Serikali iruhusu uwekezaji wa kibiashara katika Magereza ili wafungwa wanaoweza kugharamia walipie na kutumikia vifungo vyao

bize signal

Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
29
Reaction score
50
Kwanza kabisa niwasalimu kwa salamu ya kitaifa, KATIBA MPYA WANA JF.

Kimsingi nimekuwa nikijalibu kupata taarifa mbalimbali za huduma za magereza duniani.

Unapozilinganisha na za magereza zetu unaona ni kwa jinsi gani hali ilivyo mbaya kwa magerza zetu. Na kwa kuwa lengo la kuwa na magereza sio kuwapa watu huduma mbovu kiasi cha watu wengine kuugua na hasa kutokana na msongamano.

Mimi ninalo wazo jipya au ushauli kwa serekali Muda umefika serekali ifanye mabadiliko makubwa.

Iluhusu wawekezaji wa kibiashara katika magereza za kisasa ili wafungwa wenye kuweza kughalimia walipie na kutumikia vifungo vyao huko. hii itaweza saidia serekari kupunguza bajeti za huduma na kuboresha huduma kwa waliobaki katika gereza za serekali.

Hii haina tofauti na shule za private
Hii haina tofauti na bank binafsi
Hii haina tofauti na hospital private

Zingatia jambo la msingi kwa mfungwa ni kunyimwa uhuru wa kufanya mambo yake kwa taratibu zake.

Serekali ibaki na jukumu la kuwaweka askali wa magereza kuakikisha mfungwa yupo salama anatumikia kifungo(adhabu) aliopewa kwa mujibu wa sheria. swala la huduma linabaki kutolewa na muwekezaji (maradhi, chakula nk)

serekali inaweza tengeneza au kubolesha mazingira mengineyo. wewe msomaji weka hoja yako ili mfumo uweje.JAMBO JIPYA SIO LAZIMA LIANZIE ULAYA.

Nawakilisha.
 
Hili nasikia linafanyika Marekani. Lina faida na changamoto zake.

Serikali ingejenga gereza walau moja lenye viwango vya kimataifa, ikiwa halipo.

Hayo ya sekta binafsi, uendeshaji wake usitegemee wingi wa wafungwa wanaopelekwa hapo, kwani idara ya masoko ya magereza husika itataka kupata wateja wengi 😉
 
Utavunja msingi mkubwa wa sheria wa "haki sawa kwa wote".

Pia, hivi magereza hayaendeshwi kibiashara tu, watu wanabambikiwa kesi.

Ukianza kuendesha magereza kibiashara, tegemea kuona watu, hususan masikini wasioweza kujitetea, wanabambikiwa kesi zaidi ili magereza yajae na wawekezaji wapate faida.

Hili ni tatizo linaloonekana sana Marekani kwenye mfumo wa uwekezaji binafsi kwenye magereza. Wenyewe wanaita "prison-industrial complex"

Tunaoishi Marekani tunaona madhara ya hiki kitu.

Kwa habari zaidi kuhusu ubaya wa mfumo huu Marekani, anzia hapa.

Nadhani tungejadili ni namna gani iwezekane kwani toka nchi hii imekuwepo hali za magereza zetu sio sawa na ndio maana kamera ni adui namba moja gerezani!! au kungekuwa na VIP sawa na hospital. kwani lengo sio kuishi kwa tabu na adha zile ndani ya gereza!! Angalia gereza za norway kisha pima hali ya tz yetu, utagundua bila msaada au njia mbadala serekali itaighalimu miaka mingi sana.
 
Utavunja msingi mkubwa wa sheria wa "haki sawa kwa wote".

Pia, hivi magereza hayaendeshwi kibiashara tu, watu wanabambikiwa kesi.

Ukianza kuendesha magereza kibiashara, tegemea kuona watu, hususan masikini wasioweza kujitetea, wanabambikiwa kesi zaidi ili magereza yajae na wawekezaji wapate faida.

