Serikali isitishe kulipa mishahara watumishi walioamua kurudi tena masomoni ni upotevu mkubwa wa pesa tena wengine wanahama fani kabisa.

Kwani kuna shido?
Mtu kazi akirudi kazi anafanya na hutaki alipwe na hela sio yako.
Malipo ya wafanyakazi wa serikalini hayareflect ugumu wa maisha na gharama ambazo zinapanda kila siku.
Unadhani hiyo hela anayopewa kwenda kusoma kwa njia ya mshahara anaenda kulewea?
Wengine wana familia wana ndugu wanawategemea na hiyo hiyo isiyotosha ndio agawie mpaka na bibi/babu kama wapo.Na unaona kama ni kuuuubwa.
At least mtu akipewa support ya kwenda kusoma inakuwa imembusti maana mazingira yenyewe ya kufanya kazi yana changamoto zake malipo hayatoshi wakati waliopo juu wanajikatia mapande alafu waliopo uwanjani mbombo ngafu semina hakuna,bonus hakuna,overtime hakuna,on call zipo ila malipo hakuna.
Serikali inafanya kama kurudisha fadhila kuwapeleka watu kusoma maana kama hiyo isingekuwepo pia watu wengine wasingeingia kwenye mfumo kwa sababu ni advantage kubwa inayowasukuma watu kuomba kazi serikalini.
Na kwa nini taifa ling'ang'anie wasomi kwani wote wameandikiwa kufanya kazi Tz?
Mtu umefanya kazi umelipwa imetokea nafasi sehemu nzuri zaidi uache kwenda kisa uzalendo?
Wanaotaka wasomi hao wawe wazalendo waanze kwanza wao huko juu(Charity begins at home) kwa mfano wa matumizi mazuri kodi ya wananchi alafu ndio na sisi watoto wa kajamba nani tutajifunzia hapo otherwise kila mtu apambanie anapoona ni sahihi.
Mind you sio kila mwajiriwa wa serikali ana ndoto ya kufia kwenye mfumo wa serikali ,wengine wanataka career zao ziendelee wafungulie opportunities kwa wengine hata kusoma mbele na kufanya kazi mambele.unategemea huyo mtu atabaki asubirie malipo yako ya mfumo wakati kuna mashirika yanalipa vizuri zaidi kuliko gvt?
Je ni ndoto za TZ gvt kubakiza wasomi wake hapa wasitoboe anga?
Kama jibu ni ndio basi wahakikishe maslahi yao yanaangaliwa pia kwa sababu hata wakirudi kutoka shule hawalipwi hela kuuubwa kiasi hiko na majukumu yanazidi kuongezeka.
Furahieni hata wakitoka wanaachia nafasi wengine wanaingia sio kuona kama kodi za wananchi zinatumika vibaya.
Wanaozitumia vibaya wako kule juu huku chini hata makombo hawapati na bado mnataka kuwanyonga na shule wasipate sapoti.
Alafu akirudi kama akipandishwa daraja wale walio chini hakuna wanaoingia ajira mpya kabisa hata mmoja?
Hauoni kama nayo ni nafasi kwa wengine kuingia kwenye ajira mwingine akiwa amepandishwa daraja?.
Mfumo una shida na wanaoteseka ni walioko chini kabisa.
"Aliyeshiba hamjui mwenye njaa"
Mleta uzi naona umeshiba vibaya mno🀣

#Mfumoukonashida
 
Sijui ulikua una maana gani lakini unatakiwa kuelewa kua hakuna mtu anaeenda kusoma ili kujifurahisha. Mtu akiamua kwenda kusoma ujue kua hiyo elimu ni kwa faida yake na jamii inayomzunguka. Na sio lazima aitumie elimu hiyo kwenye taasisi aliyopo hata akirudi akaamua kujiajiri, kuajiriwa sekta binafsi ama kuhamia taasisi nyingine ya uma bado elimu yake ataitumia kuleta manufaa kwa jamii na finally kwa taifa pale pale alipo. Hua nashindwa kuelewa waajiri wengine wanagomea watu kuhamia taasisi nyingine ama kuwazuia watu kuhama baada ya kutoka masomoni hadi watumikie muda waliokua masomoni, sasa unajiuliza huyu mwajiriwa si anaenda taasisi nyingine na ataendelea kulitumikia taifa hili hili ila akiwa sehemu nyingine sasa shida iko wapi?! Hata akienda nje ya nchi bado kuna namna taifa litanufaika kupitia elimu yake kwasababu ni ngumu kuhama na ukoo mzima so it's obvious kwamba kuna ndugu zake watanufaika kupitia yeye and hence taifa litanufaika pia indirectly. Anyways niishie hapa kwa leo but inahitajika deep and big thinking ili uweze kuelewa vizuri hii dhana.
 
Kuna kitu hukielewi,
Kusoma kwa mtumishi ni manufaa kwa mwajiri wake.
Acha roho mbaya
 
Uongo, taasisi yetu mishahara kwa mwezi ni zaidi ya bilioni saba sasa jiulize kwa Tanzania nzima ni Tsh ngapi?
Ongea kwa facts mkuu bajeti ya mshahara serikalini ipo mitandaoni wizara ya fedha iliwasilisha haizidi 1 billion serikali kuu hapa sizungumzii mashirika ya umma kama tanesco mamlaka za maji nazungumzia serikalini kuuu mishahara kwa mwezi haizidi billion moja nipo tayari kurekebishwa kwa facts lakini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…