Serikali inatoza VAT kubwa kuliko wanavyosema, nashauri kusiwe na VAT kwenye huduma

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) ni kodi ambayo inatozwa kwenye ongezeko la thamani ya bidhaa katika kila hatua ya uzalishaji hadi kuuzwa. Hata Mamalaka ya Mapato Tanzania(TRA) wameweka maana inayofanana na hii. Kabla sijaenda kuipinga kwanza nielezee namna VAT ipo theoretically

Mfano

Mkulima kanunua bidhaa kwa Tsh 100, akaenda kuuza kwa Tsh 120, Hapo ongezeko la thamani ni Tsh 20 ambayo ndio itakatwa 18% ikiwa bidhaa ipo chini ya bidhaa zinazokatwa VAT, Maana yake serikali itakusanya ni Tsh. 3.6

Hapo utaona ya kwamba ili VAT iweze kukusanywa kiusahihi kwanza lazima muuzaji awe na risiti za alikonunulia na risiti aliyouzia ili serikali ichukua VAT vinginevyo VAT haitaweza kuonekana au watabaki kukadiria kama hali ilivyo
NB: Kumbuka kuwa VAT haizidi 18% kwa bidhaa zote za ndani na za nje kwa mujibu wa TRA tembelea kiunga hiki HAPA

Hali ilivyo sasa hasa kwa huduma, VAT ni tatizo kubwa sana kwa kua huduma nyingi hazina sehemu ya awali ambako zinatokea, mathalani Consultancy, Ada za Shule, Malipo mbalimbali ya huduma za serikali nk
Angalia mfano wa Kifurushi,

1.png

Kodi hiyo ukiingalia sio tu ni kubwa, bali pia sio kodi ya ongezeko la thamani kwa kuwa
305.08 ni 18% ya Tsh. 1694.88 maana yake ni kuwa mtandao huo umenunua airtime kwa Tsh 305.11 na kuongeza 1694.888 ili kuuza kwa mtumiaji wa kawaida.

Kwa hesabu hizo utagundua kuwa si kweli kwa kuwa mnyumbulisho umeonesha kuwa 1694.92 ndio bei halisi na 305.08 ni ongezeko la thamani, which means kodi ilibidi iwe 54.92 ambayo ndio 18% ya 305

2.png

Aidha ukiangalia hii nyingine Gharama ni Tsh 1000, VAT ni 152.54. Lakini hiyo VAT tukiamini kuwa ni 18% basi imekatwa kutoka kwenye 858.5555 kitu ambacho hakiendi sawa

Hitimisho

VAT inaonesha kuwa inakatwa kwenye bei halisi na sio Ongezeko la Thamani kama wanavyosema

Nimeeleza awali kuwa VAT ni kodi ya ongezeko la thamani hivyo kunahitajika risiti ya ufahamu bei ambayo kitu kilinunuliwa na bei ya kitu kinapouzwa ili tofauti itozwe kodi. Hali hii ya kuhitaji risiti awali inafanya moja kwa moja huduma zisiweze kutozwa kodi kwa kuwa huduma nyingi zinaponunua vitu hunua kama ‘end user’ sio intermediate na huduma anazotoa hazina zinakotoka, I.e Daktari ananunua vifaa kama end user yeye haviuzi, huduma anayoitoa haiwezi kuwa na risiti ya awali. Hii ni tofauti na anayeuza dawa ambaye amenunua sehemu kwa jumla na anaenda kuuza kwenye duka lake

Kwa Point hiyo nasema, VAT inatozwa sehemu kubwa, pia Huduma zisitozwe kodi ya Ongezeko la Thamani
 
Hua nawaza tanesco ni ya serikali na VaT ni ya serikali hivi hiyo vat si upigaji tu kwa Mwananchi?
 
Wewe uoni ikiwa hivyo unavyotaka udanganyifu utakuwa mkubwa, hesabu yako ni ya kichina hauwez kutumika nchi nyingine
 
VAT kodi ya ongezeko la thamani, sasa unajuaje ongezeko la thamani kwenye huduma?

Suala la risiti linasisitizwa kwa kuwa ndio linasaidia kukokotoa VAT

Ulinunua kitu kwa TSh. 1000 ukauza kwa TSh 1200, ongezeko la thamani ni 200, then wanakata 18% yao.

