Serikali Iongeze nguvu kwenye masomo ya Hisabati na fizikia

Kuna la kujifunza kutoka kwenye shule za St Fransis,Marian Boys,Cannosa,Feza boys,Ahmes.. sijui hawa wenye shule za Kikatoliki na private wana siri gani kwenye kufaulisha physics na maths.
Tutazunguka Sana mkuu Siri izo shule hapo juu wamewekeza kwanzia miundo mbinu mpk kuwalipa walimu vizuri
 
Ila mambo ya kina diamond harmonise juma lokole shyshy wanayajua [emoji23][emoji23][emoji23]
Uko pwani ipi lakini mamdenyi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Nilijitahidi nao na kuwaahidi zawadi naona na mmoja tu hapa kaleta ripoti kawa wa 4,

Wazazi nao wanajisahau kufuatilia maendeleo ya watoto wao
 
Nauliza lini serikali itatambua kwamba waalim wengi sio woote wa shule za misingi hawawezi fundisha HISABATI na baadhi ya mada za masomo ya sayansi.
Ikishaliona hilo ibadili vigezo vya udahili wa waalim wa GRADE 3A ambao wengi wao baada ya kuhitimu huende kufundisha primary schools huku masomo hayo ya sayansi na hisabati waliangukia pua form 4. Wengi wao sio woote
 
Walimu wengine wao wenyewe hawajui vya kutosha bla bla nyingi na mazingira ya kufanya kaz mabovu uyo mwalimu wa math hawez fundisha vzuri kwa mazingira ya shule zetu.... motisha kwa walimu hamna hata kidogo inafanya walimu kujaa stress za ajabu kabla hata hajaanza fundisha,, hadi kufikia kipindi mwanafunz akikosea kidogo tu hesabu ni bakora za maana, hadi mwanafunzi anajuta why asome sayansi mwishowe unatengeneza kizazi cha kukimbia masomo tajwa ikiwemo math.
 
Tutazunguka Sana mkuu Siri izo shule hapo juu wamewekeza kwanzia miundo mbinu mpk kuwalipa walimu vizuri
1. Ushirikiano kati ya walimu,wazazi/walezi, wanafunzi na utawala wa shule jambo ambalo linawezesha kila mtu kutimiza wajibu wake katika mazingira yenye utulivu.

2. Mazingira mazuri (shule ilipo, madarasa ya kutosha, mabweni, vyoo na mahitaji mengine sawa na hayo).

4. Maktaba bora.

5. Maabara yenye vifaa vya kutosha.

6. Walimu wa kutosha wenye sifa na wanaojituma.

7. Ibada.
8. Motisha kwa Walimu.
 
Wale wa St Fransis,Marian,Feza,Ahmes na nyingi za Kikatoliki mbona wanafaulu kwenye hiyo format mpya.Hapa tuna la kujifunza kutoka kwao hasa kwenye uwekezaji katika miundo mbinu bora na motisha kwa walimu.
 
Siyo Physics tu hata Hisabati wamebadili mfumo wa utungaji maswali.
Hivi Shule yenye wanafunzi 1500 na walimu wawili unafikiri watafundishwa kwa kuelewa au kukariri?
 
Masomo ya Sayansi Kiukweli ni Magumu huwezi linganisha Hesabu, Fizikia , Chemistry na masomo ya Sanaa
 
Tatizo ni waalimu wa hayo masomo wana vipindi vingi, mtu ana vipindi 30 kwa wiki, anazunguka madarasa yote kufundisha halafu mshahara unalingana na mwalimu mwingine mwenye vipindi viliwi(double) kwa wiki.
Hapo mwalimu wa hayo masomo lazima afundishe siku ziende ila sio wanafunzi waelewe.

Serikali inatakiwa iwalipe posho walimu hao.
 
Kwa nini shule za private zimeonyesha kufaulu kwenye fizikia na hesabu? Labda tuanzie hapo
Ukifeli wastani unafunga mabegi yako mapema tu hawana mchezo. Ila huku Chamwino secondary school hata upate wastani wa 8% utasoma hadi mtihani wa taifa ukukute
 
Mara nyingi kila matokeo yanapo toka ndio tunashtuka na tunaanza kuangalia nani kakosea nini au nini kimekosekana wapi, ila swala la Elimu hatuwezi kulitatua kwa kuliangalia kwa vipande vipande yaani kama tuamue kutatua kwa labda kuongeza waalimu wa masomo yenye ufaulu mdogo au kuamua kuongeza vitabu kwa baadhi ya masomo,
Swala la Elimu lazima tuliangalie na kuliboresha ktk mapana yake ili tuweze pata matokeo chanya na ya mda mrefu.
1. Kwanza kabisa Lazima tumuangalie mwanafunzi, na tumjenge awetayali kupokea elimu tunayo mpatia kuanzia anatoka nyumbani mpaka shule, tuwe na mpango mkakati juu ya elimu tunayo mpatia, nafasi ya matumizi ya elimu hiyo ktk jamii inayo mzunguka.
2. Pili, watoa elimu kwa maana ya waalimu, tangu vyuoni inabidi tumuandae mwalimu kwa lengo la kumtengeneza mwanafunzi, mwalimu ni kiungo muhimu sana ktk makuzi ya mwanafunzi. ( tunaitaji pia mwalimu wa ku mmotivate mwanafunzi, mwalimu wa kumfundisha nidhamu, usafi, utu na mambo kama haya ambayo mara nyingi huwa tunayasahau)
3. Tatu, miundombinu na vifaa bora kwa ajili ya kutolea elimu. Bila kusaha mazingira bora ya shule ikijumuisha upande wa mwalimu pia yaani makazi bora, mishahara na posho za kulipwa kwa wakati.
 
Ukifeli wastani unafunga mabegi yako mapema tu hawana mchezo. Ila huku Chamwino secondary school hata upate wastani wa 8% utasoma hadi mtihani wa taifa ukukute
Iliboru nao wanafungasha mabegi😂😂
 
Shida NI kwamba HAKUNA walimu wala physics Wala hisabati was kutosha
Na wengi wanaona ualimu gozigozi wanaenda kusoma uhasibu enveneering na kozi nyingine
Hawapo kabisa
 
Wazazi waache kuwalisha Watoto chips Kuku badala yake wawalishe Ngano ( Chapati) + vichwa vya Samaki mfano Sato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…