Liverpool VPN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2020
- 6,958
- 16,358
Ndugu inaonyesha unaishi sanaa mjini, Kuna wilaya za ajabu kwenye miundo mbinu ndugu huku public transport inatoka asubuhi na kurudi jioni na ni gari MOJA tu, bro umefika wilaya kama Songwe, Kilolo, Momba, Mburu??Mbona viongozi wengine waandamizi wa serikali (mawaziri, wakuu wa wakala na idara kubwa n.k.) utumia magari ya serikali kwa shughuli zao binafsi? Waziri anavyoenda kanisani au msikitini kwa gari la serikali, hiyo siyo shughuli binafsi?
Kama alivyosema mdau hapo juu, nami nakubali kabisa haya magari ni mzigo mkubwa sana kwa serikali. Nilishawahi kusema humu kwamba tunapaswa kuwa na ‘government car pools’ kubwa katika kila wilaya, idara na taasisi yenye magari ya aina (size, space, power etc.) tofauti tofauti kukidhi mahitaji husika ya matumizi. Pesa itakayookolewa ikaongezee bajeti za kuboresha usafirishaji na usafiri wa umma. Wakuu wa idara na taasisi watakuwa na options za kutumia magari yao binafsi (kwa kupata misamaha ya kodi na incentives zingine) ama usafiri wa umma kwa shughuli za kutimiza wajibu wao.
#YNWA