Serikali iruhusu ushindani wafanyakazi wajiunge na bima ya afya wanayoitaka

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
2,828
Reaction score
3,579
Hadi sasa kuna kampuni nyingi za bima ya afya nchini ikiwemo NHIF. Cha ajabu, katika mazingira sawa ya kibiashara licha ya NHIF kuwa na upendeleo wa kuwa na wanachama wengi kuliko kampuni zote za bima nchini kwa kujaziwa wanachama lukuki kutoka serikalini na taasisi za serikali, ni NHIF pekee ndiyo yenye huduma mbovu na kila kukicha inaleta mbinu za kuumiza wanachama zaidi. Wenzao akina Jubilee, Strategis nk wanaendelea vizuri. Matokeo yake wananchi ndio wanaumia kupitia utendaji mbovu wa NHIF.
Ushauri wangu kwa serikali, iruhusu ushindani, mtumishi wake achague bima anayotaka miongoni mwa zinazofanya huduma nchini. Na hata wananchi wote wengine waliobaki, wachague bima wanayoipenda tusiwalazimishie NHIF. Katika utaratibu wa public-private partnership, kampuni zote za bima ziruhusiwe kujitangaza na kuandikisha wanachama kutoka kila kundi nchini, ikiwemo watumishi wa serikali na taasisi zake. Halafu biashara ya bima iendeshwe kiushindani, kampuni itakayoshindwa hata kama ni NHIF ikafilie mbali, lengo liwe ni kuhudumia wananchi na siyo kuibeba NHIF.
 
Hiyo ni remedial action, but lazima kuwe na scientific approach ya kusuluhisha matatizo yaliyopo ili NHIF iwe stable and sustainable.

Kwanza, wajue mataatizo yanazalishwa na kitu gani, gap kwenye sheria au uongozi mbaya;

Pili, wajitathmini kama wanahitaji kuhodhi soko lote, yaaani watumishi wa umma na raia wa kawaida;

Tatu, watengeneze catalogues of medicines and services ikiwa na indicative prices ili kupunguza ubabaishaji na ku-predict their financial liability ambayo ita determine realistic premium ambayo wanachama wanapaswa kuchangia; na

Mwisho, wa automate process zote
 
Hadi sasa kuna kampuni nyingi za bima ya afya nchini ikiwemo NHIF. Cha ajabu, katika mazingira sawa ya kibiashara licha ya NHIF kuwa na upendeleo wa kuwa na wanachama wengi kuliko kampuni zote za bima nchini kwa kujaziwa wanachama lukuki kutoka serikalini na taasisi za serikali, ni NHIF pekee ndiyo yenye huduma mbovu na kila kukicha inaleta mbinu za kuumiza wanachama zaidi. Wenzao akina Jubilee, Strategis nk wanaendelea vizuri. Matokeo yake wananchi ndio wanaumia kupitia utendaji mbovu wa NHIF.
Ushauri wangu kwa serikali, iruhusu ushindani, mtumishi wake achague bima anayotaka miongoni mwa zinazofanya huduma nchini. Na hata wananchi wote wengine waliobaki, wachague bima wanayoipenda tusiwalazimishie NHIF. Katika utaratibu wa public-private partnership, kampuni zote za bima ziruhusiwe kujitangaza na kuandikisha wanachama kutoka kila kundi nchini, ikiwemo watumishi wa serikali na taasisi zake. Halafu biashara ya bima iendeshwe kiushindani, kampuni itakayoshindwa hata kama ni NHIF ikafilie mbali, lengo liwe ni kuhudumia wananchi na siyo kuibeba NHIF.
Tatizo kubwa ni forgeries za watu wa sekta binafsi. Mifuko ya bima ya binafsi inausimamizi wa hali ya juu kuhusu madai na huduma ila huu wa NHIF nadhani kuna collusions.
 
But Kuna misuse of fund pia
 
Mashirika ya Umma yamejaa makada watiifu wa chama Cha fisiemu hivyo watu kupewa nafasi sababu ya itikadi na undugulization badala ya sifa stahiki pia yamekaa kijimaa sana kwa kutegea upendeleo toka serikalini badala ya ushindani.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mwenda zake alichukua 56b za NHIF kufadhili kundi la wasiojulikana lililokuwa likiongozwa na Kingai
 
Waziri kasema NHIF ipo taabani na sababu inadaiwa kuwa ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza yanayotibiwa kwa gharama kubwa miongoni mwa wanachama wake.

