Serikali itoe adhabu Kali, wanaume wanaoshika Maungo ya wanawake hadharani kwenye maeneo ya Umma kama Sokoni na Stendi

Serikali itoe adhabu Kali, wanaume wanaoshika Maungo ya wanawake hadharani kwenye maeneo ya Umma kama Sokoni na Stendi

Nimeweka hoja stara sio lazima kuvaa majuba, nikab au hijab au kujifunika gubigubi....kuna nguo nzuri tu za stara ukivaa Bi. Yoda utapendeza na kubadili mwenekano wako! Wala haiitaji degree au kuhamia Afghanistan au Iran.
Nowdays; mtu anavaa kajinguo kakipochi kanajichoraa haya sio maadili. Nadikir kuna haja wizara kama imeweka zuio la kuvaa stara katika maeneo ya ofisi za umma kuna haja kuweka zuio pia kuvaa maeneo ya masoko makuu; nguo hizo vaa beach
Mkuu,huyo Binti uliyemquote amesha hamishia hii mada kwenye chuki ya udini,nadhani hujamjua tu,huyo kila mada hua anaihamishia kwenye chuki ya udini.
 
Ni hoja nzuri, ila upande mwingine suala la uvaaji la dada na mama zetu ni tatizo. Wanavaa ili waonyeshe "kalio" zao.
Mtu umeficha "kalio" nani ataliona na akubonyeze.
 
mleta mada amesema huyo mama alivaa dera. naimani dera ni vazi la heshima pia ila bado akasumbuliwa. kwa mdada ukiweza kukwepa haya maeneo ya masoko ukatuma mtu akusaidie kununua ni vema zaidi. Kama inakulazimu basi heri kwenda na mume au ndugu wa kiume hutapata hiyo bugudha maana wale watu hawajali hata kama umevaa gauni ndefu ya stara.
 
Shida ipo polisi na mahakamani utakanyagia mpaka miguu ipinde na kila kitu chako kisimame kama sio kuharibika. Masuala ya kesi katika nchi zetu hizi ni kukaribisha umaskini tu
 
Nimeweka hoja stara sio lazima kuvaa majuba, nikab au hijab au kujifunika gubigubi....kuna nguo nzuri tu za stara ukivaa Bi. Yoda utapendeza na kubadili mwenekano wako! Wala haiitaji degree au kuhamia Afghanistan au Iran.
Nowdays; mtu anavaa kajinguo kakipochi kanajichoraa haya sio maadili. Nadikir kuna haja wizara kama imeweka zuio la kuvaa stara katika maeneo ya ofisi za umma kuna haja kuweka zuio pia kuvaa maeneo ya masoko makuu; nguo hizo vaa beach
Hii sio Iran au Afghanistan ambapo raia huru wanapangiwa aina za mavazi za kuvaa.
Stara ni utamaduni wa pwani pia ambao umeathiriwa zaidi na waarabu na dini yao.
 
Mkuu,huyo Binti uliyemquote amesha hamishia hii mada kwenye chuki ya udini,nadhani hujamjua tu,huyo kila mada hua anaihamishia kwenye chuki ya udini.
Nchi za kidini tu ndio hulazimisha wanawake kujifunika gubigubi eti ili wanaume wenye tamaa wasiwatamani. Hakuna nchi secular(isiyo ya kidini) inayolazimisha wanawake wajifunike mwili mzima au wasivae mavazi ya kubana.
 
Nchi za kidini tu ndio hulazimisha wanawake kujifunika gubigubi eti ili wanaume wenye tamaa wasiwatamani. Hakuna nchi secular(isiyo ya kidini) inayolazimisha wanawake wajifunike mwili mzima au wasivae mavazi ya kubana.
Kwanini hukutuma picha za masister waliovaa kiheshima ila ukatuma picha za Wanawake wa kiislamu?
Binti Islamophobia inakutesa sana,hizo nguvu za chuki ya udini zitumie kupambana na maisha yako ili usije ukawapa watu wengine kazi ya kukulea uzeeni mwako,
Time is waiting for no one.
 
Kwanini hukutuma picha za masister waliovaa kiheshima ila ukatuma picha za Wanawake wa kiislamu?
Binti Islamophobia inakutesa sana,hizo nguvu za chuki ya udini zitumie kupambana na maisha yako ili usije ukawapa watu wengine kazi ya kukulea uzeeni mwako,
Time is waiting for no one.
Masista hawalazimishwi kuwa masista, wamechagua wenyewe kuwa masista na kuvaa wanavyovyaa.
 
Uzi mrefu bila maana.

Kama ndugu yako anajistri hawezi kufikia huko.

Jikite katika kuwaelimisha ndugu zako hao wote uliwataja.
 
Uzi mrefu bila maana.

Kama ndugu yako anajistri hawezi kufikia huko.

Jikite katika kuwaelimisha ndugu zako hao wote uliwataja.
Tunataka nchi ambayo watu watashughulika na maendeleo, kuzuia ufisadi, utawala wa sheria, uhuru na kufuata mambo yao yanayowahusu badala ya kushughulika zaidi na vimini vya wanawake na makalio yao yasiyowahusu.
 
