Serikali iongeze bei ya energy drinks ili kunusuru maisha ya Watanzania

Serikali iongeze bei ya energy drinks ili kunusuru maisha ya Watanzania

Nisaidie basi kufikiri Mkuu
Tufanye nini ili watoto wetu wanunue maji, maziwa na juice badala ya eneji!???
Hiyo NI elimu ya ngazi ya familia, Mimi nimeacha muda mrefu Tu kutumia energy na kahawa pia.

Ni ngumu kuachia vyote lakini vingine NI rahisi Sana.

Mfano watu wanateseka Sana na vidonda vya tumbo, Kwa nini hawa Wahindi wasijenge viwanda vya madawa wauzie watu vidonge vya anti gas na anti heartburn Kwa bei nafuu tutokomeze ugonjwa wa vidonda vya tumbo?
 
Mkuu; tusiilaumu sana Serikali(Japokuwa nayo inachangia/inahusika) ila sisi walaji tunayo tabia sugu ya kutokutaka au kujisumbua kujua mambo kwa undani au kusoma maelekezo ya mtengenezaji, ni nini hasa kilichomo (ingredients)kwenye hicho kinywaji ila tunadanganyika kirahisi mno na ladha ya sukari au kupuuzia yale yanayohusu Afya zetu ni hadi litukute jambo ndo tunashtuka. Hatukubali kwamba Mwili wetu ni kile tunachokula.
Aidha wazazi esp.akina mama utamkuta mama kambeba mwanaye na chupa ya juice eti anampenda mwanaye kwa kumnunulia hiyo juice.Hajiulizi hata kidogo kwamba ni shamba gani kubwa hivyo hapa Tz linauwezo wa kuzalisha embe, machungwa n.k. kwa mwaka mzima na kutosheleza waTz zaidi ya mil. 60???
Kweli ndugu yangu, hatusomi maelekezo yaliyowekwa kwenye hivyo vinywaji , energy zote wamesema zisinyweke zaidi ya mbili kwa siku, pia zisinyweke muda mfupi kabla ya kulala, sisi sasa ni kunywa tu tahamaki athari zimeshakuwa kubwa!
 
Ni tatizo linatengenezwa na serikali inakaa kimya kwa maana imeruhusu watu wake wawe weaknesses hapo mbeleni, yote ni serikalini kuto kuithamini kesho.
Hata wenye viwanda pamoja na kuangalia wingi wa faida leo lakini sijui kama wanapiga hesabu ya hasara kwa kesho .

Naunga mkono bidhaa hizo zipande bei au zipunguzwe uzalishaji na usambazaji ziweze kuadimika automatically bei itapanda na taratibu watu tutaacha kununua hizo energy drink mimi binafsi ni miongoni mwao wanaotumia hivyo vinywaji.
Sasa serikali kama inaruhusu Visungura itapiga vita Vipi energy?

Msipopambana wenyewe ngazi ya familia imekula kwako, sasa wewe mtu mzima anashindwa Vipi kuachia energy?

Mimi nilishapiga chini kitambo, hata itokee dharura kama nitahitaji kunywa energy basi nitanunuwa redbull ndio iko standard.
 
Wasalaam wana jamiiforum

Kumekua na matumizi mabaya sana ya energy drinks Tanzania. Mbaya kuliko ni kwamba hadi watoto wadogo wa shule za msingi ni wanywaji wakubwa wa hivi vinywaji.

Na wanavichukulia powa kwamba vinawachangamsha na kuwaondolea uchovu lakini taratibu vinawamaliza.

Nimewaza bei yake madukani na vile zinazalishwa kwa wingi na makampuni tofautitofauti nikagundua soko lake ni kubwa sana nikaona ni heri serikali sasa ipandishe bei ipate mapato ya kusaidia waathirika na kupunguza matumizi yake kwa watanzania.

Bei ya chini ikiwa 5,000 kwa chupa sio mbaya kabisa

View: https://youtu.be/fHEDEy-P_xc?si=bJdgfMoKoEku53HJ

Watakaoshindwa kutumia ni vizuri warudi kwenye kutumia chai, kahawa na juice

Serikali ipige stop hizo takataka kunusuru maisha ya vijana ambao ni taifa la kesho,hatakama inapata kodi kubwa
 
Ila bora nyie wanaume caffeine madhara yake sio makubwa kama sisi.
Ukitaka uache nunua nyingi zitakukinai tu
Sina hakika sana kama caffeine ina madhara zaidi kwa aina ya jinsia.
Nimeanza kunjwa energy tokea 2015 ingawa natumia kila asubuhi kabla ya kazi na mara chache mchana au usiku kama kazi imekua nyingi, imefika bila hio kazi inakua nzito .

Ngoja nijaribu kutumia mfululizo ili kukata hamu.
 
MO extra, azam energy, defender, Jembe,
Zote hizo zikizidi sana bei ni mia saba hatari sana kwa afya
 
Ukiweka limao caffeine inapungua ama uraibu unapungua?
Limao NI anti acid, inondowa uric acid na ina kazi nyingi Sana positive mwilini.

Wafuatilie wazungu wanapokunywa kahawa wanachanganya na maziwa, fuatilia kwenye Milo na vinywaji lemon ni lazima, hawa hii elimu wanayo tangu utotoni ndio maana hawadamkii kwenye supu asubuhi.
 
Wasalaam wana jamiiforum

Kumekua na matumizi mabaya sana ya energy drinks Tanzania. Mbaya kuliko ni kwamba hadi watoto wadogo wa shule za msingi ni wanywaji wakubwa wa hivi vinywaji.

Na wanavichukulia powa kwamba vinawachangamsha na kuwaondolea uchovu lakini taratibu vinawamaliza.

Nimewaza bei yake madukani na vile zinazalishwa kwa wingi na makampuni tofautitofauti nikagundua soko lake ni kubwa sana nikaona ni heri serikali sasa ipandishe bei ipate mapato ya kusaidia waathirika na kupunguza matumizi yake kwa watanzania.

Bei ya chini ikiwa 5,000 kwa chupa sio mbaya kabisa

View: https://youtu.be/fHEDEy-P_xc?si=bJdgfMoKoEku53HJ

Watakaoshindwa kutumia ni vizuri warudi kwenye kutumia chai, kahawa na juice

Bei itoke 600 hadi sh ngap?
 
Back
Top Bottom