Serikali itunge sheria kuhusu uzazi wa mpango angalau watoto wawili kila familia maana kasi ya uzazi Tanzania inatisha

Serikali itunge sheria kuhusu uzazi wa mpango angalau watoto wawili kila familia maana kasi ya uzazi Tanzania inatisha

Babe la mji

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2019
Posts
983
Reaction score
2,058
Ndugu zangu kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha Sana. Juzi nilikua wilayani Ukerewe nimeshangaa vijiji vya hii wilaya Yaani Kila Kijiji kina shule za msingi mbilimbili lakini bado hazitoshi

Fikiria Kijiji kina shule mbili za msingi lakini bado shule zimezidiwa na wanafunzi. Hizi shule unakuta shule Ina hadi watoto mia Saba hadi mia tisa.

Nimeitolea Ukerewe kama mfano lakini najua hata sehemu nyinginezo za nchi yetu hali iko hivyo. Kama hali hii isipodhibitiwa na wizara ya afya basi huko mbeleni kazi ya serikali itakua kujenga madarasa na hospitals badala ya kufanya miradi ya maendeleo.

Australia nchi yenye maendeleo makubwa Ina watu ambao wahazidi million Saba Sasa ukija Tanzania Hali inatisha. Uzazi wa mpango utungiwe sheria ili tuweze kuwaletea Wananchi wetu maendeleo maana kasi ya uzazi ni kubwa kuliko ukuaji wa uchumi.

Asanteni.
 
Kuna mtoto wa jirani anakuja kuchukua ada kwako?

Vipi serikali yenu ya mtaa imepitisha sheria ya mtu mmoja kuruhusiwa kula nyumba yoyote?

Kwani wanaozaa watoto wengi wamelalamika kuwa wanaonewa na Serikali?

Nchi ina rasilimali lukuki, hata Watanzania tungekuwa bilioni moja kama serikali ingeweza kusimamia rasilimali zetu ziwe productive kila familia ingekuwa na maisha bora.

Serikali isikwepe jukumu lake, serikali ndio mmiliki wa kila kitu Tanzania ikiwemo ardhi. Hata leo chini ya kitanda chako ikigundulika dhahabu utatimuliwa kama mbwa ukikataa kutimuliwa kistaarabu.
 
Ndugu zangu kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha Sana.Juzi nilikua wilayani Ukerewe nimeshangaa vijiji vya hii wilaya Yani Kila Kijiji kina shule za msingi mbilimbili lakini bado hazitoshi .Fikilia Kijiji kina shule mbili za msingi lakini bado shule zimezidiwa na wanafunzi.Hizi shule unakuta shule Ina hadi watoto mia Saba hadi mia tisa.

Nimeitolea Ukerewe kama mfano lakini najua hata sehemu nyinginezo za nchi yetu hali iko hivo .Kama Hali hii isipodhibitiwa na wizara ya afya basi huko mbeleni kazi ya serikali itakua kujenga madarasa na hospitals badala ya kufanya miladi ya maendeleo .
Australia nchi yenye maendeleo makubwa Ina watu ambao wahazidi million Saba Sasa ukija Tanzania Hali inatisha.Uzazi wa mpango utungiwe sheria ili tuweze kuwaletea Wananchi wetu maendeleo maana kasi ya uzazi ni kubwa kuliko ukuaji wa uchumi .
Asanteni.
Nasimama na mwenda zake, hahahahaaa Wewe ni mtoto wa 9, unazaa watoto 2, mama yako angezaa 2 ungeiona Dunia!!!
 
Mwanzo 1:28

"Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.”

Kuzaliana kwa wingi ndiyo mojawapo ya majukumu ambayo mwanadamu alipewa na Muumba wake. Wewe ebu jaribu kuangalia, Yesu akiwa hapa duniani kwa mama yake mzazi Maria alikuwa na wadogo zake wa kiume wanne na wakike pia (maumbu zake).

Tukirejea katika maandiko matakatifu, nukuu kutoka katika vitabu vya injili Mathayo 12:46, Luka 8:19, na Marko 3:31 inathibitisha kwamba Yesu alikuwa na ndugu wanne wa kiume na majina yao ni Yakobo, Yusufu, Simioni na Yuda, ingawaje majina ya dada zake hayakutajwa (Mathayo 13:55).
 
Nchi hii ni kubwa sana.mfano kutoka chalinze mpaka morogoro ni mapori na misitu yenye utajiri mkubwa.kwa maoni yangu tuendelee kuzaana ili tuwe na uhakika wa solo la ndani.uwingi sio tatizo tatizo ni fikra na juhudi.
Tatizo ni CCM inayoongoza tangu Uhuru kushindwa kuibadili nchi yenye Tunu ya rasilimali kuwa kama Califoniyaa(in mwendazake's voice)
 
Ndugu zangu kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha Sana.Juzi nilikua wilayani Ukerewe nimeshangaa vijiji vya hii wilaya Yani Kila Kijiji kina shule za msingi mbilimbili lakini bado hazitoshi .Fikilia Kijiji kina shule mbili za msingi lakini bado shule zimezidiwa na wanafunzi.Hizi shule unakuta shule Ina hadi watoto mia Saba hadi mia tisa.

