Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SERIKALI ITAENDELEA KUJENGA BARABARA KUU LA MUSOMA VIJIJINI KWA KIWANGO CHA LAMI: WAZIRI BASHUNGWA ASISITIZIA UAMUZI HUO WA SERIKALI
Jana, Jumanne, tarehe 10.10.2023, Waziri ya Ujenzi, Mhe Waziri Innocent Bashungwa alifanya ziara ya kikazi Musoma Vijijini kwa lengo la kuwatoa wasiwasi wananchi kuhusu ujenzi wa barabara yao kuu kwa kiwango cha lami.
Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera yenye urefu wa kilomita 92 ndiyo barabara kuu inayounganisha Vijiji 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini na Miji ya Musoma na Mwanza.
Ujenzi wa barabara hilo kwa kiwango cha lami unasuasua sana kwani ni kilomita tano (5) tu zilizokwishajengwa kwa kiwango cha lami. Ujenzi wa kilomita hizo tano (5) ulichukua miaka minne (4)
Barabara hili ndilo roho kuu ya uchumi na ustawi wa wananchi wa Musoma Vijijini, na liko kwenye Bajeti ya Mwaka huu (2023/2024).
Tafadhali msikilize Mhe Waziri Innocent Bashungwa kwenye CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumatano, 11.10.2023