kimsingi watu masikini hawawezi kulipia huduma za jela private, so kubambikiwa sio inshu nzito ikiwa tu mifumo itawekewa uwazi na sheria za kudhibiti ikiwa ni pamoja na adhabu kwa wabambikaji,police husika na hakimu.
Umeelewa point yangu iko wapi?
Nakwambia hivi, ukishaweka faida inayotokana na jela kujaa watu, kwa jinsi nchi yetu isivyo na mifumo ya kuhakiki kesi, idadi ya watu wanaobambikiwa kesi itazidishwa makusudi ili watu walio jela wazidi, halafu wafanyabiashara wanaofanya biashara hizi wapate faida zaidi.
Mimi sisemi haya kwa kukariri tu, nimeyaona Marekani. Kwa watu hao hao masikini ambao unasema hawawezi kulipia huduma za private jela, wamewekwa katika mfumo ambao ama wao watalipia, ama ndugu zao walio nje itawabidi walipie.
Mtu akishakuwa na kesi kubwa atachangisha familia, atauza kiwanja cha urithi, atafanya lolote ili apate huduma fulani kama za mawasiliano ili kuonesha hana hatia.
Na hapa ndipo watakapowapata watu, by the time umeonesha huna hatia, ushatumia hela nyingi sana kwenye hizo huduma.
Nimeweka link ya "prison industrial complex" hapo juu, imeelezea matatizo haya kwa nchi ambayo ishafanya mfumo huu, Marekani.
Nimeona watu wanakamatwa kwa kesi mbuzi kabisa wanawekwa jela Marekani, halafu mfumo wa kibiashara wa jela unawapiga kuanzia kuongea na simu na ndugu zao walio nje kwa bei ya ajabu sana, mpaka chakula.
Mfumo wa haki unaendeshwa na kanuni moja kubwa, haki sawa kwa wote.
Ukishaanza kuweka madaraja katika kutoa haki, hawa watakaa jela yenye huduma hizi bora kwa sababu wana hela, na hawa wataoza huku kwa sababu hawana hela, hapo utakuwa umevunja msingi wa haki sawa kwa wote.
Kama kuna haja ya kuboresha hali magerezani, tuboreshe tu kwa fedha za walipa kodi watu wote wapate huduma sawa.
Ukishaanza kuweka faida ya kibiashara kwenye mfumo wa magereza, unatengeneza incentive za watu wasio hatia kufungwa ili faida ya wawekezaji waliowekeza kwenye mifumo ya magereza iongezeke.
Ukitaka kuona mifano hai ya ubaya wa mifumo ya magereza na huduma zake kubinafishwa, angalia mifumo ya magereza ya Marekani.