Serikali isiyotimiza wajibu wake wa Kikatiba tunaiwajibishaje? Hapo ni baada ya kuiba kura kama dhambi ya kuu ya kwanza

Serikali isiyotimiza wajibu wake wa Kikatiba tunaiwajibishaje? Hapo ni baada ya kuiba kura kama dhambi ya kuu ya kwanza

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Kila kinachofanywa na serikali yetu pendwa ni utekelezaji yakinifu wa ilani ya chama kilichopo madarakani.

Wananchi ndiyo wanaoiweka serikali madarakani kwa kuchagua chama kitakachoiendesha. Lakini haki hiyo imepokwa kikatiba kwa sababu Katiba ya sasa inaelezea uwezo na utaratibu wa wananchi kuiweka madarakani serikali kupitia ngazi mbalimbali za uchaguzi. Lakini eneo la kuwajibisha iwapo serikali haitotimiza wajibu wake kikamilifu halijaguswa na Katiba.

Tuna issues
Umeme wa uhakika
Maji safi na salama
Miundombinu
Kilimo
Afya
Bima ya Afya
Ufisadi
Elimu
Maliasili
Ardhi
Na Kadhalika

Hayo yote ni mfupa mgumu ulioshindikana na serikali ya CCM.

Tunaeezaje kuiwajibisha ama kuichukulia hatua serikali inayowatia hasara na simanzi wananchi wake? Chukulia kwamba dola inashirikiana na chama kukwapua ushindi wa chaguzi kuu mbalimbali

Tunafanyaje?
 
Back
Top Bottom