Vijana wengi nikiwemo mimi mwenyewe ni wahanga, tunakosa fursa na tunabanwa na kujiunga vyuo vikuu kusoma degree baada ya kuhitimu diploma za afya kama ifuatavyo.
Mtu unasoma Diploma in Clinical Medicine kwa kutumia Cheti cha Form Four katika combination ya PCB, mimi binafsi nina C ya Chemistry, C ya Biology na D ya Physics nilifeli tu hesabu, nikaomba chuo nikapata na nimemaliza nimepewa leseni nafanya kazi.
Ila sasa hivi kusoma degree eti unatakiwa mpaka uwe na walau d grade ya Hesabati ilhal tayari nina diploma na niliposoma hiyo diploma sikudaiwa Math na kibaya zaid nje ya nchi unasoma bila Hesabu lakini pia hapa hapa kwetu Tanzania wanaotoka form 6 wanasoma bila hesabu pia why?
Tunaomba tuliosoma Diploma za Medicine kwa vile tumepewa vyeti na leseni tuonewe huruma tutumie PCB ya Form 4 na vyeti vya diploma tukasome Doctor of Medicine Degree. Inakujawe mtu anatoka form 6 fresh school anaruhusiwa tena. Bila Math kusoma MD LKN SIS wenye profession tayari tunabanwa kisa Hesabu.
Mtaala wote unalazimisha hesabu kwa wanaotoka diploma kutaka MD ila kwanini Form 6 hawajui hata medicine wao wanaruhusiwa kusoma MD bila math kwanini lakini tunaomba Serikali ituone kwa hili.
Nimesoma hapahapa Zanzibar, Chemistry nilipata C, Biology C, Physics D english C, Geography D, Dini ya Kiislam D, Math F nikapata division 3 point 23 ila nimesoma chuo nimepata first class 4.6GPA OUT OF 5.
Nataka kuenda degree naambiwa lazima Math why this na mpaka leo watu wanasoma diploma hawana Math na wanakubaliwa sasa kwanini watukubali afu degree watuzuie tena tayari tuna professionalism yetu ila form six wawachukue bila Bath na hawana profession ni fresh from school.
Hii ni changamoto inatusakama wengi, ajira hamna mtu unataka ukasome at least degree zinatoka ajira tutumiie taifa letu ila still tunabanwa.
Nilisoma Zanzibar School of Health, ni private na ni chuo bora sana kwa Zanzibar, kimeshatoa madaktari wengi tu.