Serikali iongeze bei ya energy drinks ili kunusuru maisha ya Watanzania

Oky, asante sana mku🙏🙏
 
Energy ni mbaya bora unywe beer
Kibaya zaidi hadi Kuna wamama wanawapa watoto wao under 5yrs nadhani ni elimu hawana juu ya hii kitu
 
Kwani Dr Msukuma na wenzake pale mjengoni wanalijua hili.

Baba wa Taifa aliona mbali sana kutenganisha biashara na Utumishi wa umma.
 
Niliwahi kuambiwa na mtaalamu wa afya mmoja kwamba wanawake tujiweke mbali na caffeine zinasababisha fertility problem. Nikajua nyie mpo safe kiasi.

Pole sana jitahidi kwa bidii zote
 
Kwani hizo energy zina shida gani?
 
Ukiona kinyangi kinaongezwa vitu kibao. Ujue kuna matatizo.
 
Leo Saa 12 asubhi nimekutana na jamaa ana energy pamoja na karanga za kukaanga za mia 5 mpaka tumbo likaanza kunikoroga kwa kutizama tu.
 
Hizo energy drinks za mo, azam na zinginezo kama nimekunywa sana tangu ziingie mitaani basi nimekunywa 5 tu baada ya hapo niliachana nazo kabisa
 
fertility

Niliwahi kuambiwa na mtaalamu wa afya mmoja kwamba wanawake tujiweke mbali na caffeine zinasababisha fertility problem. Nikajua nyie mpo safe kiasi.

Pole sana jitahidi kwa bidii zote
Asante sana nitajitahidi niombee!
Katika kusoma soma kwangu caffeine haina madhara makubwa sana isipo kuwa ikizidishwa au ikitumiwa kwa wingi hutengeneza uraibu, hio ndio shida kuu.
Kama inashida na mfumo wa uzazi ni bora kukaa mbali nayo, lakini pia caffeine hupatikana kwenye chai, tunaweza kuikwepa chai ndugu yangu!
 
Niliwahi kuambiwa na mtaalamu wa afya mmoja kwamba wanawake tujiweke mbali na caffeine zinasababisha fertility problem. Nikajua nyie mpo safe kiasi.

Pole sana jitahidi kwa bidii zote
Energy drinks hutangazwa kama vinywaji vinavyoweza kuongeza nguvu na kuamsha ubongo.

Matumizi ya bidhaa hii yameongezeka sana siku za hivi karibuni jambo linaloongeza hamu ya kujifunza na kufahamu madhara yake kwa sasa na baadae.

Wingi wa kemikali za caffeine huathiri utendaji kazi wa moyo na mishipa ya damu. Hii huongeza nafasi ya kuugua magonjwa ya moyo na shinikizo la damu.

Vinywaji hivi huharibu pia mpangilio wa saa ya ndani ya mwili wa binadamu inayoongoza mzunguko wa usingizi, huufanya mwili upoteze kiasi kikubwa cha maji, hupunguza uoni wa macho pamoja na kufanya baadhi ya watu wapatwe na hali ya kuweweseka.

Aidha, kopo moja dogo lenye ujazo wa 16 oz ( 470 mls) huwa na nyongeza ya sukari inayofikia hadi gramu 54-62. Kiwango hiki kinazidi mahitaji ya kawaida ya kila siku ya mwili hivyo huongeza nafasi ya kuugua ugonjwa wa kisukari, kuongezeka kwa uzito pamoja na kuoza kwa meno.

Watu wenye magonjwa sugu, wanawake wajawazito pamoja na watoto ni makundi matatu yasiyoshauriwa kutumia kinywaji hiki.

Kama ilivyo kwa vitu vingine, madhara yake huonekana pale kinapotumika kwa kiasi kikubwa.
 
Nakuombea mpendwa.
Chai achana nayo kabisa, tumia mchaichai , karafuu nk
 
Asante mkuu kwa haya maelezo
 
Vyakula vyote vizuri ni kutoka shambani hadi mdomoni. Waafrika tumeishi miaka 10,000 kwa huu utaratibu.
 
Inabidi serikali idhibiti uzalishaji wa hiyo bidhaa na baadhi ya bidhaa zingine kama vile vipombe vya kwenye kopo za plastiki zinamaliza sana nguvu kazi mdogo mdogo, hadi watoto wa sekondari wanakunywa kutokana na kua na bei ndogo kama ya vocha
 

Sio kila familia inatoa elimu mkuu ndio maana tuna watoto wa mtaani na panya rd
angalia vizuri utaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…