Serikali ingilieni kati kushusha bei ya vitu

Serikali ingilieni kati kushusha bei ya vitu

Waziri wa TOZO!
Ukiona vitu vinapanda bei kwa haraka sana sababu kubwa ni inflation tuu, hapo serikali imechapisha pesa kuliko ilizonazo/inazokusanya, yule mchumi fake wa tozo aliyesema wahamie Burundi inaonekana ni mtupu kama maskafu yake anayovaag
 
Hawa wanaokula bure wala hawafikiriii maslahi mapana ya nchi zao ni matumbo yao kwnza
Labda tuweke sheria kila mbunge lazima aishi maisha ya kipato cha Mtanzania wa kawaida kwa miezi sita hivi katika miaka yao mitano.

Inaweza kuwafanya kufikiria zaidi maamuzi wanayofanya na kuchangia na ķuamua maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Au labda nafasi kadhaa katika bunge zingetengwa kwa Walimu, wakulima, Nurses, Madaktari, wamachinga, mama lishe watu wa kawaida. Hawa wangekuwa na uchungu zaidi na pesa yao na wangepigania zaidi maslahi mapana ya taifa na ya watu kawaida.
 
Ni wakati wa maskini kuishi kama mashetani na matajiri kama malaika.
R.I.P JPM
 
Hilo ni gumu ktk nchi ambayo ujinga na unafiki umetamalaki
Labda tuweke sheria kola mbunge lazims aishi maisha ya kipato cha Mtanzania wa kawaida kwa miezi sita hivi katika miaka yao mitano.

Inaweza kuwafanya kufikiria zaidi maamuzi wanayofanya na kuchangia na ķamua maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Au labda nafasi kadhaa katika bunge zingetengwa kwa Walimu, wakulima, Nurses, Madaktari, wamachinga, mama lishe watu wa kawaida wangekuwa na uchungu zaidi na pesa yao na wangekuwa tayari zaidi kupigania maslahi yao wenyewe (wa kawaida).
 
Hilo ni gumu ktk nchi ambayo ujinga na unafiki umetamalaki

Hili ni tatizo la elimu, wananchi hawajui nguvu zao kwa pamoja. Labda kodi na tozo zikiongezeka zaidi itaanza kutafanya watu watambue nguvu zao kuielekeza na kuishinikiza serikali kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya taifa
 
Nadhani alishasema kama unaona huyawezi uende Burundi.

Labda kama mnataka arudie kwa sauti ya juu.
 
Nafasi za ubunge, zinatakiwa ziwe za utumishi, uwakilishi, kutumikia wananchi, kuwakilisha na kutatua kero na changamoto zao.

Zisiwe ajira za kudumu. Wananchi wawezeshwe kupiga kura ya kutokuwa na imani na mbunge, na viongozi wengine ambao hawatimizi wajibu wao na kuwafuta uhunge, kutengua nafasi zao.

Miaka mitano inatosha kuwa mwakilishi, baada ya hapo aje mwingine. Mshahara wa ubunge usiwe mbali sana na kipato cha Mtanzania wa kawaida.

Kwahiyo mtu akienda pale anajua amebeba ya dhamsns kubwa, anaenda kujitolea kupigania watu wake nchi yake. Sio tumbo lake tu.
 
Hela si zimeanza kuonekana mitaani zitumie kununua hivyo vitu

R.I.P JPM
 
Ni kweli mkuu mfumuko wa bei ni mkubwa mno sio sekta ya ujenzi ni sekta zote. Kwa kweli ni shida tupu viongozi wapo kimya kizito huku wakijisifu uchumi unapanda na kwamba wao ni wachumi bora. Kazi ipo na uzi kama huu haupati wachangiaji maana wengi wamekuwa makuwadi wa siasa uchwara
Viongozi hawapo kwa ajili ya uongozi wapo kwa ajili ya matumbo yao
 
Sasa hivi kila mtu ana makunyanzi. Maisha tight sana.
Tatizo kila siku na kila mwaka watu huwa wanasema maisha yamekuwa tight. Hakuna mwaka ambao watu walisema maisha yakikuwa mazuri.

Tunaishi kinafiki hivyo hivyo.
 
Ndio biashara huria tuliokuwa tunaitamani. Tusiwaingilie watafunga biashara jamani.
 
Nitofautiane kidogo nawe kuhusu elimu,mana wapo wasomi wengi tu lkn tumbo imekuwa kila kitu kwao
Hili ni tatizo la elimu, wananchi hawajui nguvu zao kwa pamoja. Labda kodi na tozo zikiongezeka zaidi itaanza kutafanya watu watambue nguvu zao kuielekeza na kuishinikiza serikali kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya taifa
 
Ukishaweka maskhara na kucheza na bei za mafuta , kila kitu kinapanda.
Wakati wa mdororo wa uchumi , OPEC walifikia hadi kuuza mafuta kwa negative dollars, viongozi wetu wakaona ni muda muafaka wa kuyajaza kodi mafuta maana yalikuwa cheap bin rahisi.
Sasa mafuta yanarudi kwenye bei zake halisi huko uarabuni, tutafika 4000 kwa lita very soon
 
Aisee. Ni kweli mambo magumu sana. Yaani Mungu atusaidie kwa kuwapumzisha viongozi mizigo serikalini. Eeh Mungu tusaidie maana hatuna kimbilio tena. Watetezi wamepewa kesi bandia, wengine wamekimbia nchi.
 
Ongeza thamani ya huduma zako. Kama muajiriwa subiri uwezekano ni mkubwa mishahara kuongezwa ili kuleta equilibrium. Serikali inarudisha fedha kwa wananchi lazima vitu vitapanda bei tu. Bado magari na viwanja.
 
Back
Top Bottom