Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Serikali ya Tanzania inatafuta muwekezaji wa kukifufua kiwanda cha kutengeneza matairi kilichopo jijini Arusha cha General Tyre kuhudumia soko la ndani na kanda.
Uhuishaji wa General Tyre East Afrika(GTEA) kilichoanzishwa miaka 55 iliyopita unalenga uzalishaji wa matairi milioni moja kwa mwaka kwaajili ya vyombo vya moto.
Ripoti kutoka wizara ya viwanda na biashara kupitia NDC mwezi June wamesema muwekezaji mpya atakodi kiwanda kwa miaka 33 ikijumuisha makubaliano ya kuongeza mkataba.
GTEA ilianzishwa mwezi Februari mwaka 1969 chini ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na General Tyre ya nchini Marekani kikiwa na uwezo wa kuzalisha matairi 320,000 kwa mwaka wakati huo.
Kilianza shughuli zake mwaka 1971 lakini kilisimama mwaka 2007 kutokana na ushindani sokoni ambapo kulijaa matairi nafuu kutoka nje hasa nchini China.
Pia, soma=> General Tyre: Is it a slow death to a once an East Africa Giant??
Mwaka 2012 General Tyre ilifanyiwa ukarabati na ilitarajiwa kingeanza uzalishaji mwaka 2013 na NDC walipewa kazi ya kuifufua ambapo walianza kukarabati miundombinu ya umeme, jengo la utawala na matengenezo mengine.
Pia, soma=> General Tyre [EA] Ltd kuanza uzalishaji mwaka 2013
Ilipoingia Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli, Mwezi March 2016 Serikali ilichukua hisa zote za General Tyre na kusema wako mbioni kukifufua. Waziri wa viwanda na biashara wakati huo, Charles Mwijage alisema Serikali ilikuwa mbioni kuanza uzalishaji.
Serikali ilizinunua tena hisa zake asilimia 26 mwaka 2015 kwa shilingi bilioni 2.1 kwa Continental AG ilizouza miaka ya nyuma.
Pia, soma=> Serikali yachukua hisa asilimia 100 katika kiwanda cha General Tyre
Miezi mitano baadae, Agosti 2016 Serikali ilikacha mipango yake ya kukiendeleza kiwanda cha General Tyre na kusema imejipanga kujenga kiwanda kipya cha matairi. Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda, Dkt. Adelhem Meru aliiambia kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali(PAC) kiwanda kipya kitajikita kwenye teknolojia mpya.
Meru alisema kiwanda kipya kitakuwa mbadala ya General Tyre na hakuna mpango wa kuifufua General tyre kutokana na mashine za kizamani zilizotumika.
Pia, soma=> Serikali kujenga kiwanda kipya cha matairi, kuitosa General Tyre ya Arusha
Mwaka 2017 waziri wa Fedha wa wakati huo, Philip Mpango alisema Serikali ilitenga bajeti kwenye mwaka wa fedha 2017/18 kwa ajili ya kukifufua kiwanda cha matairi cha General Tyre, ikiwa ni miaka saba sasa mpango husika ulishindikana kuingia kwenye utekelezaji.
Pia, soma=> Bungeni: Waziri Mpango asema Serikali imetenga bajeti 2017/18 kufufua kiwanda cha General Tyre