Ndio maana unaambiwa unaisaidia serikali kukusanya hela yake...
 
Tanzania tunacalculate vat vibaya sana. Halafu vat ya tz tunakadiriwa mno. Yaani kisheria inatakiwa bidhaa ikuzwa 10000 inatakiwa wewe muuzaji upandishe bei iwe 11800 maana yake ni 10000 ni yako na 1800 ndio ya serikali. Hizo hesabu za kodi wanaweza wahindi na waarabu kwakuwa wanamitaji mikubwa na wanajua kucheza na mahesabu.

Ok hesabu ya kifurushi ni hivi. Vat ya mitandao ya simu ni 18%. Kwa hiyo bando la 1000 ilitakiwa liuzwe 1180. Ila mitandao ya simu wakainclude vat ndani. Yaani bei halisi ni 100%+ vat 18% na jumla inakuwa 118%. Kiufupi bando la 1000 bei yake ni 847.46. Sasa nije kwa uhalisia kweli kwa biashara za kibongo zilivyongumu na watu wanavyolia kupunguziwa bei je nirahisi kufuata hesabu hiyo.

Mfano: unauza nguo ukipiga hesabu ya gharama zote na faida bei ni 10000 ila inabidi uuze na vat ya 18% kwa hiyo inabidi uuze kwa 11800 ok tufanye 12000 au upandishe iwe 20000 ili mtu akipungua afike 15000 ili usikose vat ya kulipa. Ila unajikuta haujauza kama wiki nzima na unanjaa ya hela na familia inakutegemea na mtu anasema atanunua kwa 10000 na atachukua nguo 20 unalegea tu halafu unamwambia risiti sikupi ili usije sumbuliwa na tra. Kisha unauza unachukua hela unaendelea na harakati zako. Hao tra wakija watakupelekesha balaa. Ila ndio hivyo watu tunavyopambana. Ngoja niishie hapo tupate na maoni ya wengine.
 
Tanzania tunacalculate vat vibaya sana. Halafu vat ya tz tunakadiriwa mno. Yaani kisheria inatakiwa bidhaa ikuzwa 10000 inatakiwa wewe muuzaji upandishe bei iwe 11800 maana yake ni 10000 ni yako na 1800 ndio ya serikali. Hizo hesabu za kodi wanaweza wahindi na waarabu kwakuwa wanamitaji mikubwa na wanajua kucheza na mahesabu.

Ok hesabu ya kifurushi ni hivi. Vat ya mitandao ya simu ni 15%. Kwa hiyo bando la 1000 ilitakiwa liuzwe 1150. Ila mitandao ya simu wakainclude vat ndani. Yaani bei halisi ni 85%+ vat 15% na jumla inakuwa 100%. Kiufupi bando la 1000 bei yake ni 847.46. Sasa nije kwa uhalisia kweli kwa biashara za kibongo zilivyongumu na watu wanavyolia kupunguziwa bei je nirahisi kufuata hesabu hiyo.

Mfano: unauza nguo ukipiga hesabu ya gharama zote na faida bei ni 10000 ila inabidi uuze na vat ya 18% kwa hiyo inabidi uuze kwa 11800 ok tufanye 12000 au upandishe iwe 20000 ili mtu akipungua afike 15000 ili usikose vat ya kulipa. Ila unajikuta haujauza kama wiki nzima na unanjaa ya hela na familia inakutegemea na mtu anasema atanunua kwa 10000 na atachukua nguo 20 unalegea tu halafu unamwambia risiti sikupi ili usije sumbuliwa na tra. Kisha unauza unachukua hela unaendelea na harakati zako. Hao tra wakija watakupelekesha balaa. Ila ndio hivyo watu tunavyopambana. Ngoja niishie hapo tupate na maoni ya wengine.
HApa wewe ndio umeelewa concept yangu...

Concept ya VAT tuliyonayo haipo kwenye uhalisia
 
Vat ni value added tax ni kodi ambayo wewe mfanyabiashara unatakiwa ukusanye kwa niaba ya serikali. Kwa hiyo kama kitu unauza kwa 10000 inabidi uongeze 18% ya bei ya kitu hicho. Kwahiyo bei ni 11800 na hiyo 1800 ndio upeleke serikalini. Hii kodi ipo duniani kote kasoro nchi chache sana. Ila nchi za wengine ni ndogo na mfumo wa kukadiria kodi ni rahisi na umenyooka kwakuwa kule wao ni system zinafanya kazi na want nikuswipe card yaani hawatumii cash kwahiyo ni rahisi.

