Serikali inatoza VAT kubwa kuliko wanavyosema, nashauri kusiwe na VAT kwenye huduma

Serikali inatoza VAT kubwa kuliko wanavyosema, nashauri kusiwe na VAT kwenye huduma

Kwa mfano bei halisi ya vocha ya 1000 ni shilingi ngapi? Na iliyo ongezeka ya thamani ni kiasi gani?
Bei ya kifurushi mathalani ni 847.46 Tzs, thamani iliyoongezeka ni 152.54. Hence kodi inabidi iwe 18% ya 152.54 ambayo ni thamani iliyoongezeka, lakini hesabu za bongo wanakata 18% ya 1000, ambayo sio ni real price included, na ukiangalia hiyo 152 ndio wameichukua yote kama VAT ambayo ni approximately to 18% ya 1000
 
Bei ya kifurushi mathalani ni 847.46 Tzs, thamani iliyoongezeka ni 152.54. Hence kodi inabidi iwe 18% ya 152.54 ambayo ni thamani iliyoongezeka, lakini hesabu za bongo wanakata 18% ya 1000, ambayo sio ni real price included, na ukiangalia hiyo 152 ndio wameichukua yote kama VAT ambayo ni approximately to 18% ya 1000
Kwa maana hiyo 18% inatakiwa ikokotolewe toka kwenye 152.54 siyo?
 
Wewe uoni ikiwa hivyo unavyotaka udanganyifu utakuwa mkubwa, hesabu yako ni ya kichina hauwez kutumika nchi nyingine
Kwahiyo unataka kusema tuhalalishe uonevu kwasababu ya kukwepa ubadhirifu?!

Aina ya watu kama wewe ndio wapo kwenye maofisi ya serikali wanakuja na maamuzi yaliyogubikwa uzembe wa kufikiri na uzito wa kusimamia kanuni ili mambo yaende.

Taifa haliwezi kupiga hatua na aina hii ya mifumo ya uhujumu raia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
VAT kodi ya ongezeko la thamani, sasa unajuaje ongezeko la thamani kwenye huduma?

Suala la risiti linasisitizwa kwa kuwa ndio linasaidia kukokotoa VAT

Ulinunua kitu kwa TSh. 1000 ukauza kwa TSh 1200, ongezeko la thamani ni 200, then wanakata 18% yao.

Ndio maana unaambiwa unaisaidia serikali kukusanya hela yake...
Amesoma ila hajakuelewa hata kidogo. Ndio shida ya vijana wa siku hizi na unakuta hapo ana degree kwenye vyeti vyake ila uwezo wa kuelewa ni mdogo sana anabakia kuwa mtu wa kupinga na kuchallenge jambo ambalo amelitafasiri kwa namna yake ila sio kwa uhalisia wake.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) ni kodi ambayo inatozwa kwenye ongezeko la thamani ya bidhaa katika kila hatua ya uzalishaji hadi kuuzwa. Hata Mamalaka ya Mapato Tanzania(TRA) wameweka maana inayofanana na hii. Kabla sijaenda kuipinga kwanza nielezee namna VAT ipo theoretically

Mfano

Mkulima kanunua bidhaa kwa Tsh 100, akaenda kuuza kwa Tsh 120, Hapo ongezeko la thamani ni Tsh 20 ambayo ndio itakatwa 18% ikiwa bidhaa ipo chini ya bidhaa zinazokatwa VAT, Maana yake serikali itakusanya ni Tsh. 3.6

Hapo utaona ya kwamba ili VAT iweze kukusanywa kiusahihi kwanza lazima muuzaji awe na risiti za alikonunulia na risiti aliyouzia ili serikali ichukua VAT vinginevyo VAT haitaweza kuonekana au watabaki kukadiria kama hali ilivyo
NB: Kumbuka kuwa VAT haizidi 18% kwa bidhaa zote za ndani na za nje kwa mujibu wa TRA tembelea kiunga hiki HAPA

