mkamanga original
JF-Expert Member
- Jan 21, 2015
- 637
- 663
Muundo wa Halmashauri zetu zina idara 12 na vitengo 6. Hivyo kufanya jumla ya wakuu wa idara na vitengo kuwa 18 . Kabla ya kuondoka watalaam wa Maji kwenda RUWASA Halmashauri ilikuwa na wakuu wa idara na vitengo 19.
Idara zilizopo katika Halmashauri ni idara ya Elimu Msingi, Idara ya elimu Sekondari, Idara ya utumishi na utawala, Idara ya Mipango na ufuatiliaji, Idara ya Ujenzi, Idara ya Kilimo na umwagiliaji, Idara ya mifugo na Uvuvi, Idara ya Ardhi na Maliasili(ijapokuwa wameshahamia wizarani),Idara ya Afya , Idara ya usafi na mazingira, Idara ya Fedha. Vitengo ni Kitengo cha uchaguzi, kitengo cha manunuzi, kitengo cha ukaguzi wa ndani, kitengo sheria, kitengo cha Tehama, na Kitengo cha Nyuki.
Kimsingi wakuu wa idara na vitengo katika Halmashauri ndio wanao unda timu ya usimamizi wa Halmashauri ( CMT- Council management team). Wakuu wa idara na vitengo wanafanya kazi chini ya Mkurugenzi, Mkurugenzi wa Halmashauri ndio mwenyekiti wa CMTs .Timu hii ndio inayosimamia shughuri za kila siku za Halmashauri , kila mkuu wa idara na vitengo anajukumu la kusimamia watumishi wa chini yake kwa kuhakikisha anawafikia wadau wake waliopo chini kabisa, ikiwa ni pamoja na wananchi .
Wakuu wa idara na vitengo wote wana hadhi sawa, kwa maana ya stahiki zao na katika usimamizi .Tofauti ipo katika utekelezaji wa Majukumu na uzito wa majukumu.
Tumeona serikali kupitia waziri mkuu akikabidhi magari kwa wakuu wa idara ya elimu Msingi, Magari hayo yatasaidia katika ufuatiliaji wa shughuri za elimu katika Halmashauri. Nitoe pongezi za dhati kwa serikali kwa kuliona hilo.
Lakini ushauri wangu kwa serikali ni wakuu idara walio wengi hawana magari ,hivyo inawawia vigumu sana katika kutekeleza majukumu yao ya kila Siku . Kuwaachia Halmashauri wanunue magari kwa ajili ya matumizi ya idara na vitengo imekuwa changamoto kubwa. Ziko idara ambazo ukifanya sensa Leo kati ya Halmashauri 185 utakuta karibu 95% ya idara hizo hazina magari pamoja na umuhimu wake .Mfano tu idara ya ujenzi ambayo ndio wasimamizi miradi ya maendeleo hawana magari kabisa fanyeni sensa muone . wahandisi wa halmashauri matokeo yake wanafanya kazi ya usimamizi wa miradi kwa Simu,Siku hizi serikali inapeleka fedha moja kwa moja kwenye mashule,waandisi wakisha waandalia BOQ walimu na kuwakabidhi basi hawana uwezo wa kwenda site kwenda kufanya ufuatiliaji ,ndio maana miradi mingi baada ya miaka 2 utakuta sakafu imetifuka ,madarasa yamebaki vumbi tu, kwa sababu ya usimamizi hafifu. Utakuta Halmashauri ina magari 4 , mweka hazina atumie hilo hilo kwenye mapato, afisa elimu atumie hilo hilo kwenye elimu , afisa kilimo atumie hilohilo, Afisa mipango atumie hilo hilo katika kukusanyia takwimu mbalimbali za miradi. Afisa maendekeo ya Jamii atumie hill hill kwenda kugawa fedha za Tasaf .Gari ambalo linakuwa nzima muda wote ni la Mkurugenzi tu, mengine yote hayatengenezwi.
Waziri mkuu aziagize kila wizara ihakikishe inanunua magari kwa ajili ya wakuu wa idara wao waliopo kwenye Halmashauri, wananchi wanakosa baadhi ya huduma kwa sababu tu maafisa wanashindwa kuwafikia na kutatua changamoto zao. Serikali inaagiza tu maafisa wasikae ofisini, huku vijijini hao maafisa wanaendaje , wakodi yebo au boda boda.
Mama Ummy Mwalimu saidia hili, mwenzako Jaffor alishindwa kabisa hapo tamisemi kuwa mbunifu wa kuzitafutia ufumbuzi changamoto za Halmashauri kazi yake maneno mengi utekelezaji sifuri, Alikuwa amekosa ubunifu . Mshauri Rais kule wizara ya ujenzi kuna magari mengi ya miradi ya wahisani ambayo imephase out, chukueni hayo pelekeni Halmashauri, Bandarini kuna magari mengi ambayo wamiliki wake wameshindwa kuyagomboa chukueni hayo pelekeni Halmashauri. Mtakuwa mmezisaidia Halmashauri kuwafikia wananchi kwa wakati.Wizara ya tamisemi ndio wizara ambayo IPO jirani na wananchi, hivyo wapewe magari, au vile vyanzo ambavyo vilichukuliwa virudishwe Halmashauri