Serikali itupie macho huduma zinazotolewa hospitali ya wilaya ya Maswa.

Serikali itupie macho huduma zinazotolewa hospitali ya wilaya ya Maswa.

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Utoaji wa huduma duni za afya katika hospitali ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu unaweza kuwa na sababu nyingi, na si lazima lawama zote ziwe kwa mganga mkuu wa wilaya,Dk Hadija Zegega moja kwa moja, japokuwa yeye ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa huduma za afya kwenye wilaya.

Hospitali hiyo ina majengo mazuri sana katika mkoa huo ukiachilia majengo yaliyoko katika Hospitali ya rufaa ya mkoa ila huduma zake ni mbovu hasa kwa wakinamama wajawazito,watoto chini ya miaka mitano na wazee wenye miaka 60 na zaidi.

Makundi haya yapaswa kupatiwa bure kutokana na sera ya afya ya taifa ya mwaka 2007 ililenga kuhakikisha kuwa makundi haya maalum yanapata huduma za afyabila malipo ili kuboresha afya na ustawi wao.

Lakini katika hospitali ya wilaya ya Maswa makundi hayo yamekuwa yakitozwa fedha ili waweze kupata huduma za matibabu kinyume na sera ya afya ya Taifa ya mwaka 2007 na hivyo kuzua malalamiko ya mara kwa mara kwa viongozi wa ngazi za juu wanaofanya ziara wilayani humo.

Sababu zinazoweza kuwa chanzo cha huduma mbovu katika hospitali hiyo ni pamoja na usimamizi dhaifu licha ya kuwepo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali lakini hana usimamizi mzuri, hawezi kuhakikisha kuwa watumishi wanatimiza wajibu wao ipasavyo, vifaa vinatumika vizuri, na wagonjwa wanahudumiwa kwa heshima na ufanisi.

Motisha duni kwa watumishi ni kwamba hawalipwi kwa wakati stahiki zao licha ya mazingira yao ya kazi kuwa mazuri maana kuna dawa na vifaa tiba vya kutosha tena vya kisasa lakini huduma zinazotolewa ni duni.

Lugha isiyo ya staha kwa wagonjwa zinazotolewa na wauguzi walioko katika wodi ya akinamama wajawazito ambao wanasubiri kujifungua ni moja ya kero sugu katika hospitali hiyo na ambayo imeshindwa kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu licha ya kuripotiwa mara kwa mara kwa viongozi wa juu wa serikali wa wilaya na mkoa.

Ufuatiliaji na uwajibikaji hafifu katika hospitali hiyo kwani hakuna mifumo ya kupima utendaji au kutoa adhabu kwa watumishi, hivyo uzembe huo unaendelea bila kukemewa.

Kwa hiyo, mganga mkuu ana sehemu kubwa ya kuwajibika, lakini pia kuna mfumo mzima wa afya unaohusika. Ikiwa matatizo yanaendelea kwa muda mrefu bila suluhisho, basi usimamizi kwa ujumla – kuanzia ngazi ya hospitali hadi halmashauri unapaswa kuangaliwa kwa kina.
 
Hayo yapo kila sehemu mkuu. Hii bchi Iko kwenye autopilot mode tangu machi 17
 
Hiyo sera haitekelezeki karibia NCHI nzima, wanasiasa wanawagombanisha watoa huduma wa Afya na Wananchi

Ukinitajia vituo vi3 nchi hii hio sera inatekelezeka kwa 100% nakutumia 10k
 
Back
Top Bottom