Hali ilivyo sasa hasa kwa huduma, VAT ni tatizo kubwa sana kwa kua huduma nyingi hazina sehemu ya awali ambako zinatokea, mathalani Consultancy, Ada za Shule, Malipo mbalimbali ya huduma za serikali nk
Angalia mfano wa Kifurushi,

View attachment 1918186

Kodi hiyo ukiingalia sio tu ni kubwa, bali pia sio kodi ya ongezeko la thamani kwa kuwa
305.08 ni 18% ya Tsh. 1694.88 maana yake ni kuwa mtandao huo umenunua airtime kwa Tsh 305.11 na kuongeza 1694.888 ili kuuza kwa mtumiaji wa kawaida.

Kwa hesabu hizo utagundua kuwa si kweli kwa kuwa mnyumbulisho umeonesha kuwa 1694.92 ndio bei halisi na 305.08 ni ongezeko la thamani, which means kodi ilibidi iwe 54.92 ambayo ndio 18% ya 305

View attachment 1918187
Aidha ukiangalia hii nyingine Gharama ni Tsh 1000, VAT ni 152.54. Lakini hiyo VAT tukiamini kuwa ni 18% basi imekatwa kutoka kwenye 858.5555 kitu ambacho hakiendi sawa

Hitimisho

VAT inaonesha kuwa inakatwa kwenye bei halisi na sio Ongezeko la Thamani kama wanavyosema

Nimeeleza awali kuwa VAT ni kodi ya ongezeko la thamani hivyo kunahitajika risiti ya ufahamu bei ambayo kitu kilinunuliwa na bei ya kitu kinapouzwa ili tofauti itozwe kodi. Hali hii ya kuhitaji risiti awali inafanya moja kwa moja huduma zisiweze kutozwa kodi kwa kuwa huduma nyingi zinaponunua vitu hunua kama ‘end user’ sio intermediate na huduma anazotoa hazina zinakotoka, I.e Daktari ananunua vifaa kama end user yeye haviuzi, huduma anayoitoa haiwezi kuwa na risiti ya awali. Hii ni tofauti na anayeuza dawa ambaye amenunua sehemu kwa jumla na anaenda kuuza kwenye duka lake

Kwa Point hiyo nasema, VAT inatozwa sehemu kubwa, pia Huduma zisitozwe kodi ya Ongezeko la Thamani
Kimsingi fiscal policy yetu inahitaji reform kubwa sana kama tulizofanya way back in 2005.

Tumeanza kurudi kule kwenye kuwakamua wananchi to the maximum wakati fursa za kuzalisha kipato zinaendelea kupungua sana.
 
Kimsingi fiscal policy yetu inahitaji reform kubwa sana kama tulizofanya way back in 2005.

Tumeanza kurudi kule kwenye kuwakamua wananchi to the maximum wakati fursa za kuzalisha kipato zinaendelea kupungua sana.
Umeongea ukweli ulio nona kama mwanakondoo wa bwana. Ipo hivi, sheria wakati zikitungwa mahitaji yakauwapo makubwa sana kama sasa.

Kwasasa mahitaji ni makubwa na mapato ni madogo so serikali na mamlaka zake za udangaji wanajikuta wanafurukuta na masheria yao haya waliyocopy kuedit na kupaste bila kufanya tafiti za kiutaalamu za madhara yake kwa raia na uchumi kwa ujumla.

Hapa ili kutoka tunahitaji majukwaa ya wasomi kuwawajibisha serikali kwa kuwa na mijadala ya wazi ya huu ubadhirifu unaofanywa na serikali wazi wazi kupitia mamlaka zake.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo kubwa kwenye hii nchi, VAT analipa mfanyabiashara badala ya mnunuzi. ndio mana husikii wananchi kulalamikia VAT unless iwe kwenye suala la umeme tu, Lakini kwa kweli VAT ni janga, na wafanyabiashara wanapolia na kodi ni kweli kabisa wana hali mbaya sana.
 
Back
Top Bottom