Serikali ingilieni kati kushusha bei ya vitu

Serikali ingilieni kati kushusha bei ya vitu

Ongeza bei ya Bati, hivi hawa Alf wapo realistic kweli?
 
Aisee. Ni kweli mambo magumu sana. Yaani Mungu atusaidie kwa kuwapumzisha viongozi mizigo serikalini. Eeh Mungu tusaidie maana hatuna kimbilio tena. Watetezi wamepewa kesi bandia, wengine wamekimbia nchi.
Umetoa comments ya maana sana kuliko mwingine kwenye huu uzi
 
Tunaomba serikali haswa waziri wa fedha na uchumi aumize kichwa kujaribu kusadia kushuka kwa bei ya vitu haswa vya ujenzi.

Nondo mm 10 sasa hivi imefika 20,000.
Nondo mm 16 kutoka 25000 mpaka 45,000.
Gypsum board ya Thailand imefika 30,000.

Tani moja ya nondo imetoka 1,850,000 mpaka kufikia 2,220,000.

Aluminium profile kutoka 30,000 mpaka 55,000 na vioo toka 53,000 mpaka 130,000. Ujenzi unazidi kuwa aghali sana na sekta ya mafundi itazidi kuenda kukosa ajira sababu wateja wakitajiwa bei ya vitu hivi wanaacha kabisa au kuahirisha ujenzi.

Bei ya bundle inazidi kupanda sababu vifurushi vimezidi kupunjwa kwa bei kubwa.

Gesi ya kupikia majumbani 15kg inagonga 54000.

Petrol bei ya Total ni 2427 kwa lita moja. Nadhani haya ni mambo ya msingi yanayopelekea maisha kuwa aghari sana

Nawasilisha
Unachekesha wewe,ukiona bei juu ujue uhitaji ni mkubwa na bidhaa zinatoka.

Kazi ya serikali sio kupanga bei za soko, Serikali inaweza kuingilia kwenye umeme,mafuta na xhakula tuu sio nondo mara mabati nk
 
Back
Top Bottom