Serikali isitishe kulipa mishahara watumishi walioamua kurudi tena masomoni ni upotevu mkubwa wa pesa tena wengine wanahama fani kabisa.

Kumbuka mitaala ya vyuo hupitwa na wakati hivyo kuna haja ya waajiriwa kujiendeleza na kuongeza ujuzi n.k.
Kwa taarifa yako kwa mfumo wa serikali hii ukiacha kazi mfumo haukukubali ukiajiriwa upya.
Mwisho taasisi za serikali zinahitaji wabobevu kwenye fani mbalimbali lazima waruhusu waajiriwa kujiendeleza na iwapo unabadili fani yakupasa uache kazi ama uombe likizo bila malipo.
 
Unawivu wa kikonyo sana. Unashindwa kuwalalamikia wabunge na mawaziri wanaojilipa mamilioni bila lolote la maana? We una shida ya akili, kwanza r na l bado mtihani. Takataka.
 
Punguza roho ya kwa nn

kwa kifupi zipo likizo mbalimbali na zote mwajiriwa anapaswa kulipwa kasoro likizo isiyo na malipo
khs kwenda kusoma kwa mfanyakazi ni haki ya msingi na mwajiri anapaswa kugharamia
 
Hivi unajua background za watu wewe,watumishi.wengi ni zao la vijijini,walikuwa na limited opportunity lakini wakakomaa,by the way,hizo ni haki kwa mfanyakazi kujiendeleza sababu hata akipanda kwenda kwingineko na.wewe bumunda utaingia hapo,na sio wote wanafanikiwa kujiendeleza wengine wanakosa kila kitu.
 
U

Useless mind
 
Ona huyu!!
 
Ni kweli watumishi wote wakienda masomoni wanarudi na uwezo uleule? Mfano, nesi kaamua kujiendeleza na kuwa Dokta kama inawezekana, anaweza kuwa anafanana na nesi kiuwezo?

Pia, mtumishi huyu ana familia na watoto, hivyo ukisitisha mshahara, je ataishije?

Pia, mtumishi akibadilisha fani, akimaliza masomo akaenda sekta nyingine ya serikali kuna ubaya gani wakati anaendelea kuwahudumia Watanzania wale wale, ile nafasi iliyoachwa wazi si wataziba ajira mpya, au?
 
Fikiria mtoa mada angekuwa kwenye nafasi za juu za maamuzi huko serikalini. Huyu kiumbe ana roho mbaya sana ya kwa nini? Duu! duniani kuna baadhi ya viumbe ni vya ajabu sana ambavyo vimejivika jina la binadamu.
 
Roho ya kichawi&umaskini hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…