PAZIA 3
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 1,102
- 1,919
Hili ni andiko juu ya sensa na makazi KUHUSU kuwepo kwa uwazi wa zoezi lenyewe.
Nimeamua kukumbushia hili maana tayari zimebakia siku 7 tu ili wananchi wapate kuhesabiwa.
Zoezi hili Lina manufaa mengi Sana na linaigharimu serikali yetu mamilioni ya pesa. Hizo pesa ni kodi zetu na endapo zoezi halitofanikiwa maana yake wasomi wote tulioshiriki zoezi hili na washauri wa serikali tutakuwa tumefeli wote, hivyo tutapata hasara ya mali, muda na Mambo mengineyo.
UMUHIMU WA SENSA
1. Serikali itajua idadi ya wananchi wake kwa ujumla waliopo katika jografia yake. Hii itasaidia usambazaji wa huduma za kijamii kwa usawa kulingana na eneo husika.
2. Serikali itajua idadi ya wasomi na wasio wasomi. Hii itasaidia kuongeza budget katika wizara za ki-elimu maana taifa bila wasomi haliwezi kuendelea kwa haraka.
3. Serikali itajua idadi na uwezo wa wananchi wake kiuchumi. Wenye uwezo wa chini kabisa, wa Kati na wajuu
4. Serikali itajua idadi ya jinsi za wananchi wake, hii itasaidia kujua nguvu kazi ya taifa
CHANGAMOTO ZA ZOEZI HILI
1. Kuna usili mkubwa Sana wa fomu za sensa. Elimu inatolewa kuhamasisha tu watu wajitokeze tarehe 23 August lakini hawaonyeshi fomu zenye taarifa ya maswali atakayoulizwa mwananchi. Ilipaswa fomu hii isambae kila mahali ili ikitokea mtu akawa bize na shughuri zingine, anaweza kuziacha taarifa sahihi hata kwa watoto wake maana zoezi hili haliwezi kuchukua nusu saa kwa nchi nzima Kuhesabiwa, lazima watu wakafanye kazi. Kama zoezi la upigaji kura uchaguzi mkuu huwa tunapewa fomu za mfano, kwanini isiwe SENSA?.
Niombe tu Serikali iachane na usili wa kuficha fomu ya maswali yatakayoulizwa na itasaidia kwa watu kuiona na kurekebisha Kama baadhi ya taarifa zitakosekana haswa taarifa muhimu. Kwasasa kila mtanzania hajui ataulizwa nini na sidhani Kama taarifa hizo zilizopo kwenye fomu hiyo zinajulikana na wabunge au watu wa haki za BINADAMU.
Serikali itumie media kuonesha mfano wa hiyo fomu tuione kabla ya zoezi lenyewe.
Ahsante

Upvote
1