Wanabodi,
Hii ni Nipashe ya Leo, 30.01.2022
View attachment 2100761
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huteremka na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" leo ni swali na pongezi. "Serikali inapokosolewa kwa constructive criticism, kama ushauri uliotolewa ni ushauri nzuri wenye maslahi kwa taifa, jee serikali ifuate ushauri huo, au iupuuzie kwa kushupaza shingo?. Hongera sana Bunge letu Tukufu kwa kufuata ushauri na kutuondolea ubatili katika Barua ya kujiuzulu Spika JYN!.
Kikawaida ni a being, ila sio human, hivyo serikali haiwezi kukosea jambo lolote, lakini serikali inaendeshwa na watu na inaongozwa na watu, human beings, watu hao wanaoongoza serikali ni binadamu na sio malaika, hivyo wanaweza kukosea, watu hao wanapokosea, inahesabika kuwa ni serikali ndio imekosea, hivyo serikali inapokosea au kwa kukosea yenyewe au kwa kukoseshwa, lazima ikubali kuwajibika kwa makosa hayo. Japo nimesema serikali kama serikali haiwezi kukosea, ila watendaji ndio wanaokosea na kuikosesha serikali.
Kila serikali inapofanya makosa, sometimes huwa kunatokea watu wenye jicho tunduizi, ambao wanaona makosa hayo na kuikosoa serikali kwa kutumia ukosoaji wa ujengaji (constructive criticism) ambao hufanyika kwa kuonyesha kosa lililofanyika na wakati huo huo kutoa mapendekezo ya jinsi ya kurekebisha makosa na kushauri a way forward kurekebisha makosa yaliyofanyika yasijirudie na maisha yaendelee. Naishauri serikali yetu tukufu, pale inapokosolewa kwa makosa ya wazi, kwanza isikasirike, pili ifuate ushauri na kurekebisha makosa na kujitahidi makosa kama hayo yasijirudie. Kitendo cha serikali kukubali kosa, not expressly but impliedly kwa kurekebisha kosa bila kukiri kosa, kwa kupokea ushauri, sio udhaifu ni uimara, na kuonyesha serikali yetu ni serikali sikivu.
Moja ya makala yangu ya nyuma, nilishauri, viongozi wa kisiasa na wa serikali, wanapofanya makosa ya wazi na kuifanya serikali ionekane imekosea, wanapaswa kwanza kukubali makosa, kuomba msamaha na kuwajibika. Hiki ndicho kilichofanyika kwa Spika aliyejiuzulu, Mhe. Job Ndugai,
Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere? kwanza alikubali makosa, kisha akaomba msamaha, japo msamaha wenyewe ulikuwa ni msamaha batili
Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu!
akidhani atasamehewa, na baada ya kuomba msamaha huo batili, sisi waona mbali tukashauri,
Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away? na baada ya shinikizo, ndipo JYN akakubali kujiuzulu ila huku nako alikurupuka na kuandika barua batili, hatukukaa kimya,
Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away?
Taarifa ya kujiuzulu uspika ya Spika Mhe. Job Ndugai kwa vyombo vya habari, iliyosambazwa na ofisi ya Bunge, ni hii
View attachment 2100870
Taarifa hii ya Ofisi ya Bunge kwa vyombo vya habari, illionyesha Spika Ndugai ameandika barua ya kujiuzulu na kuilekeza kwa Katibu Mkuu wa CCM na nakala ofisi ya Bunge. Msemaji wa Katibu Mkuu wa CCM akakiri kuipokea barua hiyo, na Ofisi ya Bunge ikakiri kupokea nakala ya barua hiyo kutoka CCM.
Taarifa hiyo ya kujiuzulu ilisababisha mjadala mkubwa wa kwanini ipelekwe CCM badala ya ofisi ya Bunge kama katiba inavyoelekeza. Mjadala huo ulihitimishwa na taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa alichokifanya Spika Ndugai kuandika barua CCM badala ya Bungeni ni sawa tuu. Mimi nami nikaweka ukosoaji wangu ila ukosoaji wangu ulikuwa ni a constructive criticism kwa kukosoa na kushauri kitu sahihi cha kufanyika.
Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge?
Mimi nilisema jambo fulani likielekezwa na katiba namna ya kufanyika, hakuna tena mjadala lifanyikeje, ni lazima lifanyike kwa jinsi ile ile katiba ilivyoelekeza, likifanyika kinyume, linakuwa ni batili au batilifu. Hivyo nilionyesha kifungu cha katiba kinachoekeza Spika akijiuzulu barua yake ya kujiuzulu inaandikwa kwa nani.