Hili ni tatizo linaloonekana sana Marekani kwenye mfumo wa uwekezaji binafsi kwenye magereza. Wenyewe wanaita "prison-industrial complex"

Tunaoishi Marekani tunaona madhara ya hiki kitu.

Kwa habari zaidi kuhusu ubaya wa mfumo huu Marekani, anzia hapa.

kubambikiwa kesi ni mjadala unaoweza kujitegemea tofauti!. na wakibambikiwa wote wanaishia gereza hizihizi. swala ni kubadili hali ilivyo katika gereza zetu.
 
Unaweza kubadilisha hali katika magereza bila kufanya magereza yaendeshwe kwa biashara.

Ukishaanza kufanya magereza yaendeshwe kwa biashara, na ikiwa magereza yanayojaa wafungwa yanatengeneza biashara nzuri zaidi kuliko magereza matupu, hapo ndipo mwanzo wa kesi za kubambikiwa kuongezeka, ili magereza yajae, ili biashara zipate faida zaidi.

Huoni mantiki hii rahisi tu?
 
Kwanza kabisa niwasalimu kwa salamu ya kitaifa, KATIBA MPYA WANA JF.

Kimsingi nimekuwa nikijalibu kupata taarifa mbalimbali za huduma za magereza duniani.

Unapozilinganisha na za magereza zetu unaona ni kwa jinsi gani hali ilivyo mbaya kwa magerza zetu. Na kwa kuwa lengo la kuwa na magereza sio kuwapa watu huduma mbovu kiasi cha watu wengine kuugua na hasa kutokana na msongamano.

Mimi ninalo wazo jipya au ushauli kwa serekali Muda umefika serekali ifanye mabadiliko makubwa.

Iluhusu wawekezaji wa kibiashara katika magereza za kisasa ili wafungwa wenye kuweza kughalimia walipie na kutumikia vifungo vyao huko. hii itaweza saidia serekari kupunguza bajeti za huduma na kuboresha huduma kwa waliobaki katika gereza za serekali.

Hii haina tofauti na shule za private
Hii haina tofauti na bank binafsi
Hii haina tofauti na hospital private

Zingatia jambo la msingi kwa mfungwa ni kunyimwa uhuru wa kufanya mambo yake kwa taratibu zake.

Serekali ibaki na jukumu la kuwaweka askali wa magereza kuakikisha mfungwa yupo salama anatumikia kifungo(adhabu) aliopewa kwa mujibu wa sheria. swala la huduma linabaki kutolewa na muwekezaji (maradhi, chakula nk)

serekali inaweza tengeneza au kubolesha mazingira mengineyo. wewe msomaji weka hoja yako ili mfumo uweje.JAMBO JIPYA SIO LAZIMA LIANZIE ULAYA.

Nawakilisha.
😂😂😂😂😂😂😂

Nimecheka kwa sauti.

Ila umefikiria kuwa nchi yetu ni miongoni mwa nchi ambazo bado tunabambikiziana kesi???

Hayo magereza yakiwepo ujue wamiliki wake watakuwa mahakimu, Askari Magerza na mapolisi 😂😂😂

Au wamiliki wake lazima watakuwa wanakula na hao watu. Kwa mantiki hiyo tegemea nyundo za kutosha 😂😂😂😂

Ni wazo zuri lakini kwa sasa tuliache kwanza. Ni rahisi zaidi kuboresha hali za magereza yetu hayahaya.
 
Hivi hapa hakuna vifungo vya nyumbani kwa wanasiasa?

Na hao wanaofungwa kwa sababu nyingine (vibaka nk) wangekuwa wanafanya kazi kama kujenga barabara na za kuzalisha kuko huko selo kwa kulipwa kima cha chini ili wakitoka wawe na pesa za kuwasaidia kuanzisha hata vibiashara ....bila ya hivi ni rahisi kuona wanarudia tena makosa yao wakirudi uraiani bila pesa..
 
