Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,828
- 3,579
Hadi sasa kuna kampuni nyingi za bima ya afya nchini ikiwemo NHIF. Cha ajabu, katika mazingira sawa ya kibiashara licha ya NHIF kuwa na upendeleo wa kuwa na wanachama wengi kuliko kampuni zote za bima nchini kwa kujaziwa wanachama lukuki kutoka serikalini na taasisi za serikali, ni NHIF pekee ndiyo yenye huduma mbovu na kila kukicha inaleta mbinu za kuumiza wanachama zaidi. Wenzao akina Jubilee, Strategis nk wanaendelea vizuri. Matokeo yake wananchi ndio wanaumia kupitia utendaji mbovu wa NHIF.
Ushauri wangu kwa serikali, iruhusu ushindani, mtumishi wake achague bima anayotaka miongoni mwa zinazofanya huduma nchini. Na hata wananchi wote wengine waliobaki, wachague bima wanayoipenda tusiwalazimishie NHIF. Katika utaratibu wa public-private partnership, kampuni zote za bima ziruhusiwe kujitangaza na kuandikisha wanachama kutoka kila kundi nchini, ikiwemo watumishi wa serikali na taasisi zake. Halafu biashara ya bima iendeshwe kiushindani, kampuni itakayoshindwa hata kama ni NHIF ikafilie mbali, lengo liwe ni kuhudumia wananchi na siyo kuibeba NHIF.