Mfano: bando la 1000 ndani yake vat ipo maana yake ni 1000 ni 118% ya bei. Ukicross mataputapu utakuta 100% ni 847 halafu vat ndio 153.
 
Sasa hapo sio kodi ya Value Added bali taking the value added, ilibidi kwenye hiyo 1800 ambayo ndio Value Added, Itozwe kodi ambayo ni 18% which means ni 180%. Ukisema uchukue chote haiwi value added tax, bali value added taken
 
Hii vat kwenye makaratasi au nadharia inaonekana ni kitu rahisi. Ila kiuhalisia ni ngumu na jinsi watu wanavyotaka kupunguziwa bei na halingumu ya kitaa inabidi uipotezee. Makadiria ya tra ya ritani yakija na jamaa tra wakikutaiti lazima upatwe na presha. Yaani hapo ni kupambana ukadiriwe kidogo ili ulipe ritani zao uendelee na mishemishe.

Ngoja wengine waje kuchangia.
 
Namna bora ya kukusanya kodi ni kuweka malipo yawe ya kimtandao, kwa kuwa hata mtu akilipa kidogo analimwa VAT, nimezungumza kwenye thread iliyopita

Ubaya badala ya kuzipa electronic payments tunaweka tozo kubwa ambazo zinachochea malipo ya cash ambayo mtu anaondoka bila risiti na kutolipa kodi, ikitokea makadirio yakawa chini
 
Hayo yote ni unyonyaji wa chama na serikali ya CCM,wanachoangalia ni namna ya kuneemeka wao na si wananchi
 
Namna bora ya kukusanya kodi ni kuweka malipo yawe ya kimtandao, kwa kuwa hata mtu akilipa kidogo analimwa VAT, nimezungumza kwenye thread iliyopita

Ubaya badala ya kuzipa electronic payments tunaweka tozo kubwa ambazo zinachochea malipo ya cash ambayo mtu anaondoka bila risiti na kutolipa kodi, ikitokea makadirio yakawa chini
Shida ya electronic ni tozo na makato. Ila electronic payments zitafeli maana hapatakuwa na bargaining yaani mtu ukisha kadiria bei kuwa laki+vat yaani hakuna kushusha hapo lazima mambo yatakuwa magumu zaidi 😂. Na serikali walivyo na njaa wataweka makodi mengine humo balaa yaani unauza laki ila mpunga unasoma elfu sitini 😂
 
Wewe uoni ikiwa hivyo unavyotaka udanganyifu utakuwa mkubwa, hesabu yako ni ya kichina hauwez kutumika nchi nyingine
Hakuna cha maana ulichoshauri hapa zaidi ya kuponda tuu. Kama unaamua kuponda hoja weka alternative option hapa ili tupime hoja kwa hoja.
 
Fuata maelekezo ya TRA/ Dunia ndio sahihi ya kwako ni upotoshaji
 
HUJUI LOLOTE KUHUSU KODI. ULIZA UELEKEZWE VAT INATOZWAJE.
 
Shida ya electronic ni tozo na makato. Ila electronic payments zitafeli maana hapatakuwa na bargaining yaani mtu ukisha kadiria bei kuwa laki+vat yaani hakuna kushusha hapo lazima mambo yatakuwa magumu zaidi [emoji23]. Na serikali walivyo na njaa wataweka makodi mengine humo balaa yaani unauza laki ila mpunga unasoma elfu sitini [emoji23]
We jamaa hujamuelewa mleta mada!

