Serikali inapokosolewa kwa Constructive Criticism, je, Ifuate Ushauri? Hongera Bunge letu tukufu kufuata ushauri na kutuondolea ubatili huu

Barua ya marekebisho bila Shaka iliandikwa baada ya wiki 2 kupita, lakini tarehe ikawa hiyo hiyo 6 January! Kwa maana hiyo, hiyo ni barua ya kughushi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hapana, ile sio barua ya kughushi, kama mwandishi ni wewe, ukiandika mwanzo, ukakosea, uka withdraw na kupeleka barua sahihi, sio kughushi, hoja za kisheria kuhusu barua ile nimeizungumza kupitia kitu kinachoitwa, halali, batili na batilifu. Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge?
Barua ya kwanza ilikuwa batilifu, kwenye ubatilifu ubatilifu ukiondolewa inakuwa halali bila kughushi chochote!.
P
 
Kwa ni sawa serikali kusema uongo mahakamani? Huoni kuwa ni hatari nchi kuongozwa na viongozi wanaokosa uadilifu kiasi cha "kutengeneza" barua ya uongo na kuipeleka mahakamani?
No sio barua ya uongo, ni barua ya ukweli, kwasababu hakuna yoyote aliyeiona ile barua ya mwanzo zaidi ya kuhadithiwa kwenye ile press release ya Bunge. Mahakama inafanyia kazi, kile kitu kilicholetwa mbele yake, kilicho pelekwa mbele ya mahakama ni barua, bonafide genuine.
P
 
Asante sana Mayalla kwa udadavuzi wako kwa Katiba ya Jamhuri...

Pamoja na kwamba shauri la Mbatia lilitupwa ila binafsi naona Mbatia ndio mshindi maana amewafanya wafanye vile katiba inataka.
 
Mahakamani kuna sheria tu, ukweli na haki havipatikani mahakani. Swali ni je ile press release ya bunge ilitolewa na mwendawazimu? Kwanini sasa wanazidoa kwenye website yao? Wanasheria mnapenda kujiita wasomi ila msomi asiyejiuliza maswali ni mjinga japo amekaa darani
 
Mkuu Gulwa, kwanza heshima kitu cha bure, makosa ya kibinaadamu ni kitu cha kawaida kwenye maisha, usiite watu wendawazimu kwa human mistakes hata Press Release za Ikulu sometimes zinamakosa madogo madogo.

Ile Press Release ya Bunge iliyosema barua imepelekwa CCM ndicho Chanzo cha yote, hivyo baada ya marekebisho, hiyo taarifa lazima iondolewe, hivyo imeisha ondolewa kwenye Website ya Bunge.
P
 
Mkuu, kwamba mahakama imepata nyaraka iliyofichika ambayo. Hata Job ndugai hailewi.. imewasilishwa na nani?
Kwa kifupi mahakama ingetakiwa ifanye kazi kikatba then spika hakiri kutokufuata utaratibu wa kujiuzulu .... na hapewe nafasi upya ya kuita press. Ndipo harusiwe kujiuzulu mamna sheria inavyotaka ..
Wenda ndugai haelewi taratibu, namna spika anavyojiuzulu .
 
Ni kuchanganyikiwa tuu,
na tuliisha muombea msamaha Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!
hayo marekebisho yamefanywa na JYN mwenyewe ila hawakuandaa Press Release nyingine, the document is authentic bonafide genuine.
P
 
Hii the so called Barua rasmin ni Ubatili Mtupu
Imeandikwa baada ya Mbatia ku file kesi, tena huenda hata hakaandika Ayubu Mwenyewe
 
Ile Press Release ya Bunge iliyosema barua imepelekwa CCM ndicho Chanzo cha yote, hivyo baada ya marekebisho, hiyo taarifa lazima iondolewe, hivyo imeisha ondolewa kwenye Website ya Bunge.
P
Sema walikosea.
Na walirekebisha baada ya kukosolewa.
Chukua credit were due.
Tusonge mbele kuisaka Katiba Bora!
 
Ile Press Release ya Bunge iliyosema barua imepelekwa CCM ndicho Chanzo cha yote, hivyo baada ya marekebisho, hiyo taarifa lazima iondolewe, hivyo imeisha ondolewa kwenye Website ya Bunge.
P
Press release ilipaswa kueleza barua imewasilishwa kwa katibu wa Bunge

Bunge lina wanasheria waliopaswa kumshauri Spika Ndugai nini cha kufanya katika mkanganyiko

Mh Mbatia alieleza nia ya kwenda Mahakamani kufuatia press release. Katika mazingira ya kawaida kama barua ilikuwepo ingetolewa bila kusubiri na kupoteza muda wa kuitoa Mahakamani

Hata kama Ndugai angechelewa kuipeleka , busara ilikuwa kutoka na kuomba radhi, au basi kueleza tu kuwa amepeleka tena kwa katibu wa Bunge katika tarehe tofauti.
Kumbuka 'Ndugai had nothing to lose''

Kwa ushauri wako bw. Pascal ni mzuri kwa nchi zisizofauta taratibu kama Tanzania.

Laiti ingalikuwa nchi nyingine tayari kungekuwa na harufu ya ''forgery' kwa maana kwamba uchunguzi ulitakiwa kubaini ni lini barua ilisajiliwa kwa Katibu wa Bunge

Kama ingebainika hakuna tatizo umma ungejulishwa.

Ingebainika kuna 'ushauri wa pascal uliofanyiwa kazi'' watu wangepukutishwa akiwemo katibu wa Bunge kwa kukubali barua iliyoghushiwa tarehe ya usajili na pengine kutumika mahakamani.

