Serikali itupie macho Kaburi la shujaa Balozi,Luteni Jenerali,Silas Peter Mayunga lililopo Maswa

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Licha ya kuwa mmoja wa viongozi mashuhuri na mashujaa waliolitumikia Taifa kwa uadilifu na uzalendo wa hali ya juu, kaburi la Balozi na Luteni Jenerali mstaafu Silas Peter Mayunga limeonekana kuwa katika hali ya kusikitisha, kana kwamba limetelekezwa.

Kaburi hilo lililopo katika makaburi ya Wasabato, Unyanyembe, mjini Maswa, mkoani Simiyu, halina alama ya heshima wala uangalizi wa aina yoyote kutoka serikalini, licha ya mchango mkubwa wa marehemu katika historia ya Tanzania.

Silas Mayunga alizaliwa mwaka 1940 na alifariki dunia Agosti 6, 2011, kabla ya kuzikwa rasmi mnamo Agosti 12, 2011 katika eneo hilo. Licha ya hadhi yake kama mwanajeshi mwandamizi,Mkuu wa mkoa na balozi aliyewahi kuiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali, kaburi lake linakosa matunzo na linaonekana kupuuzwa.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Maswa waliozungumza leo Julai 25,2025 ambayo ni kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa hapa nchini wameeleza masikitiko yao wakitaka serikali kuu na mamlaka za mkoa wa Simiyu kuchukua hatua za haraka kuheshimu mchango wa shujaa huyo.

"Ni aibu kwa Taifa kuona kaburi la mtu mkubwa kama Luteni Jenerali Silas Mayunga likiwa katika hali hii. Huyu ni mtu aliyelipigania Taifa, akalitumikia kwa moyo wote, lakini sasa ni kama amesahaulika," amesema mkazi mmoja ambaye mmoja wa wazee wa eneo hilo kwa masikitiko.
 
Attachments

  • KABURI MAYUNGA 4.jpg
    KABURI MAYUNGA 4.jpg
    2.8 MB · Views: 48
  • KABURI LA MAYUNGA 2.jpg
    KABURI LA MAYUNGA 2.jpg
    1.7 MB · Views: 45
  • images (2) (1).jpeg
    images (2) (1).jpeg
    12.4 KB · Views: 44
Aliyekufa kafa , Hamna fadhila keep Energy on living beings.
 
Hebu totelee hapa,ushabiki wako maandazi.........serikali iache kugawa chanjo kuwalinda watoto dhidi ya magonjwa,.......ianze kulinda makabuli?
Upo serious kweli wewe?,Kati ya Abdulwahid Sykes,Aziz Ally,na Biti Titi Mohamed,wapambania uhuru,........na huyo kamanda wako UCHWARA nani ni wa muhimu?,
Shauri serikali,ichimbe madini yake yenyewe,hata wewe upate huruma Bora,na sio kuja na ajenda ya kulinda makabuli
Licha ya kuwa mmoja wa viongozi mashuhuri na mashujaa waliolitumikia Taifa kwa uadilifu na uzalendo wa hali ya juu, kaburi la Balozi na Luteni Jenerali mstaafu Silas Peter Mayunga limeonekana kuwa katika hali ya kusikitisha, kana kwamba limetelekezwa.

Kaburi hilo lililopo katika makaburi ya Wasabato, Unyanyembe, mjini Maswa, mkoani Simiyu, halina alama ya heshima wala uangalizi wa aina yoyote kutoka serikalini, licha ya mchango mkubwa wa marehemu katika historia ya Tanzania.

Silas Mayunga alizaliwa mwaka 1940 na alifariki dunia Agosti 6, 2011, kabla ya kuzikwa rasmi mnamo Agosti 12, 2011 katika eneo hilo. Licha ya hadhi yake kama mwanajeshi mwandamizi,Mkuu wa mkoa na balozi aliyewahi kuiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali, kaburi lake linakosa matunzo na linaonekana kupuuzwa.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Maswa waliozungumza leo Julai 25,2025 ambayo ni kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa hapa nchini wameeleza masikitiko yao wakitaka serikali kuu na mamlaka za mkoa wa Simiyu kuchukua hatua za haraka kuheshimu mchango wa shujaa huyo.

"Ni aibu kwa Taifa kuona kaburi la mtu mkubwa kama Luteni Jenerali Silas Mayunga likiwa katika hali hii. Huyu ni mtu aliyelipigania Taifa, akalitumikia kwa moyo wote, lakini sasa ni kama amesahaulika," amesema mkazi mmoja ambaye mmoja wa wazee wa eneo hilo kwa masikitiko.
 
Yaani Kodi ilipwe kutunza makaburi? Ivi hii nchi nan ameturoga tuone kila kitu ni KAZI ya serikali? Ina maana hana ndugu,jamaa na marafiki?
Poor brains.
 
CCM ikishakutumia kujichambia inakutupa chooni na kuflashi choo
 
Hebu totelee hapa,ushabiki wako maandazi.........serikali iache kugawa chanjo kuwalinda watoto dhidi ya magonjwa,.......ianze kulinda makabuli?
Upo serious kweli wewe?,Kati ya Abdulwahid Sykes,Aziz Ally,na Biti Titi Mohamed,wapambania uhuru,........na huyo kamanda wako UCHWARA nani ni wa muhimu?,
Shauri serikali,ichimbe madini yake yenyewe,hata wewe upate huruma Bora,na sio kuja na ajenda ya kulinda makabuli
Huyo ni shujaa kama hao ni lazima apewe heshima yake kama walivyo wengine
 
Huyu mwamba na akina musuguri ndo waliomfurusha Iddi Amini kule Uganda kipindi cha vita vya Kagera, hayo majina kipindi hicho ndo ilikuwa habari ya mjini vijana wa leo siyo rahisi kujua umuhimu wao
 
Back
Top Bottom