Serikali ingilieni kati kushusha bei ya vitu

Serikali ingilieni kati kushusha bei ya vitu

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2015
Posts
2,805
Reaction score
3,640
Tunaomba serikali haswa waziri wa fedha na uchumi aumize kichwa kujaribu kusadia kushuka kwa bei ya vitu haswa vya ujenzi.

Nondo mm 10 sasa hivi imefika 20,000.
Nondo mm 16 kutoka 25000 mpaka 45,000.
Gypsum board ya Thailand imefika 30,000.

Tani moja ya nondo imetoka 1,850,000 mpaka kufikia 2,220,000.

Aluminium profile kutoka 30,000 mpaka 55,000 na vioo toka 53,000 mpaka 130,000. Ujenzi unazidi kuwa aghali sana na sekta ya mafundi itazidi kuenda kukosa ajira sababu wateja wakitajiwa bei ya vitu hivi wanaacha kabisa au kuahirisha ujenzi.

Bei ya bundle inazidi kupanda sababu vifurushi vimezidi kupunjwa kwa bei kubwa.

Gesi ya kupikia majumbani 15kg inagonga 54000.

Petrol bei ya Total ni 2427 kwa lita moja. Nadhani haya ni mambo ya msingi yanayopelekea maisha kuwa aghari sana

Nawasilisha
 
Hakuna dalili ya kushuka vitu bei muimu ni kupandisha bei na wewe ya vitu unavyouza
 
Mkuu tulielezwa tumefika uchumi wa kati naona hai reflect na uhalisia kanisa hapa ardhini
 
Ni kweli mkuu mfumuko wa bei ni mkubwa mno sio sekta ya ujenzi ni sekta zote. Kwa kweli ni shida tupu viongozi wapo kimya kizito huku wakijisifu uchumi unapanda na kwamba wao ni wachumi bora.

Kazi ipo na uzi kama huu haupati wachangiaji maana wengi wamekuwa makuwadi wa siasa uchwara
 
Ukiona vitu vinapanda bei kwa haraka sana sababu kubwa ni inflation tuu, hapo serikali imechapisha pesa kuliko ilizonazo/inazokusanya, yule mchumi fake wa tozo aliyesema wahamie Burundi inaonekana ni mtupu kama maskafu yake anayovaaga
Na ni kweli hawa jamaa inaonekana wanachapisha pesa nyingi
 
Sababu kubwa inaweza kuwa wameanzisha na kuongeza kodi nyingi mpya kwa muda mfupi sana.

Bora wangeziingiza taratibu kwa muda wa mrefu. Serikali ijikite kupunguza matumizi na gharama zisizo za lazima na kutanua vyanzo vipya vya mapato (exports), kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji, kuondoa rushwa, urasimu
 
Takwimu kama hizi ni vizuri ulivyoonyesha kwa baadhi bei imeongezeka kutoka kiasi gani kwenda kingine, fanya kwa zote na ukiweza weka tarehe mfano (Nondo mm 16 kutoka 25000 (DD/MM/YYYY) mpaka 45,000 (04/10/2021) na baadhi ya maeneo

***ni kweli kuna ongezeko la bei za baadhi ya bidhaa
 
Hao wauza cement na nondo huwa wanajipandishia tu bei .hawako regulated kabisa.

Sekta ya ujenzi iangaliwe sana
 
Dk. Mpango alionekana yupo vizuri Sana upstairs ktk masuala ya kiuchumi, na mama alimuomba awe VP lkn asimamie uchumi. Sasa kwann mambo yanaenda hovyo hovyo namna hii?
 
Hizi ndizo hoja wananchi tunapenda kuzisikia wabunge wetu, mawaziri wetu wakizifafanua wanasaidiaje kupunguza mfumuko wa bei namna hii.

Hata huo ujenzi wa madarasa kila shule utakuwa wa kusuasua maana bei ya material haitoshikika.

Oddafrica watu wanajenga hoja kuhusu mama dangote mara dullah makabila mara simba kuuza wachezaji, mara madadapoa.

Tungependa mwanajamii formu CM aka Msigwa afikishe ujumbe hali ya bei za vitu mtaani hazishikiki kipande cha muhogo siku hizi 200.
 
Tunaomba serikali haswa waziri wa fedha na uchumi aumize kichwa kujaribu kusadia kushuka kwa bei ya vitu haswa vya ujenzi.

Nondo mm 10 sasa hivi imefika 20,000
Nondo mm 16 kutoka 25000 mpaka 45,000
Gypsum board ya Thailand imefika 30,000

Tani moja ya nondo imetoka 1,850,000 mpaka kufikia 2,220,000.

Aluminium profile kutoka 30,000 mpaka 55,000 na vioo toka 53,000 mpaka 130,000. Ujenzi unazidi kuwa aghali sana na sekta ya mafundi itazidi kuenda kukosa ajira sababu wateja wakitajiwa bei ya vitu hivi wanaacha kabisa au kuahirisha ujenzi.

Bei ya bundle inazidi kupanda sababu vifurushi vimezidi kupunjwa kwa bei kubwa.

Gesi ya kupikia majumbani 15kg inagonga 54000.

Petrol bei ya Total ni 2427 kwa lita moja. Nadhani haya ni mambo ya msingi yanayopelekea maisha kuwa aghari sana

Nawasilisha
Bei hushuka iwapo inflation itapungua. Inflation husababishwa na kuwepoa kwa hela nyingi mzungukoni bila kuwa na uwiano wa uzalishaji. Sasa kipindi hiki cha kupiga madili, pesa itakuwa nyingi mzungukoni, kwa hiyo inflation ni un-escapable side effect. Wakati wa Magufuli inflation ilikuwa checked sana, na bei hazikupanda kabisa hata kama zilikuwa za juu zilibakia kiwango kile kile.
 
Vitu viko juu sana uchumi umeporomoka unataka serikali ishushe bei ya vitu kwani yenyewe inafanya biashara gani? tunatakiwa kuwa wakweli tu maisha yamekua magumu sana nyakati hizi, kwa wafanyabiashasra ndio usiseme hakuna faida wanayopata na hao TRA wanakamua hukohuko. Nashangaa sana kipindi hiki na shida zote hizi jitu limefuga hadi kitambi.
 
Bei huwa haishuki jamani, mnakumbuka serikali ilivyojaribu kushusha bei ya sukari ? 🐒
 
Back
Top Bottom