chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Nashauri serikali ipeleke muswada wa sheria unaoondoa ulazima wa kulipia ada za T.L.S ili kupata leseni ya uwakili, hii pia itaondoa lile sharti la points ambazo hupatikana kwa wakili kuhudhuria semina. Vitu hivi ndivyo huifanya T.L.S ipate fedha, kwa sasa Mwabukusi atatumia fedha hizo kutukana kila mtu.
Badala yake, T.L.S iwashawishi watu wake wailipe kwa hiyari yao, badala ya kutegemea mgongo wa nguvu ya Mahakama kuzuia leseni za mawakili kwa kutolipa ada za T.L.S na kuhudhuria semina ili wapate points.
Pia Mwanasheria Mkuu apendekeze badiliko la sheria ambalo litaibakiza T.L.S katika majukumu ya kitaaluma tu, na kuwaondoa katika siasa. Hii itajumuisha kuwaondolea wao kama chama mamlaka ya kusajili kesi yoyote kwa jina lao, ila kama anasajili mwanachama binafsi iwe sawa. Kwa sababu fedha ya chama isidhamini mambo ambayo si kila mwanachama anayakubali.