Masista hawalazimishwi kuwa masista, wamechagua wenyewe kuwa masista na kuvaa wanavyovyaa.
Una akili ndogo sana wewe Dada,hujui hata unachokitetea,
Ukisha ingia kwenye usister ni lazima uvae mavazi ya stara,mbona unakua na akili nzito hivyo?
 
Una akili ndogo sana wewe Dada,hujui hata unachokitetea,
Ukisha ingia kwenye usister ni lazima uvae mavazi ya stara,mbona unakua na akili nzito hivyo?
Hatuhitaji mwanamke akizaliwa au akiingia Tanzania alazimishwe kujifunika gubigubi.
 
cc Dkt. Gwajima D inasikitisha na kuhuzunisha sana swala hili linatakiwa lipigiwe kelele na jamii yote,wanawake waheshimiwe na walindwe kwa wivu mkubwa sana,hata hivyo ninavyojua kwa uelewa wangu mdogo kufanya hivyo kisheria ni shambulio la aibu na adhabu yake siyo kama ulivyosema kwamba watandikwe viboko bali adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela,pumbafu kabisa hao wanaodhalilisha wadada,watoto na wamama...hongera kwa kuchukua hatua Mtibeli ingawa pale kuna watu wa vyombo vya usalama ilitakiwa pia uwaripoti kwa hatua zaidi
Shida uvaaji wao unawavutia vijana wawafanyie vitu vya hovyo. Tuanze na wanawake wenyewe kwanza.
 
Shida uvaaji wao unawavutia vijana wawafanyie vitu vya hovyo. Tuanze na wanawake wenyewe kwanza.
Nenda mahakamani utakuta zimejaa kesi tele za vijana kubaka watoto wadogo ambao hawajavunja hata ungo na wanaume kulawiti watoto wadogo.
 
SERIKALI ITOE ADHABU KALI, WANAUME WANAOSHIKA MAUNGO YA WANAWAKE HADHARANI KWENYE MAENEO ya UMMA KAMA SOKONI NA STENDI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli!

Kwa ambao hamjazoea Lugha Kali. Niwasihi muishie hapahapa! Kwani nitaitumia ili kugusa hisia na mioyo iliyolala. So kama Una tatizo na lugha Kali, au unaadabu Sana, au unakiapo cha kutosoma, kusikiliza au kuona lugha Kali basi ishia hapahapa. Kuendelea kusoma haitahesabika hatia kwangu mwandishi!

Utajisikiaje Mamaako kaenda Sokoni labda ni Karume au Kariakoo alafu vijana wakawa wanamvutavuta na kumshikashika matako yake? Utajisikiaje wewe!

Utajisikiaje, mkeo yupo zake sokoni, vijana wapumbavu wanamvuta vuta na kumbonyezabonyeza nyama zake? Hivi utajisikiaje!

Utajisikiaje, Binti yako mzuri labda yupo likizo, umempa pesa akanunue mahitaji yake ya shule kwani likizo imeisha na wiki ijayo wanatakiwa wakaripoti. Anafika sokoni vijana wanamdandia dandia na kumtomasa tomasa kwenye maziwa yake. Na hakuna anayejali. Utajisikiaje?

Jana bhana! Nilikuwa maeneo ya Karume, nilienda kwa shughuli zangu.
Nikiwa natembea kutafuta kilichonipeleka. Ghafla mbele yangu namwona kijana mmoja anamshika Mwanamke aliyejaliwa umbo, lakini kavaa dera. Yule kijana akamshika matako Yule mama. Sasa Yule mwanamke akang'aka na kushtuka, yule kijana akisaidiana na vijana wengine wauzaji wa kupanga vitu kwenye meza na chini wakawa wanamshika mono. Nunua hapa!
Yule mwanamke alisimama si kwakupenda, hasira na kutokujua aliyemshika tako lake ndicho kilichomsimamisha. Hakuwa na mpango wa kusimama kununua wala kuangalia bidhaa za wale vijana.

Mwanamke akaanza kurusha maneno, wale vijana nao wakaanza kumshambulia na kumdhalilisha kwa Maneno.
Kumbe pembeni yake Yule mwanamke alikuwa na mtoto wake Kama wa darasa la Saba hivi.

Mimi nikapunguza mwendo, ili kuangalia muelekeo wa lile Sakata.
Kilichoniuma zaidi ni Yule mtoto wa kiume. Alikuwa ameumizwa Sana kumwona mama yake akidhalilishwa.

Kwanza aliona akishikwa Tako. Mimi ni Shahid.
Pili, alikuwa akisikia matusi ambayo Mamaake alikuwa akiambiwa na wale vijana. Matusi ya nguoni kabisa.

Jamani! Sisi wanaume tunaelewa jinsi Mama zetu wakihusishwa na mambo ya kikahaba tunavyoumia. Tunaumia kuona mama zetu wakivaa nguo za hovyohovyo na kufanya au kufanyiwa matendo ya kihuni.

Kweli hicho ndio kiliigusa zaidi.
Watu wengine walikuwa wakicheka tuu, wengine wakipuuza. Ni kama Jambo hilo limezoeleka maeneo ya masokoni na stendi.
Kushika shika wanawake mikono na maungo yao bila ridhaa yao.

