Serikali itunge sheria kuhusu uzazi wa mpango angalau watoto wawili kila familia maana kasi ya uzazi Tanzania inatisha

Serikali itunge sheria kuhusu uzazi wa mpango angalau watoto wawili kila familia maana kasi ya uzazi Tanzania inatisha

Wawili imekuwa China? Mpemba hamna hamna 10 kwa mke mmoja, akiwa na wake wanne basi anapiga 50.
 
Uzi huu auone boss wa boss wa boss wa wizara ya afya pamoja na msaidizi wake.
 
Babe la mji
Kama China inaweza kulisha watu wake 1.4 plus bilion na India inaweza kulisha watu wake 1.3 plus bilion huoni hata aibu kutuambia tusizae?
Kinachosumbua huko kwenu Murutunguru Ukerewe Ni huu utawala wa CCM.
Siku zinavyosogea ndio idadi ya watu wanaoweza kulisha taifa inavyopungua sababu ya technolojia. Kitu ambacho CCM hawakijui.
60 m inakupa wasiwasi?
 
Ndugu zangu kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha Sana. Juzi nilikua wilayani Ukerewe nimeshangaa vijiji vya hii wilaya Yani Kila Kijiji kina shule za msingi mbilimbili lakini bado hazitoshi

Fikiria Kijiji kina shule mbili za msingi lakini bado shule zimezidiwa na wanafunzi.Hizi shule unakuta shule Ina hadi watoto mia Saba hadi mia tisa.

Nimeitolea Ukerewe kama mfano lakini najua hata sehemu nyinginezo za nchi yetu hali iko hivo. Kama hali hii isipodhibitiwa na wizara ya afya basi huko mbeleni kazi ya serikali itakua kujenga madarasa na hospitals badala ya kufanya miladi ya maendeleo.

Australia nchi yenye maendeleo makubwa Ina watu ambao wahazidi million Saba Sasa ukija Tanzania Hali inatisha.Uzazi wa mpango utungiwe sheria ili tuweze kuwaletea Wananchi wetu maendeleo maana kasi ya uzazi ni kubwa kuliko ukuaji wa uchumi .
Asanteni.
Uliochoandika hakieleweki. Hujui matumizi ya angalau in english at least rudi shule!
 
Katika watu vilaza unashika namba za juu sana. Hiyo hela ya kujenga madarasa unayoisema kutoka kwa serikali inatoka wapi kama sio population?? Umeshuhudia makato ya tozo kutoka kwenye population ndani ya mwezi tu yanaenda kujenga madarasa 500+ na vutuo vya afya vya kumwaga. Unafikiri mkizaa hao watoto wawili wawili hiyo population ya kutosha kufanya maendeleo mtaiotoa wapi??

Watu ndio mtaji wa kwanza kiuchumi (kama taifa hakitaingiliwa na mataifa makubwa kwa vita, magonjwa ya kutengeneza,n.k). Angalia nchi zote zilizopiga hatua kubwa kiuchumi duniani mfano China, USA, India, Nigeria na nyingine zina watu wengi sana. Wewe unadanganywa na akina Bill Gates ambao wanajua wanachokitafuta wanapokwambia watu wakiwa wengi hali itakuwa mbaya.

Acha upopoma. Mtuache tuzae. Bila kuwa na watu hayo maendeleo ni ya nini??
Ujinga ni mzigo kuelimimika sio kukariri tumia akili yako kuitambua tz walau kidogo Jambo lolote uamuliwa na uhitaj na ugavi
je tz Ina lipi Ina uhitaji sana au ugavi sana hapo ndipo utoe pendekezo tuna rasilimari za kutosheleza watu wangapi
Ndipo uje na pendekezo la idadi ya watu
Kama hujui tz hata watu bilioni 1
wataishi na kutosheka hiyo ndiyo kweli acha kukalillI longolongo
Jifunze jiografia ya darasa la tano na uelewe kuhusu tz jibu utapata
 
Acha huo upuuzi umewacost ulaya hadi sasa wanachukua wakimbizi toka Afrika na Uarabuni kupata nguvu kazi
 
Uzazi wa mpango pekee sio solution Mkuu..
China walifanya hivuo nakipotisha sheria ya kuzaa mwisho watoto wawili tu.. baada ya kupigwa na corona na factors nyingine kama vile idadi ya wazee kuwa kubwa kuliko vijana sasa wameamuwa wenye kuruhusu watu wazaliane ...
Maana nguvu kazi inahitajika sana.. hadi sasa china kila siku ina ajiri watu/vijana wengi kutoka nchi nyingine za huko asia kama Philippines..thai etc

na hata hivyo wengi wachina walikuwa wakiendelea kuzaa nje ya nchi na watu wa mataifa mengine...

Umetolea mfano Australia.. kwa mtazamo wangu hata hao pia kwa nchi kubwa kama ile maana ni kama bara linalojitegemea.. uzazi wao wa mpango huo .. ..

unawafanya watafute nguvu kazi kwa kigezo cha immigrants/experts..atlist ndivyo ninavyowaza kwa haraka haraka labda naweza rekebishwa juu ya hilo
 
Wawili imekuwa China? Mpemba hamna hamna 10 kwa mke mmoja ,akiwa na wake wanne basi anapiga 50.
China wameachana na hiyo ya watoto 2, corona imewapiga na nchi yao pia ina wazee wengi sana kuliko vijana nguvu kazi hakuna... ina ajiri watu kutoka nchi za jirani..
So rais wao amerihusu
 
Iwe watoto wawili kwa kila mwanamke au kila mwanamme?
Umeuliza swali la msingi sana maana mwanaume mmoja anaweza kuwa na wake hadi watatu na mwanamke anaweza kuwa aliolewa akazaa watoto wawili kisha akaachika na kuja kuolewa tena na mwanaume ambaye hana kabisa mtoto.
 
