LGE2024 Serikali itoe elimu kuelimisha wananchi umuhimu wa kujiandikisha, huo utaratibu wa kuwafata majumbani kuwaandisha haulisaidii taifa

LGE2024 Serikali itoe elimu kuelimisha wananchi umuhimu wa kujiandikisha, huo utaratibu wa kuwafata majumbani kuwaandisha haulisaidii taifa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
ulifuatwa na watu wa vyama vya siasa au maafisa yandikishaji au matapeli?

ulivyokwenda kituoni kujiandikisha, wale maafisa ulowakuta, walikua ni wale waliokufuata nyumbani kwako au siyo? :NoGodNo:
Aliye kuja ni dada aliye niandikisha ila hakujua ninapo ishi sasa walivyo gonga geti akatoka kijana wangu akaja kuniita ndani wakati natoka ndiyo namuona yule dada, alipo niona akanisalimia akawambia alio kuja nao huyu mzee alisha kuja na mke wake, maana alikunikumbuka wakati ananiandikisha nika weka utani kidogo naona alinikalili.
 
ulifuatwa na watu wa vyama vya siasa au maafisa yandikishaji au matapeli?

ulivyokwenda kituoni kujiandikisha, wale maafisa ulowakuta, walikua ni wale waliokufuata nyumbani kwako au siyo? :NoGodNo:
Zama za kuchezea kura za wanaume zimeisha. Hakuna mtu ataendelea kushiriki chaguzi za kishenzi ili kuhalalisha chama cha majizi kukaa madarakani. Ni aidha machafuko au mapinduzi ya kijeshi ili heshima ya box la kura irejee.
 
kwahiyo umefuatwa na maafisa waandikishaji hadi nyumbani kwako kama kipindi kile cha sensa vile, right?:pedroP:

kwamba wewe ni muhimu sana au niaje kwa mfano tuanzie hapo, isije ikawa unapotosha gentleman? :NoGodNo:
Msiwe mnabisha tu kila kitu Ili muonekane ni CCM Bora....hali huku chini ni mbaya sana basi tu mmeamua kutotumia akili.
 
Wanaopita majumbani ni watu wa CCM. wapinzani wako bize mitandaoni, alafu wakila za uso waanze kusema wameibiwa kura. Hawako serious kabisa.
Hakuna zoezi serious hapo, ccm kushinda kihalali imeshashindikana. Watu hawwgomeia kama wajinga boss.
 
Sio kweli kabisa. 2019 na 2020 ndio miaka pekee ambayo uchaguzi uliharibika. Mwaka huu na mwakani mambo yatakuwa fair. Ndio maana CCM wanafanya kazi ya ziada.
Acha upotoshaji, miaka yote hasa kuanzia 2010 chaguzi zetu zimekuwa zikitoa matokeo ya kuchezewa, ila 2019-20 ndio ushenzi ulifanywa kwa uwazi zaidi. Umesahau 2015 uchaguzi Znz ulifutwa kisa CUF walishinda? Ccm Wanafanya kazi ipi ya ziada wakati tumeshawachoka? Kwanini hamsomi alama za nyakati kuwa kizazi hiki kimeshawachoka, ni lazima mtolewe kwa machafuko?
 
Subiri uje uone takwimu za mwisho na idadi ya waliojiandikisha
Hiyo kuweka idadi ya kupika haiondoi ukweli kuwa watu wamewachoka. Kama huamini waambie hao viongozi wa mchongo waitishe mkutano hapo mtaani kama watu watajitokeza wa kuridhisha.
 
yani unifuate nyumbani kujiandikisha,wakati ni hiari,je wakati wa kupiga kura napo mtanifuata nyumbani! jamani,kama ni hiari ya mtu kufanya jambo hili tusifanye kuwa lazma,hata wakiishia wawili waliojiandkisha kumchagua mwenyekiti wa mtaa wao basi hao hao wanatosha. tulazmishane kwenye mambo ya lazma si ya uchaguzi.
 
Msiwe mnabisha tu kila kitu Ili muonekane ni CCM Bora....hali huku chini ni mbaya sana basi tu mmeamua kutotumia akili.
CCM maeneo mengi tayari wamesha jiandikisha kwa wingi sana kwa sehemu kubwa,

wanasubiri tu,
kuchukua kuweka waaaa🐒
 
Zama za kuchezea kura za wanaume zimeisha. Hakuna mtu ataendelea kushiriki chaguzi za kishenzi ili kuhalalisha chama cha majizi kukaa madarakani. Ni aidha machafuko au mapinduzi ya kijeshi ili heshima ya box la kura irejee.
wewe huruhusiwi kujiandikisha wala kupigakura kwasabb za kiutimamu...

so,
kaa pembeni na utulie, usimbwele mbwele hapa 🐒
 
Hakuna haja ya kujiandikisha na kupiga Kura ndani ya taifa hili,maana kufanya hivyo ni kuunga mkono upumbavu ambao hutokea kipindi cha uchaguzi.
 
Siasa za ushindani na kidemokrasia zinapokosa msisimko madhara yake ni wananchi kupata kiu na mawazo yakujitafutia viongozi wanaowataka kwa njia nyingine isiyo rasmi.Mifano iko mingi dunia kwasababu ata mapinduzi mbalimbali chanzo chake kikubwa ni kudharauliwa kwa box la kura.Kuna ambao wanaona sawa kwasababu wananufaika ila hawajui icho wanachonufaika nacho leo kinaweza kuharibika ndani ya siku moja endapo sanduku la kura litaendelea kudharauliwa.
 
Back
Top Bottom