Mleta mada anamaanisha VAT ya asilimia 18 haipaswi kukatwa kwenye 10,000 Kama unavyosema wewe au utaratibu unaofanywa Tanzania ila inabidi kukatwa kwenye ongezeko la thamani
 
Shida ya electronic ni tozo na makato. Ila electronic payments zitafeli maana hapatakuwa na bargaining yaani mtu ukisha kadiria bei kuwa laki+vat yaani hakuna kushusha hapo lazima mambo yatakuwa magumu zaidi 😂. Na serikali walivyo na njaa wataweka makodi mengine humo balaa yaani unauza laki ila mpunga unasoma elfu sitini 😂
Hapana, inabidi ujue bei ya mzigo ulivyonunuliwa na bei ya mzigo ulivyouzwa, kile kilichoongezeka ndio kiwe taxed, Ie, hata ukienda supermarket unafanyiwa discounts na unaona jinsi VAT inavyochange kwenye risiti

Bargaining itakuwepo, kwa kuwa kivyovyote muuzaji hawezi kuuza chini ya bei aliyonunulia, so kipo kitakachokuwa kimeongezeka. Atakachokuwa anafanya muuzaji ni kupunguza cha juu
 
Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) ni kodi ambayo inatozwa kwenye ongezeko la thamani ya bidhaa katika kila hatua ya uzalishaji hadi kuuzwa. Hata Mamalaka ya Mapato Tanzania(TRA) wameweka maana inayofanana na hii. Kabla sijaenda kuipinga kwanza nielezee namna VAT ipo theoretically

Mfano

Mkulima kanunua bidhaa kwa Tsh 100, akaenda kuuza kwa Tsh 120, Hapo ongezeko la thamani ni Tsh 20 ambayo ndio itakatwa 18% ikiwa bidhaa ipo chini ya bidhaa zinazokatwa VAT, Maana yake serikali itakusanya ni Tsh. 3.6

Hapo utaona ya kwamba ili VAT iweze kukusanywa kiusahihi kwanza lazima muuzaji awe na risiti za alikonunulia na risiti aliyouzia ili serikali ichukua VAT vinginevyo VAT haitaweza kuonekana au watabaki kukadiria kama hali ilivyo
NB: Kumbuka kuwa VAT haizidi 18% kwa bidhaa zote za ndani na za nje kwa mujibu wa TRA tembelea kiunga hiki HAPA

Hali ilivyo sasa hasa kwa huduma, VAT ni tatizo kubwa sana kwa kua huduma nyingi hazina sehemu ya awali ambako zinatokea, mathalani Consultancy, Ada za Shule, Malipo mbalimbali ya huduma za serikali nk
Angalia mfano wa Kifurushi,

View attachment 1918186

Kodi hiyo ukiingalia sio tu ni kubwa, bali pia sio kodi ya ongezeko la thamani kwa kuwa
305.08 ni 18% ya Tsh. 1694.88 maana yake ni kuwa mtandao huo umenunua airtime kwa Tsh 305.11 na kuongeza 1694.888 ili kuuza kwa mtumiaji wa kawaida.

Kwa hesabu hizo utagundua kuwa si kweli kwa kuwa mnyumbulisho umeonesha kuwa 1694.92 ndio bei halisi na 305.08 ni ongezeko la thamani, which means kodi ilibidi iwe 54.92 ambayo ndio 18% ya 305

View attachment 1918187
Aidha ukiangalia hii nyingine Gharama ni Tsh 1000, VAT ni 152.54. Lakini hiyo VAT tukiamini kuwa ni 18% basi imekatwa kutoka kwenye 858.5555 kitu ambacho hakiendi sawa

Hitimisho

VAT inaonesha kuwa inakatwa kwenye bei halisi na sio Ongezeko la Thamani kama wanavyosema

Nimeeleza awali kuwa VAT ni kodi ya ongezeko la thamani hivyo kunahitajika risiti ya ufahamu bei ambayo kitu kilinunuliwa na bei ya kitu kinapouzwa ili tofauti itozwe kodi. Hali hii ya kuhitaji risiti awali inafanya moja kwa moja huduma zisiweze kutozwa kodi kwa kuwa huduma nyingi zinaponunua vitu hunua kama ‘end user’ sio intermediate na huduma anazotoa hazina zinakotoka, I.e Daktari ananunua vifaa kama end user yeye haviuzi, huduma anayoitoa haiwezi kuwa na risiti ya awali. Hii ni tofauti na anayeuza dawa ambaye amenunua sehemu kwa jumla na anaenda kuuza kwenye duka lake

Kwa Point hiyo nasema, VAT inatozwa sehemu kubwa, pia Huduma zisitozwe kodi ya Ongezeko la Thamani
Kwa mfano bei halisi ya vocha ya 1000 ni shilingi ngapi? Na iliyo ongezeka ya thamani ni kiasi gani?
 
Back
Top Bottom