Serikali ingeondoa kodi zote kwa magari ya umeme

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Bei yamafuta inazidi kupanda. Maana yake nchi tutatumia pesa nyingi sana kununua mafuta. Pesa ambazo zingeweza kufanya mambo mengine ya kukuza uchumi. Nashauri serikali ifanye mambo yafuatayo ili tupunguze kwa kiasi kikubwa matumizi ya mafuta.

1.Tungeondoa kodi zote kwa wale wanaonunua magari ya umeme. Hili ni kufanya iwe nafuu kuyanunua. Magari mapya na yaliyotumika ya umeme yawe na zero tax.

2. Ikiwezekana serikali iwape incentives nyingi wale wanaotaka kuwekeza nchini kwenye masuala yanayohusiana na magari ya umeme. Watu wanaotaka kuunda betri, motor, magari yenyewe, pikipiki, wakufanya refurbishing nk.

_117286665_saic.jpg.jpeg
cadillac_100789698_m.jpg
IMG_20220404_064741.jpg
 
Practically gari la umeme linaweza kutumika Tanzania? Kwa umeme huu wa mgao? Kuna station ngapi za ku-charge magari? Kwa kiasi gani mafuta umeme tunaozalisha unategemea mafuta?
 
Magari ya umeme unachaji tu nyumbani kwa umeme huu huu. Kama itahitajika vituo vya kuchajia kwa wale wa masafa marefu basi vitajengwa. Na serikali iwezeshe kwa kuwapa incentives wale wanaotaka kuwekeza kwenye charging station
 
Sasa ndugu, wakiondoa kodi automatically in the next 5 yrs asilimia 60 ya wabongo watakua wanaendesha electric vehicles. Hapo changamoto kwa serikali ni zifuatazo
1. Watakosa kodi wanayokusanya kwenye mafuta
2. Pressure ya wananchi itakua kubwa kuhusu masuala ya umeme wa kusuasua
3. Gridi ya taifa inaeza kuzidiwa bkoz gari kubwa inayotumia umeme lazma ile kwelikweli
4. Serikali itabd itengeneze barabara nzuri zaidi ili kuhakikisha magari hayaharibiki
5. Wakubwa itabd waache kutembelea vieite zinazokunywa mafuta yanayolipiwa na sisi walipa kodi.
Hizo no chache, reasons ni nyingi. Nchi kma Tz bado haijafika kwenye hiyo technological advancement, sisi ndo kwaaanza tunahangaika kujenga madarasa kwa hela ya covid
 
Bei yamafuta inazidi kupanda. Maana yake nchi tutatumia pesa nyingi sana kununua mafuta. Pesa ambazo zingeweza kufanya mambo mengine ya kukuza uchumi. Nashauri serikali ifanye mambo yafuatayo ili tupunguze kwa kiasi kikubwa matumizi ya mafuta.

1.Tungeondoa kodi zote kwa wale wanaonunua magari ya umeme. Hili ni kufanya iwe nafuu kuyanunua. Magari mapya na yaliyotumika ya umeme yawe na zero tax.

2. Ikiwezekana serikali iwape incentives nyingi wale wanaotaka kuwekeza nchini kwenye masuala yanayohusiana na magari ya umeme. Watu wanaotaka kuunda betri, motor, magari yenyewe, pikipiki, wakufanya refurbishing nk.

View attachment 2178069View attachment 2178072View attachment 2178077
Aaaaaahhhh, UNACHEKESHA 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Unajua serikali inakusanya mapato kiasi gani kwenye mafuta????
Mfano tu; Unajua mfuko wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) inategemea tozo zitokanazo na matumizi ya mafuta ili kuendeleza miradi yake ya ujenzi wa barabara vijijini na mijini???

Magari ya umeme hayatakuwa rahisi kwenye upande wa kodi na tozo ukae ukilijua hilo. Kwa sababu kwa baadae yanaenda kupunguza au kuuwa matumizi ya magari ya mafuta ambayo yalikuwa yanaipatia serikali mapato mengi tu.

Kwa taarifa tu serikali haiwezi kukubali kupoteza mapato yatokanayo na uagizaji na utumiaji wa mafuta kwa kuruhusu magari ya umeme kirahisi rahisi tu.

Nachokiona kodi za uagizaji gari za umeme zitakuwa juu sana, au kutawekwa tozo za kila mwezi kwa gari za umeme ili kufidia mapato yaliyopotea kutokana na kupungua kwa matumizi ya mafuta.