JokaKuu
 
Hivi Ndugai kesho akigeuka na kusema yeye hajawamhi kujiuzuru uspeaker,

Ya lipumba Yana weza jirudia.

Nadhani hizi barua zote wameandika kitengo.


Sema mafao ni makubwa mno kwa speaker kuleta choko choko.
 
Hii the so called Barua rasmin ni Ubatili Mtupu
Imeandikwa baada ya Mbatia ku file kesi, tena huenda hata hakaandika Ayubu Mwenyewe
Barua ya mwanzo ndio ilikuwa na ubatili, barua hii ya sasa is perfekt.
Kuondoa ubatilifu kunaweza kufanywa vyovote.
P
 
LOL! This's so funny, brother...

Man, hili ni suala la Kikatiba, Kanuni za Bunge na Sheria zilizotungwa na Bunge!! Wakati msingi wa suala zima ndo huo niliousema, wewe katika kujenga hoja zako, umeunga unga tu maneno kwa kutumia hisia badala ya kuangalia katiba/sheria/kanuni zinasemaje!

Na hata ulipojaribu kutumia katiba, umeeleza tofauti na katiba inavyosema.
Kwa hili ndugu yangu HAKUNA upungufu wowote wa misamiati!
Nani kasema "taarifa yoyote" na hata ya mdomo ni taarifa?!

Hicho unachoona kwamba ni sahihi kwa mujibu wa maelezo yako hapo juu, ndicho nimefanya, unless kama HUKUSOMA post yangu, au kama hukuisoma kwa vituo!

Nimekuambia, na hapa narudi kwamba, kwenye katiba HAKUNA popote palipoandikwa neno BARUA bali TAARIFA! Na nikaendelea kukuambia kwamba,
na newest version ambayo ipo kwa lugha ya mabeberu imesema NOTICE of Resignation!!
Na ibara mzima inasema:-
SWAHILI VERSION:-

ENGLISH VERSION:-

Haya, niambie sasa hilo neno BARUA umelitoa kwenye katiba ipi? Unaweza kuweka ibara husika hapa?!

Au unaamini kabisa kwamba hakuna msamiati wa neno NOTICE, na ndo maana Kiswahili Version imeandika TAARIFA, kumbe according to you, NOTICE SIO TAARIFA BALI BARUA... Ndicho unachojaribu kusema?

Au Notice inakuwa barua pale inapotolewa kwa maandishi na kuwekwa sahihi kwa mkono? Hicho ndicho unachojaribu kutuelimisha?!

To be honest, siwezi kuwa na ujasiri wa kukupinga moja kwa moja kwamba sio kweli, na ndo maana kwenye post yangu nilikueleza kwamba:-
So, utakuwa sahihi endapo BARUA = TAARIFA=NOTICE!
Can you SINCERLY AND PUBLICLY declare kwamba Notice ni Barua?

Hebu angalia screenshot ulizoweka mwenyewe... screenshot ya kwanza na ya pili! Hivi hata kwa kuangalia tu huwezi kujua hapo taarifa ni ipi na barua ni ipi?

REMEMBER: Kama hoja ni nyaraka husika kutolewa kwa maandishi na kuwekwa sahihi kwa mkono, ZOTE hizo zimetolewa kwa maandishi na kuwekwa sahihi!

Kabla hatujaendelea na hayo mengine, hebu jibu hayo maswali hapo juu, manake nachelea nikiandika sana, utashindwa kunisoma kwa vituo kama inavyoonesha hukufanya hivyo kwenye post yangu ya msingi!
 
Mwana haramu ameishapita
 
Mkuu Nguruvi3, kwa vile barua rasmi ya kujiuzulu was not a public document, bandiko hili ni la Hypothetical situation only kwamba barua ni authentic bonafide genuine, ila ile Press ya JYN ndio ilikosewa, CCM ikakosea kusema imepokea barua badala ya kupokea copy na Bunge likasema imepokea copy kutoka CCM badala ya barua kutoka kwa Spika, kwa vile mahakama inafanya kazi na document iliyowasilishwa mezani, then document ya kujiuzulu uspika iliyowasilishwa mezani ndio document halisi, an authentic copy of the original, bonafide genuine.
P
 
Mkuu Chige, usikuze mambo, notice ni barua!.
Hata kama katiba haijasema neno barua, the notice of Resignation ni barua ya kujiuzulu.
P
 
Mkuu Chige, usikuze mambo, notice ni barua!.
Hata kama katiba haijasema neno barua, the notice of Resignation ni barua ya kujiuzulu.
P
Kukuza mambo tena?!

Ukileta mambo ya eti usikuze mambo ndo unaishia kutoa maoni yako binafsi tofauti na maandiko yanavyosema!

Anyway, mimi sio mtaalamu wa haya mambo, na sikuona yeyote wa kumuuliza anifafanulie, zaidi ya Google. Huko nikitafuta source ambayo inaonekana kuwa decent traffic kwa imani yangu kwamba, a source with crap contents haiwezi kuwa na decent traffic.

Kwavile nimefundishwa na kuandika barua tangu shule ya msingi, nikalazimika kuuliza tu hivi FORMAT ya NOTICE inakuwaje kuwaje hasa, na nikajibiwa hivi:-


Haidhuru hata hkama hutaki kukuza mambo, na kwavile notice ni barua, je unaweza kueleza hapa hiyo hapo juu pia ndo format ya barua? Au haya mambo ya format haya-determine kama nyaraka husika ni barua au vinginevyo, na kwahiyo ili mradi nyaraka husika imeandikwa na kusainiwa, basi automatically inakuwa barua.

Ngoja niendelee kukuza mambo kidogo kwa kuwa-refer wenye Kiingereza chao:-


NOTICE NI BARUA....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…