Serikali itoe adhabu Kali, wanaume wanaoshika Maungo ya wanawake hadharani kwenye maeneo ya Umma kama Sokoni na Stendi

Serikali itoe adhabu Kali, wanaume wanaoshika Maungo ya wanawake hadharani kwenye maeneo ya Umma kama Sokoni na Stendi

Kuna siku nilikua shekilango pale na kidemu changu tumeongozana.

Mie nilikua mbele kama hatua 3 yeye demu alikua nyuma kidooogo(si unajua tena hawa viumbe kuharakisha ni mtihani)

Basi kuna jamaa wanne nikapishana nao, ile nageuka nyuma nikaona mmoja kamshika tako demu, mchumba akahamaki.

Hapo hapo nikapiga u turn 180 degree fastaa, mchizi keshaanza kujibishana shombo na demu.

Nilivyofika nikamshika demu nikamsogeza pembeni, halafu nikamwambia mchizi mbele ya jamaa zake ageuke na mie nimshike tako, akaanza kuleta za kuleta.

Nikarushaa moja ikampata katikati ya pua na mdomo, akapepesuka, chini, anainuka michuzi kama yote.

Demu kuona hivyo akajua kabisa nimeshaingia KUMANYOKO MODE. akasogea fasta ananiambia muache, muache, muache.

Jamaa kuinuka akaokota jiwe, akarusha, nikainama likaenda kumpiga bodaboda, kufikia hapo nikaona nimeshauza ugomvi kwa mtu sahihi haina haja ya kuendelea kumtembezea kichapo.

Kama mnavyojua bodaboda walivyo na ushirikiano, sekunde mbili washajazana wanashughulika na mtu wao, mie huyooo na mchumba tukaondoka.
Yaani Upumbavu tuu unawasumbua!
 
Nenda mahakamani utakuta zimejaa kesi tele za vijana kubaka watoto wadogo ambao hawajavunja hata ungo na wanaume kulawiti watoto wadogo.
shida sisi huwa hatutaki kinga huwa tunataka tiba. Tunataka tatizo litokee ndipo tulitatue. Hili jambo mzizi wake ni wanawake wenyewe na hata huyo aliyeshikwa maungo yake alikuwa amevaa dera huku maungo yake yakitingishika kwa madaha na hisia.
Sheria ni zote sote,tusiogope kusema ukweli kwa kivuli cha jinsia. Tuanze na wanawake
 
shida sisi huwa hatutaki kinga huwa tunataka tiba. Tunataka tatizo litokee ndipo tulitatue. Hili jambo mzizi wake ni wanawake wenyewe na hata huyo aliyeshikwa maungo yake alikuwa amevaa dera huku maungo yake yakitingishika kwa madaha na hisia.
Sheria ni zote sote,tusiogope kusema ukweli kwa kivuli cha jinsia. Tuanze na wanawake
Tunataka nchi ambayo hata mtu akitembea uchi kabisa kwa madaha haguswi na wanaume/vijana wahuni achilia mbali aliyevaa dera anatembea kwa kutingisha maungo yake kwa madaha.
 
Tunataka nchi ambayo watu watashughulika na maendeleo, kuzuia ufisadi, utawala wa sheria, uhuru na kufuata mambo yao yanayowahusu badala ya kushughulika zaidi na vimini vya wanawake na makalio yao yasiyowahusu.
You are wrong, tudiri kwanza na mmomonyonko wa maadili haswa kwa dada zetu.

Wewe unachomaanisha ni kuwa Kila mtu afanye anavyotaka, avae anavyotaka na aishi kwenye jamii Kama anavyotaka.

Social responsibility must be observed in all areas.
 
Tunataka nchi ambayo hata mtu akitembea uchi kabisa kwa madaha haguswi na wanaume/vijana wahuni achilia mbali aliyevaa dera anatembea kwa kutingisha maungo yake kwa madaha.
hiyo nchi kaitengeneze wewe mkuu na uiite jamhuri ya watu wa Yoda kisha uwaruhusu watu(wanawake) watembee uchi sisi watanzania hatutaki huu ufedhuli wako.
 
hiyo nchi kaitengeneze wewe mkuu na uiite jamhuri ya watu wa Yoda kisha uwaruhusu watu(wanawake) watembee uchi sisi watanzania hatutaki huu ufedhuli wako.
Mimi ni Mtanzania pia
 
You are wrong, tudiri kwanza na mmomonyonko wa maadili haswa kwa dada zetu.