Mimi nikamsogelea Yule kijana aliyemshika Yule mwanamke Tako. Nikamwambia kwa nini unawadhalilisha wanawake kwa kuwashika matako, si ukamshike mkeo au kama huna mke kamshike Mamaako!
Lengo lilikuwa kumpanikisha ili akose utulivu wa akili. Kabla hajajibu nikijua ameshajaa kisaikolojia kwenye Mfumo, kufumba na kufumbua nikamrukia na kichwa nikampiga kwenye pua yake.
Akadondoka chini.

Nilijua ataamka, piga teke la mbavu,kisha piga upande wa pembeni wa shingo. Yalikuwa mapigo matati ya haraka kabla sijashikwa na watu kuamulia.

Sasa vurugu ni kama imeanza. Mini ninamwili mdogomdogo, mwenye sura ya upole, macho ya hila, na huwezi dhania kama naweza kukupiga ukalazwa.
Basi wale vijana wakataka kuamsha fujo pale. Wakiungana na baadhi ya wafanyabiashara majirani.

Bahati nzuri kulikuwa pembeni wanauza mikanda, nikachukua mmoja. Dadeki! Nikauzungusha kama mara mbili kisha, nikasema; Kama mtu anahitaji afie hapahapa asogee! Sasa Ile sura ya upole haikuwepo tena. Ni kweli sikutaka kuwakadiria, najua sehemu kama zile kuumizwa hata kuuawa ni kugusa.

Hivyo ni Bora Niue mimi kuliko kuuawa. Wanasema, usalama Kwanza kisha Sheria baadaye.

Basi wanaume watu wazima wakaja kuamulia. Watu wakiwa wamejaa Sana. Wengine wakichungulia kwenye madirisha ya daladala zilizokuwa zinapita.

Yule kijana alikuwa amepasuka Mwamba wa pua yake.
Nilitamani nimuweke alama ambayo kila akiiona imkumbushe kuheshimu Wanawake, kuheshimu watu wengine. Lakini sikufanikiwa.

Serikali, fanyeni mpango muandae adhabu Kali za wazi, kukomesha huu upumbavu.

Yaani wanawake wasiwe huru kutembea masokoni kisa kero za wapuuzi wachache. Hiyo tabia ikomeshwe.

Watafutwe watu wa mfano ili Somo lieleweke!

Njia pendekezwa!

1. Atakayefanya tukio Hilo apewe adhabu ya kutandikwa viboko hadharani. Na kifungo cha miezi mitatu au faini ya million Moja.

Jinsi ya kudhibiti
1. Kila soko liwe na uongozi na kamati ya ulinzi na Sheria
2. Kila soko liwe na Sheria ya kulinda utu wa wateja.
3. Kila soko liwe na ofisi ndani ya ofisi iwe no kituo cha polisi au kamati ya ulinzi na usalama ya soko. Ambapo wateja na wanaokuja hapo sokoni pamoja na wauzaji masala yao hushughulikiwa kabla hayajafika juu.

4. Kamati ya soko, iandae na kusajili listi ya wafanyabiashara wote, kusajili mawinga wote ambao wanafanya kazi hapo.
Kila winga apewe utambulisho iwe wa namba au beji, au sare.

5. Ikiwa soko ni kubwa, soko linaweza kugawanywa kwa idadi ya watu waliomo au ukubwa wa eneo ili kuleta ufanisi na udhibiti.

6. Mawinga wanaweza kulipia ada ya soko kwa mwezi au mwaka.

7. Semina na mafunzo kwa watoa huduma kwenye masoko ikiwemo kutoa elimu ya haki za binadamu na kulinda utu wa wateja hasa watoto na wanawake zitolewe mara kwa mara.

8. Maeneo muhimu yafungwe Kamera
9. Kuondoa vipaza Sauti vinavyopiga kelele na kuleta usumbufu na uchafu wa mazingira.
Au iundwe ada au kodi ya vipaza sauti.
Mtu kama anataka vipaza sauti vitangaze biashara yake alipie kiasi Fulani kwa mwaka au mwezi.
Sio mtu apigie watu kelele, watu wateseke alafu kumbe ni bure kwa faida Yake wakati anaumiza na kusumbua wengine.

Kufikia hapo Sina la ziada!

Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Bado sio maneno makali,ni washamba,wapumbavu,wachafu na wapenda sifa,ni watu wasiojielewa na waliokosa mabadiliko kabisa Tena wa kupigwa hadharani!
 
Robert Heriel Mtibeli hatua ulizochukua jana ni kinyume cha utaratibu na sheria za tanzania,ulijichukulia sheria mkononi-ulitakiwa uwe sero mpaka muda huu! Na badala ya kupunguza tatizo basi wewe umeongeza tatizo kati ya jinsia mbili hizi hapa tanzania,ulionyesha upendeleo wa wazi kwa jinsia ya kike,huyo uliyempiga ni mmoja je waliobaki utawadhibiti vipi? Ungeanza na elimu badala ya kipigo.
 
Back
Top Bottom