Serikali inayobadilisha maamuzi yake kwa kutegemea upepo ni Serikali dhaifu, haifai

Serikali inayobadilisha maamuzi yake kwa kutegemea upepo ni Serikali dhaifu, haifai

Kinachokwamisha serikali nyingi za kiafrika kutokusonga mbele ni UFISADI, na matumizi mabovu ya fedha, na ndio maana mwananchi anakuwa mgumu kulipa kodi, leo waziri wa fedha anaulizwa kwanini wasianze wao kupunguza matumizi kwenye misafara ya viongozi, eti ana jibu kwenye misafara ile hasa ya rais wengi wao wanatumia magari yao binafsi kweli?!!yale ya ma V8, ni ya kwao binafsi!!inshu wala sio kukusanya kama hujadhibiti upotevu wa hayo mapato ni bure, huyo mnyonge mtamuua tu, na kile mnachomuahidi kamwe hatakiona!!mfano awamu ya tano tuliaminishwa kuwa makusanyo yanakusanywa kweli kweli, na pesa haipotei!!lipi la maana sana lilifanyika, kama ni deni la taifa lilipaa sio kawaida!!
Hali ya madawa hospitalini haikuwa na unafuu wowote!!
Lipa kodi ufisadi gani umeuona wewe so far? Ufisadi upo kila sehemu kwanza hapa Tzn upoyevu wa pesa ni mdogo Sana kuliko Nchi kama South Afrika,Kenya,Nigeria nk
 
Hivyo unavyovitaja utatatua kwa kutumia makalio yako au pesa? Maamuzi ya kijinga kama haya ya kuwasikiliza walalamishi,wakulaumu kama wewe na wajuaji wengine wasio na suluhisho ndio vimefanya tuendelee kuwa na changamoto zisizopungua miaka na mikaka.
Jiwe ambaye hakuwasikiliza walalamishi aliifikisha nchi wapj zaidi ya propaganda tu
 
Lipa kodi ufisadi gani umeuona wewe so far? Ufisadi upo kila sehemu kwanza hapa Tzn upoyevu wa pesa ni mdogo Sana kuliko Nchi kama South Afrika,Kenya,Nigeria nk
Ina maana hizo ripoti za CAG, za kila mwaka huwa zinaonyesha nini?Hicho kigezo cha eti ufisadi wetu ni mdogo kuliko hizo nchi, umetumia kigezo gani?kwani hizo nchi zote ulizotaja GDP, yao imekuzidi zaidi ya mala mbili yako, kwa macho unaweza kuhisi hivyo lakini ki uchumi unaweza kukuta wewe ndio una poteza pesa nyingi kuliko wao!!kwanini mzungu kulipa kodi anaona ni ufahari wakati mwafrika anaona ni mzigo?
 
Kwa Tume ya uchaguzi ipi? Mpaka mtuondoe CCM. Mmesahau mwakajana?
Unasahau kitu kimoja. Kilichowapa CCM ushindi mwaka jana sio tume, ni Magufuli, ambaye alishakufa. Ukiona basi la Sauli limekuwa la kwanza kufika Moshi, usilisifie basi, msifie dereva. Dereva akiondoka basi hilo hilo linaweza kuwa la mwisho kufika Moshi.

Samia sio Magufuli, la sivyo chanjo za zisingekuwa zimeingia Tanzania na Sabaya asingekuwa anakalia ndoo, Mfugale asingekufa kwa pressure. Na pia usisahau jambo moja, kuna ajenda ya Zanzibar ambayo wanajua haitakaa ipite for as long as kuna raisi toka CCM Tanzania bara. Kama una akili kaa utafakari.
 
Ungekuwa na akili mngepambana nchi iwe na mifumo imara lakini sio kutegemea utashi wa Rais..umeandika pumba.
 
Ina maana hizo ripoti za CAG, za kila mwaka huwa zinaonyesha nini?Hicho kigezo cha eti ufisadi wetu ni mdogo kuliko hizo nchi, umetumia kigezo gani?kwani hizo nchi zote ulizotaja GDP, yao imekuzidi zaidi ya mala mbili yako, kwa macho unaweza kuhisi hivyo lakini ki uchumi unaweza kukuta wewe ndio una poteza pesa nyingi kuliko wao!!kwanini mzungu kulipa kodi anaona ni ufahari wakati mwafrika anaona ni mzigo?
Sio kila hoja za mkaguzi basi ni ufisadi wakati mwingine ni kukosa nyaraka au kupotea nk but vitu kwenye ground vinakuwepo.

Upotevu upo lakini haufiki hata 15% ya bajeti
 
Jiwe ambaye hakuwasikiliza walalamishi aliifikisha nchi wapj zaidi ya propaganda tu
Ndio muanzilishi wa miradi ya reli,umeme etc ,,na ni vile Jiwe kafariki hii kodi iliasisiwa kipindi chake na angekuepo hakuna mtu angepayuka kama saizi.

Watu wameacha kulipa kodi,TRA wako tuu ofisini ,kodi zinaletwa eti Serikali inasalimu amri huu ni upuuzi.

Huko South waliojifanya kuandamana wamemtoa Zuma? Ufaransa watu waliandamana Kisa kukatwa Mafao serikali ikakomaa ,,hii serikali ya mama ni dhaifu Sana ndio maana inachezewa hovyo na wapiga Domo na wachambuzi uchwara.
 
Ungekuwa na akili mngepambana nchi iwe na mifumo imara lakini sio kutegemea utashi wa Rais..umeandika pumba.
Jogoo kaona almasi akaipuuza kuwa punje moja ya mhindi ni bora mara mia kuliko kijiwe kidogo kinachong'aa. Ndio akili yako ilivyo
 
Back
Top Bottom