Ibara hii ya 149 1 (c) ya Katiba imeelekeza Spika akijiuzulu, ataandika barua kuliarifu Bunge. Kitu kikiishwa elekezwa na katiba namna ya kufanyika, kikifanyika kwa namna nyingine yoyote kinyume cha katiba, kitu hicho ni batili. Kujiuzulu halali ni kuandika barua kwa mamlaka yako ya uteuzi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Spika kwa vyombo, imearifu ameandika barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM na copy kwa Katibu wa Bunge. Katiba imeelekeza barua ya kujiuzulu Spika, itatumwa kwa Bunge. Kitendo cha Spika kuandika barua na kuituma kwa CCM kabla ya Bungeni, kumeifanya Barua ya Spika kuwa Batilifu, Bila huo ubatilifu kuondolewa, then barua hiyo imekuwa ni barua barua batili!. Katibu Mkuu wa CCM ametoa taarifa ya kupokea barua ya kujiuzulu Spika na tayari ameliarifu Bunge kuhusu kujiuzulu huko, na Bunge limeipokea taarifa hiyo b
atilifu hivyo hivyo ubatili wake na kuikubali. Huu ni ubatili!. Kama Bunge ndio mhimili wa kutunga sheria, Bunge lisipofuata katiba kwa kuukubali ubatili, nani atafuata katiba?.
Haki ya CCM Kupokea barua ya kujiuzulu, ni kama Mhe Spika JYN angejiuzulu uanachama wa CCM, hivyo kupoteza ubunge wake na uspika, ndipo CCM ingeliarifu Bunge.
Jee tuliruhusu Bunge letu tukufu kukumbatia ubatili katika madogo, jee ubatili huu ukihamia katika makubwa, nani atakuwa na jeuri ya kulihoji Bunge?
Hivyo nilitoa ushauri ufuatao
- Japo Spika Mhe. JYN tayari ameisha jiuzulu uspika, kujiuzulu huko, japo ni kujiuzulu batilifu, kufuatia taarifa kupelekwa mahali kusikohusika, lakini kujiuzulu ni kujiuzulu tuu, yaani Spika Ndugai ameishajiuzulu, lakini kwa kuheshimu katiba, lazima ubatili katika barua yake ya kujiuzulu uondolewe kwa kuandikwa barua rasmi kwa mujibu wa katiba.
- Kwa vile tayari CCM imeisha kiri kuipokea barua ile batilifu, Bunge nalo limekiri kuipokea barua kutoka CCM, marekebisho ya kuondoa ubatili huu, yafanyike kimya kimya. Spika mstaafu aelekezwe kuandika barua nyingi na Bunge lipokee kimya kimya barua mpya ya kujiuzulu kwa Spika iliyoandikwa kwa mujibu wa katiba, for filing kisha Bunge ndio litoe copy kwa CCM.
Kufuatia ubatili huu, Kiongozi wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, amefungua shauri Mahakama Kuu kuupinga ubatili huu, serikali ikaleta mahakamani barua rasmi ya Spika Ngugai kujiuzulu Uspika, ambayo imeonyesha Spika Ndugai, amejiuzulu kwa mujibu wa katiba, ni hii
View attachment 2100876
Barua hii ni utekelezaji wa ule ushauri wangu wa iandikwe barua nyingine kimya kimya na kuireplece ile barua batili. Barua yenyewe rasmi sasa ndio hii, na ndiyo iliyopelekea shauri la Mbatia kutupwa!. Japo ile taarifa ya kujiuzulu batili imeoishaondolewa kwenye website ya Bunge, lakini taarifa za CCM kuipokea barua batili ile ziliishatolewa na Bunge kuipokea barua batili ile ziliisha tolewa, ila ukienda kwenye files, hukuti tena barua batili, sasa utakutana na barua halali.
Natoa wito wa dhati kwa Serikali yangu, kukosea makosa madogo madogo is not a sin, to err is a human nature, kunapotokea makosa madogo madogo kama haya, na serikali kukosolewa, ni vitu vido tuu vya kurekebisha makosa na maisha yakaendelea. Serikali yetu ingekuwa inakubali makosa na kufuata ushauri, hii sintofahamu yote hadi kufikishana mahakamani, tusingefika huku kote. Hili jambo lilikuwa ni jambo dogo tuu, baada ya Bunge kutoa taarifa ya kujiuzulu kwa Spika Ndugai ikionyesha ameandika barua CCM, badala ya Ofisi ya Bunge, Bunge lingetoa taarifa ya pili kuonyeshea kulifanyika kosa dogo kwa barua kuelekezwa CCM, badla ya Ofisi ya Bungena kuonyesha kuwa Barua imeandikwa kwa Katibu wa Bunge na copy ndio kupalekwa CCM.
Unapokosoa kwa kuandika na kushauri, kitu cha kufanyika, halafu ukaona ushauri wako umefuatwa kama ulivyo, na makosa yamerekebishwa kama ulivyoshauri, huna budi kuandika tena na kutoa pongezi kwa serikali yetu kuwa ni serikali sikivu na kuuondoa ubatili ule, hivyo hapa nalipongeza Bunge letu Tukufu kwa kuondoa ubatili wa Barua ya Kujiuzulu kwa Spika Ndugai sasa imefuata katiba. Hongera sana kwa hili.
Sasa kumebakia ubatili mmoja tuu wa Naibu Spika, ajiuzulu kwanza nafasi ya unaibu Spika kabla ya kugombea Uspika na akiisha jiuzulu uNaibu Spika, ndipo angombee Uspika.
Nawatakia Jumapili Njema.
Wasalaam
Paskali