😂😂😂😂😂😂😂

Nimecheka kwa sauti.

Ila umefikiria kuwa nchi yetu ni miongoni mwa nchi ambazo bado tunabambikiziana kesi???

Hayo magereza yakiwepo ujue wamiliki wake watakuwa mahakimu, Askari Magerza na mapolisi 😂😂😂

Au wamiliki wake lazima watakuwa wanakula na hao watu. Kwa mantiki hiyo tegemea nyundo za kutosha 😂😂😂😂
Kabla ya kuichukua mifumo, inabidi tuchunguze nchi ambazo mifumo hiyo ipo zinaendaje na mifumo hiyo.

Nimetoa mfano wa Marekani hapo juu. Marekani ndiyo nchi yenye wafungwa wengi zaidi kiujumla na kama sehemu ya watu wake duniani.

Soma hizi statistics za mwaka 2016 hapa.

"The United States has the highest prison and jail population (2,121,600 in adult facilities in 2016), and the highest incarceration rate in the world (655 per 100,000 population in 2016).

Na hili limewezekana kwa sababu ulizozitaja zilizotokana na kuendesha magereza kibiashara.

Ukishaanza kuendesha magereza kibiashara, unaweka incentive ya wafungwa kuongezeka bila kujali watu wanaofungwa wana hatia au la.

Haya ndiyo mambo tunayotaka kuiga huko kwetu?
 
Kwanza kabisa niwasalimu kwa salamu ya kitaifa, KATIBA MPYA WANA JF.

Kimsingi nimekuwa nikijalibu kupata taarifa mbalimbali za huduma za magereza duniani.

Unapozilinganisha na za magereza zetu unaona ni kwa jinsi gani hali ilivyo mbaya kwa magerza zetu. Na kwa kuwa lengo la kuwa na magereza sio kuwapa watu huduma mbovu kiasi cha watu wengine kuugua na hasa kutokana na msongamano.

Mimi ninalo wazo jipya au ushauli kwa serekali Muda umefika serekali ifanye mabadiliko makubwa.

Iluhusu wawekezaji wa kibiashara katika magereza za kisasa ili wafungwa wenye kuweza kughalimia walipie na kutumikia vifungo vyao huko. hii itaweza saidia serekari kupunguza bajeti za huduma na kuboresha huduma kwa waliobaki katika gereza za serekali.

Hii haina tofauti na shule za private
Hii haina tofauti na bank binafsi
Hii haina tofauti na hospital private

Zingatia jambo la msingi kwa mfungwa ni kunyimwa uhuru wa kufanya mambo yake kwa taratibu zake.

Serekali ibaki na jukumu la kuwaweka askali wa magereza kuakikisha mfungwa yupo salama anatumikia kifungo(adhabu) aliopewa kwa mujibu wa sheria. swala la huduma linabaki kutolewa na muwekezaji (maradhi, chakula nk)

serekali inaweza tengeneza au kubolesha mazingira mengineyo. wewe msomaji weka hoja yako ili mfumo uweje.JAMBO JIPYA SIO LAZIMA LIANZIE ULAYA.

Nawakilisha.
Usipoteze muda mkuu,,Africa jela ni jehanam .
Sio kuzuia Uhuru wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufungwa ni kunyimwa Uhuru na sio mateso.

Kumlaza binadamu mchongoma ni kukiuka haki za binadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni hivyo wengi sana tungeenda huko tena kwa hiari.
Wengine mitaani tunaishi kwa mateso ni zaidi ya gereza la kibongo. Sasa huku pakiwa na chips kuku....hakuna wa kubaki mtaani
 
Jela ni kunyimwa uhuru wa kufanya yako kwa hiayari.
Unapangiwa cha kufanya.
Jela ni sehem ya kujirekebisha ulipokosea.
Jela ni kujifunza maisha mapya.
Jela sio mateso..

