Serikali ipunguze bei ya viwanja vya kujengea viwanda, hadi 1000 kwa sqm 1 au 500 kwa sqm 1. Ili kuongeza ajira kwa vijana kupitia viwanda vidogo

Serikali ipunguze bei ya viwanja vya kujengea viwanda, hadi 1000 kwa sqm 1 au 500 kwa sqm 1. Ili kuongeza ajira kwa vijana kupitia viwanda vidogo

Akilindogosana

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2020
Posts
4,303
Reaction score
12,679
Serikali ipunguze bei ya viwanja vya kujengea viwanda, viwanja vya kuweka biashara. Kuuza kiwanja cha kiwanda kwa @20,000 kwa mita moja ya mraba au 30,000 kwa sqm au 50,000 kwa sqm ni bei juu mno na inaua uzalishaji wa bidhaa hasa kwa vijana na wazawa, hakuna kijana mwenye milioni 500 au 1B kwa ajili ya kununua kiwanja cha kiwanda. Hapo kwa bei hiyo labda anunue mtu tajiri sana au mwekezaji toka china, india, asia, marekani au ulaya.

Kuuza kiwanja cha kiwanda kwa 30,000 au 50,000 kwa square meter ni UJINGA sana

Pakiwa na viwanda vidogo vingi vitaongeza ajira kwa vijana, na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Serikali ipunguze kodi kwenye mashine na mitambo mbalimbali ya kuzalisha na kuchakata bidhaa za kilimo, ufugaji, Madini,uvuvi.

Bei ya kiwanja cha kiwanda kwa ajili ya vijana inatakiwa iwe 1000 kwa sqm au ikiwezana iwe hata shilingi miatano kwa square meter. Ili vijana wawe na maeneo yao ya kuwa na viwanda vidogo hata kwa laki tano. Vijana watashirikiana kuzalisha bidhaa na kuuza. Hivyo kuongeza ajira kwa vijana

Mfano halisi
Screenshot_20250226-104551~2.png

Hicho ni kiwanja cha kujenga kiwanda kinauzwa na serikali kwenye mfumo wa tausi kipo Kibaha Mkoa wa Pwani angalia bei ya kiwanja cha kiwanda kinauzwa 600m. Je kuna kijana au mtanzania wa kawaida anayeweza kununua tu eneo kwa 600m?

Hii sio sawa, bei ni 30,000 kwa sqm 1

Kama serikali ina nia ya dhati ya kuzalisha ajira wapunguze bei ya viwanja vya kujengea kiwanda kuwa 1000 kwa sqm au 500 kwa sqm. Vijana wanunue kwa bei ndogo wawe bize kuzalisha bidhaa na kuchakata bidhaa za kilimo, uvuvi, ufugaji, Madini n.k
 
Bei ziko juu mno. Hapo ni mpaka aje mwekezaji toka nje ya nchi kuwekeza. Na anaweza kuzalisha bidhaa ambazo hata sisi watanzania tunaweza kuzalisha. Ni aibu sana.
 
May be useme kuwe na maeneo maalum ya ukubwa mdogo kwa ajili ya viwanda vidogo, lakini SQM 20000 au 30000 lazima ujikamue
 
Ardhi ni sekta yenye thamani, hivyo uthamini umefanyika

Kiwanja kama hicho huwezi kipata kigoma au katavi kwa bei hiyo

Unaweza tafuta eneo ambalo unalimudu na kuanza nalo taratibu au ukatafuta wabia ktk biashara na uwekezaji wako, usikate tamaa bado Kuna njia ukiamua
 
Tanzania ni kubwa sana, kuna maeneo mpaka kuja kuyafikia itachukua muda kidogo.

Tungeanza kugawa haya maeneo kwa kuya categorize, sehemu ya viwanda vidogo au wafanyabiashara wadogo na kwa bei nafuu vile vile na sehemu kama hizi umeandika mtoa mada kwa bei hizo ambazo zipo hapo.

Kuweka bei sawa bila kuyagawa ni kuwaonea wafanyabiashara wadogo.
 
Upo sahihi kabisa kuweka bei ya @30000 kwa sqm au 50000 kwa sqm ni UJINGA mkubwa mno.
 
May be useme kuwe na maeneo maalum ya ukubwa mdogo kwa ajili ya viwanda vidogo, lakini SQM 20000 au 30000 lazima ujikamue
Bei elekezi ya ardhi ipo juu mno. Hapo tutaishia kuwafaidisha wawekezaji toka nje tu. Sisi tutabakia maskini na vijana wengi zaidi wasio na ajira. Bei ikiwa juu maeneo yanakaa wazi tu
 
Back
Top Bottom