Wewe unachomaanisha ni kuwa Kila mtu afanye anavyotaka, avae anavyotaka na aishi kwenye jamii Kama anavyotaka.

Social responsibility must be observed in all areas.
Maadili ni kitu cha kufikirika zaidi kichwani kwako tu na maadili yako sio sawa yawe na yangu ndio maana kila mtu anapaswa fishing kwa uhuru wake ilimradi hamuumizi mwingine. Wewe kama unaona ushungi, juba bauibui, magauni ya kuburuza ni kitu muhimu sana kwako na ndio maadili au sijui stara vaa ila usilazimishe wengine wawe kama wewe, waache wavae vimini vyao, suruali zao, vitop vyao n.k
 
Hii sio Iran au Afghanistan ambapo raia huru wanapangiwa aina za mavazi za kuvaa.
Stara ni utamaduni wa pwani pia ambao umeathiriwa zaidi na waarabu na dini yao.
Kwahiyo shida ni dini? Au watu wa pwani kuathiriwa na utamadun wa kiarabu? Kama hauvai stara kwasababu hiyo basi usiwashawishi wengine wanaopenda kuvaa stara; kuvaa stara haikufanyi kuwa muislam au kuwa mwarabu.
Na kuvaa vichupi hakukufanyi kuwa mzungu au msomi; ni mila na desturi za mwafrika tu; sijajua kama unavaa nguo za nusu uchi ukienda kwa wazazi wako waliokuzaa.
 
Mimi ni Mtanzania pia
ndio maana nimekwambia kuwa wale vijana na huyo mama ni wenye makosa,mleta mada alianza kumshambulia kijana pasipo kujua chanzo ni huyo mama
 
SERIKALI ITOE ADHABU KALI, WANAUME WANAOSHIKA MAUNGO YA WANAWAKE HADHARANI KWENYE MAENEO ya UMMA KAMA SOKONI NA STENDI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli!

Kwa ambao hamjazoea Lugha Kali. Niwasihi muishie hapahapa! Kwani nitaitumia ili kugusa hisia na mioyo iliyolala. So kama Una tatizo na lugha Kali, au unaadabu Sana, au unakiapo cha kutosoma, kusikiliza au kuona lugha Kali basi ishia hapahapa. Kuendelea kusoma haitahesabika hatia kwangu mwandishi!

Utajisikiaje Mamaako kaenda Sokoni labda ni Karume au Kariakoo alafu vijana wakawa wanamvutavuta na kumshikashika matako yake? Utajisikiaje wewe!

Utajisikiaje, mkeo yupo zake sokoni, vijana wapumbavu wanamvuta vuta na kumbonyezabonyeza nyama zake? Hivi utajisikiaje!

Utajisikiaje, Binti yako mzuri labda yupo likizo, umempa pesa akanunue mahitaji yake ya shule kwani likizo imeisha na wiki ijayo wanatakiwa wakaripoti. Anafika sokoni vijana wanamdandia dandia na kumtomasa tomasa kwenye maziwa yake. Na hakuna anayejali. Utajisikiaje?

Jana bhana! Nilikuwa maeneo ya Karume, nilienda kwa shughuli zangu.
Nikiwa natembea kutafuta kilichonipeleka. Ghafla mbele yangu namwona kijana mmoja anamshika Mwanamke aliyejaliwa umbo, lakini kavaa dera. Yule kijana akamshika matako Yule mama. Sasa Yule mwanamke akang'aka na kushtuka, yule kijana akisaidiana na vijana wengine wauzaji wa kupanga vitu kwenye meza na chini wakawa wanamshika mono. Nunua hapa!
Yule mwanamke alisimama si kwakupenda, hasira na kutokujua aliyemshika tako lake ndicho kilichomsimamisha. Hakuwa na mpango wa kusimama kununua wala kuangalia bidhaa za wale vijana.