Ni Africa pekee na Asia jela ni zaidi ya jehanam.

Mimi nimekaa jela ulaya.
Hakika ni zaidi ya hotel 5 star na pesa nimepewa.
Na still sitamani nirudi jela tena.

Kumbuka jela ni jela hakuna starehe yeyote ile.
Ila kwetu africa jela ni sehemu ya kudhalilisha,kutesa,kuwageuza watu jinsia.dume kugeuzwa mke ,,

Inashangaza sana hata haki yako ya msingi pia hupati,,
na unaweza kuliwa kiboga kisa maji ya kuoga? Au uliwe kiboga kisa simu? Au uliwe kiboga kisa sigara? Uliwe kiboga kisa sabuni?
Kumnyima mfungwa chakula kizuri ndy jela?

Waafrica tukitaka democracy na usawa kwanza tuboreshe jela zetu.
Maana kuna watu wanajiona kule hawawezi kufika hata iweje..
Hyo ndy sababu ya kuweka mateso .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu mjadala unatakiwa kuwa wa kitaifa huwa Mara kadhaa napita gereza la Butimba hakika mambo ambayo huwa naona inasikitisha Sana sio kwa Askari wala wafungwa wote maisha yao ni Kama sawa tofauti ni majina tu
 
Jela za wenzetu ulaya ni fursa kibiashara.
Jela zimebinafsishwa.
Jela zinaendeshwa na watu binafsi,,
Kuna maduka ya nguo,viatu ,sigara,soda,vyakula nk.

Ukihitaji unafanya oda yako,,unaletewa selo yako ndani ya siku 5.

Hyo yote ni kudhibiti hali ya kufanya jela kuwa sehemu ya mateso.

Siku unayohukumiwa hutomuona tena police wala bwana jela wala nyapara.

Unakutana na security wa jela tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kubadilisha hali katika magereza bila kufanya magereza yaendeshwe kwa biashara.

Ukishaanza kufanya magereza yaendeshwe kwa biashara, na ikiwa magereza yanayojaa wafungwa yanatengeneza biashara nzuri zaidi kuliko magereza matupu, hapo ndipo mwanzo wa kesi za kubambikiwa kuongezeka, ili magereza yajae, ili biashara zipate faida zaidi.

Huoni mantiki hii rahisi tu?
Kubambikiwaje?

Nadhani haujaielewa mantiki ya mtoa mada.

Yeye kasema na kulenga baadhi ya huduma za wafungwa ndani ya jela kubinafsishwa kibiashara.

Kwa mfano chakula na malazi pamoja na kujengwa jela zenye hadhi.

Huduma zilizopo sasa hivi ziwepo kwa yeyote, lakini kwa wenye uwezo wa kugharamia huduma za malazi na chakula pamoja na kufungwa jela za pesa, waruhusiwe.

Sasa hapo kubambikiwa kutakujaje?
 
Nakwambia hivi, ukizidisha huduma zinazoendeshwa kibiashara na watu binafsi kuhudumia Magereza, faida ya kutoa huduma hizo itaendana na wingi wa wafungwa.

Magereza yatakavyozidisha wafungwa ndivyo biashara zitakavyopata faida zaidi.

Na kwa jinsi nchi yetu isivyo na guardrails za kuhakiki nani anafungwa na kama kafungwa kwa haki, hususan kwa watu masikini, mfumo huu utapelekea watu kufungwa kwa kesi mbuzi za kubambikiwa ili mradi magereza yajae zaidi, na biashara zipate faida kwa magereza kujaa hivyo.

Marekani huu mfumo upo sana. Nimeweka link ya wiki ya "prison industrial complex" hapo juu.

Kabla ya kuichukua hii mifumo, tuangalie kwa wenzetu walioqnza kuitumia awali kumetokea matatizo gani.
 
Back
Top Bottom