Serikali iongeze umri wa kuanza kubeti (na sisi wenye miaka 14 tupewe nafasi

Serikali iongeze umri wa kuanza kubeti (na sisi wenye miaka 14 tupewe nafasi

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,380
Reaction score
1,686
Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️

Nimeona serikali ikisema kubeti kuanzia ni miaka 18+.
Sasa miaka 18+ niwazee hao na sisi vijana wa miaka 17- tunaitaka hii fursa ya mama samia ya kucheza kamari ambayo katuletea.

Maana leo vituo vya habari vya taifa vyote vinahamasisha sasa hii inatunyima Fulsa sasa vijana wa makamo.

Leo ukifungulia radio mambo ni hayohayo magazeti pia na hata televisheni za taifa mambo ni KUBASHIRI.
Pia naiomba wizara ya fedha na kubashiri watuletee mpaka vyiuoni yale madude unatia 200 unapata 20,000 maana zile era ni za bure.
Nayaona tu mitaani kila kona akina mama wakicheza na wazee sasa na sisi watoto tunataka maana leo asubuhi nataka kwenda shule nimeliona barazani kwetu limewekwa.

Afu kuna na kale Kandege namuonaga baba anakarusha yaani kanamwaga ela kama mchanga. Nyumbani tunakula na kusaza kwa kale Kandege. Hongera sana kwa serikali.



Asante naomba kuwasilisha kwenye serikali yenye wa wahuni ya wacheza kamali na kubashiri.
Natoa shukurani kwa waziri asiyejielewa aliyefanikisha kupitisha huu mpango na Tanzania kuwa miongoni mwa taifa la watu wa kubashiri.

Tupo pamoja mpaka tunaangamia kabisa.
 
Haha kanji atawanyoosha nyie njooni tu

Kwamba GG washambuliaji umeweka wewe sio
 
Serikali ifungie makampuni ya kubet maana betting inadumaza akili za vijana .
 
Nashauri kujiunga Jamiiforums ime mandatory kutumia NIDA, au mnasemaje wadau?
 
Back
Top Bottom