Hali mbaya kwa Nani? Kuna mtu kakuomba akupe watoto wake umsaidie kulea?
Ndiyo.
Isitoshe hapa jijini Mwanza nakutana na watoto omba omba mitaani.
Ni wengi hadi inatia huruma, wengine wana miaka 6.
Ni ukatili kuzaa mtoto bila kuwa na plan ya future yake. Anaishia kuwa mtoto wa mtaani, kisha mdokozi na kibaka halafu wananchi wenye hasira wanamuua.
 
Ndugu zangu kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha Sana. Juzi nilikua wilayani Ukerewe nimeshangaa vijiji vya hii wilaya Yani Kila Kijiji kina shule za msingi mbilimbili lakini bado hazitoshi

Fikiria Kijiji kina shule mbili za msingi lakini bado shule zimezidiwa na wanafunzi.Hizi shule unakuta shule Ina hadi watoto mia Saba hadi mia tisa.

Nimeitolea Ukerewe kama mfano lakini najua hata sehemu nyinginezo za nchi yetu hali iko hivo. Kama hali hii isipodhibitiwa na wizara ya afya basi huko mbeleni kazi ya serikali itakua kujenga madarasa na hospitals badala ya kufanya miladi ya maendeleo.

Australia nchi yenye maendeleo makubwa Ina watu ambao wahazidi million Saba Sasa ukija Tanzania Hali inatisha.Uzazi wa mpango utungiwe sheria ili tuweze kuwaletea Wananchi wetu maendeleo maana kasi ya uzazi ni kubwa kuliko ukuaji wa uchumi .
Asanteni.
Mkuu ni kweli population ya Tanzania inakua haraka sana. Kuna haja ya serikali kuwaekimisha watu ili wazae watoto wanaonudu kuwatunza vizuri. Watu wengi Bongo wanaamini kama mlo unapatikana then everything is done. Mungu atasadia.

Maasahihisho kidogo, population ya Australia iko above 25 million na siyo million 7.
 
Kwa kwel hali ni mbaya,ukiwa hospital kitengo cha watoto unaweza fanya kazi mpaka ukasahau kunywa chai,kuna mijitu mpaka unataman uipige makofi ni masikin la kutupwa hata kujenga limeshndwa lakin linazaa asubuhi na mchana
 
Ndiyo.
Isitoshe hapa jijini Mwanza nakutana na watoto omba omba mitaani.
Ni wengi hadi inatia huruma, wengine wana miaka 6.
Ni ukatili kuzaa mtoto bila kuwa na plan ya future yake. Anaishia kuwa mtoto wa mtaani, kisha mdokozi na kibaka halafu wananchi wenye hasira wanamuua.
Watoto wa mitaani siyo matokeo ya kuzaa watoto wengi. Utakuta huyo Ni mtoto pekee Ila yupo mitaani sababu ya mimba zisizotarajiwa,;kuvunjika kwa ndoa, umaskini uliokithiri, ukatili wa wazazi na mambo kama hayo.
Mimi tumezaliwa kumi na wote tupo na wengine tunazeeka Sasa.
 
Ndugu zangu kasi ya Watanzania kuzaliana inatisha Sana. Juzi nilikua wilayani Ukerewe nimeshangaa vijiji vya hii wilaya Yani Kila Kijiji kina shule za msingi mbilimbili lakini bado hazitoshi

Fikiria Kijiji kina shule mbili za msingi lakini bado shule zimezidiwa na wanafunzi.Hizi shule unakuta shule Ina hadi watoto mia Saba hadi mia tisa.

Nimeitolea Ukerewe kama mfano lakini najua hata sehemu nyinginezo za nchi yetu hali iko hivo. Kama hali hii isipodhibitiwa na wizara ya afya basi huko mbeleni kazi ya serikali itakua kujenga madarasa na hospitals badala ya kufanya miladi ya maendeleo.

Australia nchi yenye maendeleo makubwa Ina watu ambao wahazidi million Saba Sasa ukija Tanzania H
we Ni akili ndogo kusema watu wasizae watoto wengi Bali serikali inatakiwa iongeze production ya social services, kutanua na kuimarisha fursa za uchumi kwa Kasi ili hao wanaozaliwa waje kuwa productive.
 
Salaam,
Kwa kweli napingana sana na maoni ya mleta Uzi, kuangalia ukerewe tu huwezi kutoa majawabu ya watu wanazaliana sana, kwa kweli kwa miaka ya karibuni kumekuwa nachangamoto sana ya uzazi kwa watu wengi,Watu hawazai!!! Na hawana nguvu za kuzaa.
Institution niliyomo , mimi ni mmoja ya watu wachache wenye watoto wengi.
Kuna watu wameoa na kuolewa zaidi ya miska 10 na hawana watoto,wengine mtoto mmoja na wengi sana 3.
Wengi wetu tuliozaliwa mwanzoni mwa miaka ya 70 wazee wetu walituzaa watoto wengi sana.
Vijana Wa kisasa tumepunguza sana idadi ya Watoto, kwa sababu ya changamoto za maisha.Mtaani kwangu ninakoshi mwenye watoto wengi anao 4, na wazee sana wenye watoto 5 au 6.
 
Back
Top Bottom