Serikali inayokuja isifanye makosa tena kwenye kusomesha na kuajiri

Serikali inayokuja isifanye makosa tena kwenye kusomesha na kuajiri

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,669
Reaction score
33,691
Habari JF...

Serikali inayokuja, isifanye makosa tena kwenye kusomesha na kuajiribEspecially Madaktari na walimu..

Kumsomesha mtu ambaye una uhakika hutompa kazi Ni wastage of time and resources! both,kwa mwanafunzi na serikali..

Leo tuisaidie serikali inayokuja Isirudie mambo haya ya kusomesha kundi kubwa wakati ajira ni chache,

Ni hivi;

Kwa mfano madaktari Serikali iamue wanahitajika madaktari wangapi per head. Namaanisha, kama zahanati ina uwezo wa kuchukua watu kumi+/-

then,

Serikali ipige hesabu kwa kila mfano wagonjwa wanne au watano awepo daktari mmoja,so watahitajika madaktari wawili kwa hio zahanati.

Hivyo hivyo, serikali ihesabu uhitaji wa madaktari nchi nzima , kwa kudetermine uwiano kati ya Madktari/wagonjwa

Hizi hesabu za kujua kila /hospital/zahanati/ inahitaji madaktari wangapi...itakupa collectivelly wanahitajika madaktari wangapi nchi nzima..

Na ukishajua wanahitajika madaktari wangapi nchi nzima, itakuguide wewe kama serikali uchukue wanafunzi wangapi kwa course ya Udaktari,

Mbona its simple, sijui serikali yetu imejaa upotolo gani?lol

The same method goes to walimu,na fani nyingine...

Karibuni

Serikali lazima iwe na confidence kuwa ina madaktari wangapi nchi nzima...

Kabla hamjaanza kuni crash na kusema huu ndio utaratibu uliopo...

Naombeni muanze kujiuliza kwa nini
 
Wewe hujui kitu. Watu lazima wasome kuwe na ajira au hakuna ajira. Huko kwa wenzetu nchi zilizoendelea watu wanasoma na ama wanaajiriwa serikalini au kwenye sekta binafsi ikishindikana wanajiajiri. Hakuna serikali yoyote duniani Ambayo inaweza kuajiri wahitimu wake wote wa vyuo.
 
Sasa Kama serekalini inanafasi za kazi 1000...wasome Watu 1000 TU wengine WAKALIME


Mnhhhhhh....

Hapa naiongelea serikali ndugu, kama serikali ina nafasi 1000 then ichukue watu 1000 tu!, hii itakua na uwezo wa kuwapa kazi pale wanapohitimu.....kuhusu kulima, wewe unadhania hawa madaktari wanaosota mtaani wangeambiwa kulima au kusomeshwa halafu wasipate ajira,unadhania wangechagua option ipi eti?
 
Wewe hujui kitu. Watu lazima wasome kuwe na ajira au hakuna ajira. Huko kwa wenzetu nchi zilizoendelea watu wanasoma na ama wanaajiriwa serikalini au kwenye sekta binafsi ikishindikana wanajiajiri. Hakuna serikali yoyote duniani Ambayo inaweza kuajiri wahitimu wake wote wa vyuo.

Aliyekuzuia kusoma nani?? kama wewe ni msomi,utajua serikali imekurupuka, ofcourse as a nation we are not rich but hey those limited resources should be better allocated..!
 
Mnhhhhhh....

Hapa naiongelea serikali ndugu, kama serikali ina nafasi 1000 then ichukue watu 1000 tu!, hii itakua na uwezo wa kuwapa kazi pale wanapohitimu.....kuhusu kulima, wewe unadhania hawa madaktari wanaosota mtaani wangeambiwa kulima au kusomeshwa halafu wasipate ajira,unadhania wangechagua option ipi eti?
Ina Maana serekali isitoe mikopo.kwa wanafunzi wengine Zaid ya hao 1000
Mkuu unawaza vizuri Wewe.
 
Kusoma Ni Haki ya kila mwanachi..na serekali kusomesha Ni wajibu wake..elimu haianzii chuoni..INAMAANA Watu waishie elimu ya msingi...au kwanzania huko msingi wawe wanaandaliwa Watu 1000 TU? Wakuwa madoctor..
 
Mkuu una wazo zuri ila halipo sahihi,kwasababu Hata wale wanaojiajiri wenyewe au kuajiriwa ktk Sekta binafsi bado wanakuwa wanaisaidia Serikali ktk kutoa huduma kwa jamii,lkn pia hata hao unaodhani kuwa wakishasomeshwa na Serikali kwamba wataajiriwa na Serikali, si kweli,kwasababu wengine huamua kutafuta sehemu zenye maslahi zaidi,Kumbe kusiwe na Ubaguzi ktk kusomesha maana wote watasaidia jamii.
 
Kusoma Ni Haki ya kila mwanachi..na serekali kusomesha Ni wajibu wake..elimu haianzii chuoni..INAMAANA Watu waishie elimu ya msingi...au kwanzania huko msingi wawe wanaandaliwa Watu 1000 TU? Wakuwa madoctor..
Ondoa kwanza mentality ya ubishani halafu jiweke kwenye position nzuri ya kupokea alichokisema mtoa mada.

Anachosema mtoa mada ni kwamba scarce resource financially tulizonazo kama taifa zinatakiwa kutumika kwa maslahi mapana ya kuendeleza au kusaidia taifa.

Sekta ya elimu na afya zimetumika kama mifano tu, pesa inayowekezwa na serikali kwenye maeneo mbalimbali ya kuzalisha wataalamu inatakiwa kwenda sawa na demand iliyopo kwenye eneo husika. Hii demand ni kwa serikali na hata kwa sekta binafsi.

Huwezi ukawekeza Billion 100 kugharamia masomo ya vijana ambao mwisho wa siku wanageukia kufanya shughuli zilizo irrelevant na kile ambacho serikali iliwalipia ili wakakisome.

Mfano leo hii kuna vijana wengi waliosomea ualimu lakini wanafanya shughuli za tofauti sana ambazo wala hazikuwahitaji wawe walimu kuweza kuzifanya, na wengi wao unakuta walisomeshwa na serikali. Sasa hayo ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi.

Ni sawa na kulima heka mia za mpunga halafu unakuja kuvuna heka 10 na kuacha heka 90 ziwe chakula cha ndege.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilidhan utashaur serikal itengeneze mfumo bora na mzuri wa elimu utakaofanya tuwe washindan popote Africa na dunia

Kusomeshwa Tanzania haimanishi tuishie kufanya kazi Tanzania tunaweza kufanya kaz mahali popote kikubwa ni kutengeneza mfumo mzur utakaofanya tuaminike popote duniani
 
Back
Top Bottom