Mwanamke akaanza kurusha maneno, wale vijana nao wakaanza kumshambulia na kumdhalilisha kwa Maneno.
Kumbe pembeni yake Yule mwanamke alikuwa na mtoto wake Kama wa darasa la Saba hivi.

Mimi nikapunguza mwendo, ili kuangalia muelekeo wa lile Sakata.
Kilichoniuma zaidi ni Yule mtoto wa kiume. Alikuwa ameumizwa Sana kumwona mama yake akidhalilishwa.

Kwanza aliona akishikwa Tako. Mimi ni Shahid.
Pili, alikuwa akisikia matusi ambayo Mamaake alikuwa akiambiwa na wale vijana. Matusi ya nguoni kabisa.

Jamani! Sisi wanaume tunaelewa jinsi Mama zetu wakihusishwa na mambo ya kikahaba tunavyoumia. Tunaumia kuona mama zetu wakivaa nguo za hovyohovyo na kufanya au kufanyiwa matendo ya kihuni.

Kweli hicho ndio kiliigusa zaidi.
Watu wengine walikuwa wakicheka tuu, wengine wakipuuza. Ni kama Jambo hilo limezoeleka maeneo ya masokoni na stendi.
Kushika shika wanawake mikono na maungo yao bila ridhaa yao.

Mimi nikamsogelea Yule kijana aliyemshika Yule mwanamke Tako. Nikamwambia kwa nini unawadhalilisha wanawake kwa kuwashika matako, si ukamshike mkeo au kama huna mke kamshike Mamaako!
Lengo lilikuwa kumpanikisha ili akose utulivu wa akili. Kabla hajajibu nikijua ameshajaa kisaikolojia kwenye Mfumo, kufumba na kufumbua nikamrukia na kichwa nikampiga kwenye pua yake.
Akadondoka chini.

Nilijua ataamka, piga teke la mbavu,kisha piga upande wa pembeni wa shingo. Yalikuwa mapigo matati ya haraka kabla sijashikwa na watu kuamulia.

Sasa vurugu ni kama imeanza. Mini ninamwili mdogomdogo, mwenye sura ya upole, macho ya hila, na huwezi dhania kama naweza kukupiga ukalazwa.
Basi wale vijana wakataka kuamsha fujo pale. Wakiungana na baadhi ya wafanyabiashara majirani.

Bahati nzuri kulikuwa pembeni wanauza mikanda, nikachukua mmoja. Dadeki! Nikauzungusha kama mara mbili kisha, nikasema; Kama mtu anahitaji afie hapahapa asogee! Sasa Ile sura ya upole haikuwepo tena. Ni kweli sikutaka kuwakadiria, najua sehemu kama zile kuumizwa hata kuuawa ni kugusa.

Hivyo ni Bora Niue mimi kuliko kuuawa. Wanasema, usalama Kwanza kisha Sheria baadaye.

Basi wanaume watu wazima wakaja kuamulia. Watu wakiwa wamejaa Sana. Wengine wakichungulia kwenye madirisha ya daladala zilizokuwa zinapita.

Yule kijana alikuwa amepasuka Mwamba wa pua yake.
Nilitamani nimuweke alama ambayo kila akiiona imkumbushe kuheshimu Wanawake, kuheshimu watu wengine. Lakini sikufanikiwa.

Serikali, fanyeni mpango muandae adhabu Kali za wazi, kukomesha huu upumbavu.

Yaani wanawake wasiwe huru kutembea masokoni kisa kero za wapuuzi wachache. Hiyo tabia ikomeshwe.

Watafutwe watu wa mfano ili Somo lieleweke!

Njia pendekezwa!

1. Atakayefanya tukio Hilo apewe adhabu ya kutandikwa viboko hadharani. Na kifungo cha miezi mitatu au faini ya million Moja.

