chama cha siasa ni kututeulia tuu mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa, jukumu la chama cha siasa, linaishia kwenye mapendekezo tuu ya mgombea. Kwenye ubunge, udiwani na urais, jukumu hilo linaishia anapopeleka majina ya wagombea wale NEC, NEC ikiisha fanya uteuzi wa wagombea wa udiwani, ubunge na urais, sasa wanakuwa ni wagombea rasmi wa uchaguzi wa umma, kwa udhamini tuu wa chama fulani, lakini wanachaguliwa na umma, na wakiisha chaguliwa wanakuwa ni madiwani, wabunge na rais wa umma, na sio madiwani, wabunge na rais wa CCM, hawakuchaguliwa na CCM, wamechaguliwa na umma wa Watanzania, hawawajibiki kwa CCM, wanawajibika kwa umma. CCM has nothing to do with wagombea wake waliochaguliwa. Hili somo nililitoa katika bandiko hili... The Doctrine ya Mwanasiasa Kuwa Maarufu Kuliko Chama!-Ni "Utumishi wa Watu VS Utumishi wa Chama!.
Vivyo kwa Spika, jukumu la chama cha siasa, ni kututeulia tuu mgombea, akiisha chukua fumu ya kugombea Uspika na kupitishwa, jukumu la chama cha siasa, linaishia hapo, sasa anakuwa ni mgombea wa Uspika wa umma, anachaguliwa na wabunge wa Bunge la JMT, hata kama wabunge wote ni wa CCM, Spika anayechaguliwa sio Spika wa CCM, ni Spika wa Bunge la JMT, hata kama atachaguliwa na wabunge wa CCM tuu, bado atahesabiwa amechaguliwa na Bunge la JMT, hata kama wabunge wote 100% watakuwa ni wana CCM, lakini atahesabiwa amechaguliwa na Bunge la JMT na sio Bunge la CCM, na baada ya Spika kuchaguliwa, anakuwa ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa CCM, na anawajibika kwa Bunge la JMT na sio kwa CCM, hivyo siku anajiuzulu, anajiuzulu kwa Bunge la JMT na sio kujiuzulu CCM.
Hapa you are wrong my friend, Spika ni Spika wa Bunge la JMT na sio Spika wa CCM, anawajibika kwa Bunge na sio kwa chama, hivyo akijuzulu uspika, anaandika kwa Bunge na sio kwa Chama!.

Kwavile ameupata Uspika kutokana na kudhaminiwa na chama kuwa mbunge, kisha akadhaminiwa tena kugombea Uspika, kama angajiuzulu uanachama wa CCM, hivyo kupoteza ubunge na uspika, hapo sasa ndio angeandika barua kwenye plain paper, sio headed paper ya Bunge, kumtaarifu Katibu Mkuu wa CCM kuwa amejitoa CCM, hivyo kutokana na kujitoa huko, amepoteza ubunge na Uspika, then hapo ndipo CCM ingekuwa right kulitaarifu Bunge, kuwa mwanachama wetu XYZ aliyekuwa mbunge na Spika, amejivua uanachama hivyo nafasi ya ubunge na spika zipo wazi. Au kama angafukuzwa uanachama wa CCM na hivyo kupoteza ubunge, na uspika, kutokana na vikao vya CCM, hapo ingekuwa sawa kwa CCM kuliarifu Bunge.

Naomba kuchukua fursa hii kukumbushia kuwa shurti la mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni kinyume cha katiba, kama nilivyo eleza hapa. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
Mgombea akiishachaguliwa anakuwa ni mtumishi wa umma, kitendo cha chama cha siasa, kumfukuza uanachama na hivyo kupoteza utumishi wake wa umma, ni kukifanya chama kupora mamlaka ya umma!.
Katiba ni ya umma, inapata mamlaka yake kutokana na umma, mgombea anaechaguliwa na umma, anawezaje kupoteza uongozi wa umma kwa kutimuliwa uanachama wa kakikundi fulani ka watu kanakoitwa chama?. Nani zaidi kati ya chama na umma?. This is wrong!.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…