Suluhisho ni kuiongeza NHIF wanachama/wachangiaji kupitia Bima ya Afya kwa wote! Sawa.

SWALI:Hao wachangiaji wapya wao wana chanjo dhidi ya magonjwa yanayoifilisi NHIF?

Kuongeza wachangiaji ni kuongeza wagonjwa vilevile, sioni NHIF inanusurikaje kwa staili hii.
 
Tatizo siyo mfuko wala wataalamu wake, bali tatizo ni ccm
 
NHIF badala ya kutoa huduma yenyewe inataka ifanye na biashara, mpk inakopesha
 
Hadi sasa kuna kampuni nyingi za bima ya afya nchini ikiwemo NHIF. Cha ajabu, katika mazingira sawa ya kibiashara licha ya NHIF kuwa na upendeleo wa kuwa na wanachama wengi kuliko kampuni zote za bima nchini kwa kujaziwa wanachama lukuki kutoka serikalini na taasisi za serikali, ni NHIF pekee ndiyo yenye huduma mbovu na kila kukicha inaleta mbinu za kuumiza wanachama zaidi. Wenzao akina Jubilee, Strategis nk wanaendelea vizuri. Matokeo yake wananchi ndio wanaumia kupitia utendaji mbovu wa NHIF.
Ushauri wangu kwa serikali, iruhusu ushindani, mtumishi wake achague bima anayotaka miongoni mwa zinazofanya huduma nchini. Na hata wananchi wote wengine waliobaki, wachague bima wanayoipenda tusiwalazimishie NHIF. Katika utaratibu wa public-private partnership, kampuni zote za bima ziruhusiwe kujitangaza na kuandikisha wanachama kutoka kila kundi nchini, ikiwemo watumishi wa serikali na taasisi zake. Halafu biashara ya bima iendeshwe kiushindani, kampuni itakayoshindwa hata kama ni NHIF ikafilie mbali, lengo liwe ni kuhudumia wananchi na siyo kuibeba NHIF.
Izo insurance unazosema tumeshawahi kuwa wanachama, ... its the same issue ..Na kama huna evidence kama mwanachama wa Insurance zote hizo kaa kimya. Unafahamu viwango vya uchangiaji vya makampuni yote? Unajua huduma unapata kwa kiwango gani. Hoja iwe na info ya kutosha ili ueeze kueleweka.
 
Huko kwingine mtaweza gharama za makato yao? Au unafikiri bei sawa na nhif? NHIF ni nafuu
 
Tatizo kubwa ni forgeries za watu wa sekta binafsi. Mifuko ya bima ya binafsi inausimamizi wa hali ya juu kuhusu madai na huduma ila huu wa NHIF nadhani kuna collusions.
Basi kama NHIF inashindwa kusimamia madai na huduma ijifie tu, ibaki mifuko inayoweza kazi hiyo.
 
Izo insurance unazosema tumeshawahi kuwa wanachama, ... its the same issue ..Na kama huna evidence kama mwanachama wa Insurance zote hizo kaa kimya. Unafahamu viwango vya uchangiaji vya makampuni yote? Unajua huduma unapata kwa kiwango gani. Hoja iwe na info ya kutosha ili ueeze kueleweka.
Nina uzoefu na Jubilee na Stretegis, na huduma zao ni nzuri. Sijawahi kukutana na mauzauza kama hayo ya NHIF
 
Kuna sehemu ya tatizo ambalo halisemwi. Tatizo letu Watanzania la udanganyifu.
Ni sisi ambao tunawapa kadi zetu za bima ndugu zetu wakatibiwe. Ama tunawashawishi watoa huduma (kwa rushwa) au kwa upande wa watoa huduma binafsi hawafanyi due diligence kuuna anayetaka kutibiwa ni mwenye kadi halisi.
 
Mwenda zake alichukua 56b za NHIF kufadhili kundi la wasiojulikana lililokuwa likiongozwa na Kingai
Huu ni upumbav wa kuleta utani kwenye hoja ya msingi ..watu wanajadili hoja muhimu wewe unaleta ujingaujinga hapa..ukiambiwa ulete ushahidi hapa utaleta....mwendazake watu walimwelewa kiasi kwamba hata uwaambie aliiba trilion moja, watu watakwambia sawa..wataridhika..na ndio Serikali yetu hii pia ni sehem yake,. Wanaendelea kuchapa kazi mpaka mnyooke..msidhan mtapata nafasi ya kuongoza nchi kirahisi..nyie endeleeni kutafuta makaratasi ya katiba tu
 
Back
Top Bottom