Kingine serikali inaweza kupunguza kodi kwenye uagizaji wa magari ya mafuta ili kuwawezesha wananchi wengi kumiliki magari ya mafuta na kupandisha kodi ya uagizaji magari ya umeme ili kuwawezesha wananchi wachache kumudu gari za umeme. Hizi mikakati za serikali ili kuhakikisha mapato ya serikali yanayotokana na mafuta hayaathiriki kwa namna yoyote na uingizwaji wa magari ya umeme.
 
Uzuri serikali(TANESCO) ndiye muuzaji pekee wa umeme nchini. Huoni kuwepo magari ya umeme anaweza kuingiza pesa nyingi hata zaidi ya sasa?
 
Gari za umeme kwa Tanzania litakuwa janga
Kuchaji gari kunatumia minimum saa moja

Fikiria hiyo foleni itakayokuwepo vituo vya kuchaji halafu unasubiri saa nzima na zaidi moto ujae
 
Wacha kulinganisha mapato ya mafuta na bishara ya Tanesco
Biashara ya mafuta siyo ya serikali. Serikali inachukua kodi tu. Ila umeme serikali inachukua zote. Japo bei ya umeme kwa km ni ndogo ukilinganisha na mafuta lakini TANESCO wanachukua yote. Hivyo utashangaa kwenye umeme serikali ikapata pesa nyingi kulikol inayopata kwenye mafuta.
 
Mimi sijaongelea biashara nimeongelea mapato ya mafuta yanayokwenda serikalini
 
Aaaaaahhhh, UNACHEKESHA 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Unajua serikali inakusanya mapato kiasi gani kwenye mafuta????
Mfano tu; Unajua mfuko wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) inategemea tozo zitokanazo na matumizi ya mafuta ili kuendeleza miradi yake ya ujenzi wa barabara vijijini na mijini???

Magari ya umeme hayatakuwa rahisi kwenye upande wa kodi na tozo ukae ukilijua hilo. Kwa sababu kwa baadae yanaenda kupunguza au kuuwa matumizi ya magari ya mafuta ambayo yalikuwa yanaipatia serikali mapato mengi tu.

Kwa taarifa tu serikali haiwezi kukubali kupoteza mapato yatokanayo na uagizaji na utumiaji wa mafuta kwa kuruhusu magari ya umeme kirahisi rahisi tu.

Nachokiona kodi za uagizaji gari za umeme zitakuwa juu sana, au kutawekwa tozo za kila mwezi kwa gari za umeme ili kufidia mapato yaliyopotea kutokana na kupungua kwa matumizi ya mafuta.

Kingine serikali inaweza kupunguza kodi kwenye uagizaji wa magari ya mafuta ili kuwawezesha wananchi wengi kumiliki magari ya mafuta na kupandisha kodi ya uagizaji magari ya umeme ili kuwawezesha wananchi wachache kumudu gari za umeme. Hizi mikakati za serikali ili kuhakikisha mapato ya serikali yanayotokana na mafuta hayaathiriki kwa namna yoyote na uingizwaji wa magari ya umeme.
Huo utakuwa ujinga kwa kweli, yani serikali iweke makodi ya juu kwenye gari za umeme wakati zikiingia zitaenda ku boost matumizi ya luku?

Wakifanya hilo nitaamini hii serikali yetu haiko kwa ajili ya kufanya maisha ya mtanzania yawe mepesi bali kutudidimiza tufie kwenye umaskini.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 Itaboost kama charging inakula kilowatts nyingi. Charger ni charger tu haiwezi kufikia heater au pasi. Wakati kwenye mafuta karibia 50% ya bei ya mafuta ni kodi. Kwa ufuatiliaji wangu miaka kama 10 imepita hivi mafuta yaliyokuwa yanaongoza kwa matumizi nchini ilikuwa ni Diesel kwa siku Tanzania ilikuwa inatumia liter 7m za diesel sasa sijajua kwa sasa tunatumia lita ngapi za Diesel kwa siku.
 
Ni hadi mindset ya gari ni anasa sio basic needs itakapoondoka vichwani mwao ndipo wazo lako litafanyiwa Kazi.
 
Magari ya umeme yatakua ni solution kubwa ya kupanda vitu bei coz mafuta yakipanda bei pia vitu hupanda bei
 
Ila sasa tawala huwa zinaangalia nazo sehemu za kupiga pesa, hawawezi kubali mapato ya mafuta yashuke kisa gari za umeme yaani kuna sehemu watabuni kufidishia au kuongeza kipato kutokana na urahisi watakaopata wananchi kutokana na matumizi ya gari za umeme.

Keep in mind huo urahisi kuna sehemu tutaulipia.
 
Back
Top Bottom