Serikali ipige marufuku watoto wadogo kushirikishwa kwenye majukwaa ya wasanii

Serikali ipige marufuku watoto wadogo kushirikishwa kwenye majukwaa ya wasanii

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Leo huko Kigamboni Dar es Salaam lilikuwepo tamasha la muziki, moja ya mambo ambayo hayakubaliki ni utesaji wa watoto wadogo akiwemo huyu pichani mwenye umri chini ya miaka kumi!

Mtoto huyu amewekwa kwenye jukwaa linalopiga muziki wenye sauti ya zaidi ya wati 20,000! Masikio ya mtoto huyu hayawezi kuhimili kelele hizo, anaumia.

IMG_20231216_175244.jpg
 
Hapo anaandaliwa,wana muinspire mkata mauno wa badaye
Hii nchi mpaka 2035 itakuwa kama kongo ,watajaaa wakata mauno tu
Maana ukipita mitaani kila mtu ni kukata mauno

Ova
 
Leo huko Kigamboni Dar es Salaam lilikuwepo tamasha la muziki, moja ya mambo ambayo hayakubaliki ni utesaji wa watoto wadogo akiwemo huyu pichani mwenye umri chini ya miaka kumi!

Mtoto huyu amewekwa kwenye jukwaa linalopiga muziki wenye sauti ya zaidi ya wati 20,000! Masikio ya mtoto huyu hayawezi kuhimili kelele hizo, anaumia.

View attachment 2844189
Mabadiliko yanaanza na mimi, wewe na yule kwenye ngazi ya familia.

Siyo kila kitu iwe serikali. Maana kama wazazi wenyewe hawajielewi serikali haitaweza kudhibiti kila kitu kinachohusiana na maadili kama sisi wenyewe hatuwezi kuona umuhimu wake.

Kuna mambo mengi sana kuhusiana na watoto na haki zao ambayo hayaonekani kama yana maana yoyote ile.

Watoto wengi wako kwenye ma garage, “wa kujifunza ufundi” AKA manyoka, kwa mama ntilie, ambapo wanalipwa 5,000 kwa siku kuzungusha vyakula sehemu mbali mbali huku wakidhalilishwa kingono nk, kwenye bar na madanguro.

Sasa hao watoto hata wakinyimwa hayo na serikali, na huku wazazi hawajali, si wanaendelea kuyafanya kwenye private parties nk? Ambako kuna ma DJ wanapiga miziki?
 
Mabadiliko yanaanza na mimi, wewe na yule kwenye ngazi ya familia.

Siyo kila kitu iwe serikali. Maana kama wazazi wenyewe hawajielewi serikali haitaweza kudhibiti kila kitu kinachohusiana na maadili kama sisi wenyewe hatuwezi kuona umuhimu wake.

Kuna mambo mengi sana kuhusiana na watoto na haki zao ambayo hayaonekani kama yana maana yoyote ile.

Watoto wengi wako kwenye ma garage, “wa kujifunza ufundi” AKA Kanyika, kwa mama ntilie, ambapo wanalipwa 5,000 kwa siku kuzungusha vyakula sehemu mbali mbali huku wakidhilishwa kingono nk, kwenye bar na madanguro.

Sasa hao watoto hata wakinyimwa hayo, na wazazi hawajali, si wanaendelea kuyafanya kwenye private parties nk? Ambako kuna ma DJ wanapiga miziki?
Kwenye tamasha hili alikuwepo mhe. Mwigulu ambaye angeweza kuhoji uonekano wa mtoto huyo jukwaani kwani alionekana pia akimsumbua mlinzi wa baba yake.
 
Leo huko Kigamboni Dar es Salaam lilikuwepo tamasha la muziki, moja ya mambo ambayo hayakubaliki ni utesaji wa watoto wadogo akiwemo huyu pichani mwenye umri chini ya miaka kumi!

Mtoto huyu amewekwa kwenye jukwaa linalopiga muziki wenye sauti ya zaidi ya wati 20,000! Masikio ya mtoto huyu hayawezi kuhimili kelele hizo, anaumia.

View attachment 2844189
Hivi mzazi wa huyu mtoto alikuwa wapi? Usikute hapa ni saa 6 usiku mtoto anajivinjari na bongo fleva.
 
Hivi mzazi wa huyu mtoto alikuwa wapi? Usikute hapa ni saa 6 usiku mtoto anajivinjari na bongo fleva.
Mzazi ndiye huyo anayemzibua masikio mwanae na huyo ni Zuchu, alipanda naye jukwaani akiwa amembeba kisha akamtua chini na kumuweka pembeni ya spika ili naye ajifunze kuimba.
IMG_20231216_175244.jpg
 
Hapa tuwatake wanaojifanya eti wanatetea haki za watoto wako wapi? Au hili hawalioni kuwa haliwafai watoto au uelewa wao ni mdogo kuhusu mambo yapi hayawafai watoto.
 
Serikali yangu najua imeshindwa Mengi ila kushindwa kuwalinda Hawa watoto ni kosa ambalo halivumiliki.Hapo kwanza mzazi anatakiwa awe ndani,na hao waandaaji wakati mtoto akipatiwa matibabu ya kisaikolojia.The future is dark as hell tukiendelea kucheka Cheka na Hawa tuliowapa dhamana.
 
Back
Top Bottom