Jinsi ya kudhibiti
1. Kila soko liwe na uongozi na kamati ya ulinzi na Sheria
2. Kila soko liwe na Sheria ya kulinda utu wa wateja.
3. Kila soko liwe na ofisi ndani ya ofisi iwe no kituo cha polisi au kamati ya ulinzi na usalama ya soko. Ambapo wateja na wanaokuja hapo sokoni pamoja na wauzaji masala yao hushughulikiwa kabla hayajafika juu.

4. Kamati ya soko, iandae na kusajili listi ya wafanyabiashara wote, kusajili mawinga wote ambao wanafanya kazi hapo.
Kila winga apewe utambulisho iwe wa namba au beji, au sare.

5. Ikiwa soko ni kubwa, soko linaweza kugawanywa kwa idadi ya watu waliomo au ukubwa wa eneo ili kuleta ufanisi na udhibiti.

6. Mawinga wanaweza kulipia ada ya soko kwa mwezi au mwaka.

7. Semina na mafunzo kwa watoa huduma kwenye masoko ikiwemo kutoa elimu ya haki za binadamu na kulinda utu wa wateja hasa watoto na wanawake zitolewe mara kwa mara.

8. Maeneo muhimu yafungwe Kamera
9. Kuondoa vipaza Sauti vinavyopiga kelele na kuleta usumbufu na uchafu wa mazingira.
Au iundwe ada au kodi ya vipaza sauti.
Mtu kama anataka vipaza sauti vitangaze biashara yake alipie kiasi Fulani kwa mwaka au mwezi.
Sio mtu apigie watu kelele, watu wateseke alafu kumbe ni bure kwa faida Yake wakati anaumiza na kusumbua wengine.

Kufikia hapo Sina la ziada!

Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Wanwake wenyewe ndo wanapenda
 
Nobody na hatuhitaji research katika hilo.
Ubongo wako ni kama wa mtoto wa miaka miwili tu,hujui hata unachokiongea,
Umebakia kuruka ruka tu kama Kuku aliyekatwa kichwa kisha akaachiwa ghafla.
 
Kwahiyo shida ni dini? Au watu wa pwani kuathiriwa na utamadun wa kiarabu? Kama hauvai stara kwasababu hiyo basi usiwashawishi wengine wanaopenda kuvaa stara; kuvaa stara haikufanyi kuwa muislam au kuwa mwarabu.
Na kuvaa vichupi hakukufanyi kuwa mzungu au msomi; ni mila na desturi za mwafrika tu; sijajua kama unavaa nguo za nusu uchi ukienda kwa wazazi wako waliokuzaa.
Shida ni kupangia watu(civilians) mavazi ya kuvaa kama wako gerezani.
 
Ni hoja nzuri, ila upande mwingine suala la uvaaji la dada na mama zetu ni tatizo. Wanavaa ili waonyeshe "kalio" zao.
Mtu umeficha "kalio" nani ataliona na akubonyeze.

Mkuu hoja ya uvaaji hovyo hakuna atakayeiunga Mkono.
Unaweza enda Kariakoo au Karume hata Leo. Utajionea jinsi wanawake wanavyopata tabu bila kujali wamevaa Kwa heshima au kihuni.
 
Uzi mrefu sijausoma najibu kulingana na kichwa cha uzi.

Sheria zipo za kushughulikia jambo kama hili linapotokea. Nenda karipoti kama umeona tukio kama hilo
Kama sheria ipo ni jambo zuri.
Ndio nimesharipoti Ili lifanyiwe kazi na kuchukuliwa kidete.
 
Mkuu hoja ya uvaaji hovyo hakuna atakayeiunga Mkono.
Unaweza enda Kariakoo au Karume hata Leo. Utajionea jinsi wanawake wanavyopata tabu bila kujali wamevaa Kwa heshima au kihuni.
Wanawake wote wanaotembea barabarani wamevaa kiheshima, labda ungesema bila kujali wamevaa kisabato, kiisilamu au vinginevyo.
 
Tunataka nchi ambayo hata mtu akitembea uchi kabisa kwa madaha haguswi na wanaume/vijana wahuni achilia mbali aliyevaa dera anatembea kwa kutingisha maungo yake kwa madaha.

Hapana. Kutembea uchi ni kuvunjia wengine haki zao
 
Back
Top Bottom