Nimeitolea Ukerewe kama mfano lakini najua hata sehemu nyinginezo za nchi yetu hali iko hivo .Kama Hali hii isipodhibitiwa na wizara ya afya basi huko mbeleni kazi ya serikali itakua kujenga madarasa na hospitals badala ya kufanya miladi ya maendeleo .
Australia nchi yenye maendeleo makubwa Ina watu ambao wahazidi million Saba Sasa ukija Tanzania Hali inatisha.Uzazi wa mpango utungiwe sheria ili tuweze kuwaletea Wananchi wetu maendeleo maana kasi ya uzazi ni kubwa kuliko ukuaji wa uchumi .
Asanteni.
Yaani inaonesha bado haujatembea Tanzania nenda machame eneo LA tarafa ya Masama nilitembelea shule za msingi. Na kata idadi ya wanafunzi ni ndogo sana mfano shule ya sekondari sawe form one wako 16 tu shule ya msingi. Nkwakinini shule nzima wanafunzi hawafiki. Mia walimu wanadai watoto hakuna na Hao watu wamejenga shule karibu karibu mfano nilitembea toka shule. Iliyopo kwenye kituo cha afya cha kirani hadi kituo cha. Masama umbali km 2 mbili hapo kàtikati kuna shule za msingi 4 na vituo viwili Vya. Afya na wazazi wana mwamko. Wa nyota ya kijani cha msingi siyo kupunguza kuzaa shule zijengwe. Za. Kutosha aridhi yetu bado kubwa sana
 
Umesema kweli mkuu,shule nyingi za msingi maeneo ya machame hazina wanafunzi kabisa. Kuna moja darasa la saba walikuwa sita tu.
 
Ndugu zangu kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha Sana.Juzi nilikua wilayani Ukerewe nimeshangaa vijiji vya hii wilaya Yani Kila Kijiji kina shule za msingi mbilimbili lakini bado hazitoshi. Fikiria Kijiji kina shule mbili za msingi lakini bado shule zimezidiwa na wanafunzi. Hizi shule unakuta shule Ina hadi watoto mia Saba hadi mia tisa.

Nimeitolea Ukerewe kama mfano lakini najua hata sehemu nyinginezo za nchi yetu hali iko hivo .Kama Hali hii isipodhibitiwa na wizara ya afya basi huko mbeleni kazi ya serikali itakua kujenga madarasa na hospitals badala ya kufanya miladi ya maendeleo .
Australia nchi yenye maendeleo makubwa Ina watu ambao wahazidi million Saba Sasa ukija Tanzania Hali inatisha.Uzazi wa mpango utungiwe sheria ili tuweze kuwaletea Wananchi wetu maendeleo maana kasi ya uzazi ni kubwa kuliko ukuaji wa uchumi .
Asanteni.
Katika watu vilaza unashika namba za juu sana. Hiyo hela ya kujenga madarasa unayoisema kutoka kwa serikali inatoka wapi kama sio population?? Umeshuhudia makato ya tozo kutoka kwenye population ndani ya mwezi tu yanaenda kujenga madarasa 500+ na vituo vya afya vya kumwaga. Unafikiri mkizaa hao watoto wawili wawili hiyo population ya kutosha kufanya maendeleo mtaitoa wapi??

Watu ndio mtaji wa kwanza kiuchumi (kama taifa halitaingiliwa na mataifa makubwa kwa vita, magonjwa ya kutengeneza,n.k). Angalia nchi zote zilizopiga hatua kubwa kiuchumi duniani mfano China, USA, India, Nigeria na nyingine zina watu wengi sana. Wewe unadanganywa na akina Bill Gates ambao wanajua wanachokitafuta wanapokwambia watu wakiwa wengi hali itakuwa mbaya.

Acha upopoma. Mtuache tuzae. Bila kuwa na watu hayo maendeleo ni ya nini??
 
Kwani elimu si bure? Acha tufyatue tu, kupanga ni kuchagua na masuala ya uzazi wa mpango ni hiari!
 
Fyatueni tu Watanzania. Tunataka Watanzania wazaliane kama sisimizi.
 
Umesema umechukulia hali ya Ukerewe kwamba itakuwa ni hivyo hivyo nchi nzima... Huoni kumbe umefanya majumuisho pasina kufuata utaratibu!?

Utafiti gani huo sampling ya namna hiyo? Rejea topic ya Research form three kwenye Geography

Kadhalika, usisahau kujibu maswali ya mdau hapo juu post namba 4
 
Back
Top Bottom