Serikali itupie macho Ofisi ya Utumishi Karagwe

Serikali itupie macho Ofisi ya Utumishi Karagwe

Hae Mosu

Member
Joined
Dec 23, 2019
Posts
43
Reaction score
33
Kuna tatizo kubwa Kwa Afisa Utumishi wa HALMASHAURI ya KARAGWE hasa katika suala la kuhudumia watumishi.

Inajulikana kuwa Serikali kupitia wizara ya Utumishi wa Umma imetoa nafasi Kwa watumishi Kwa ambao wanahitaji kuhama ili kufuata wenza wao, waombe uhamisho ila kwa Karagwe, Afisa Utumishi anagoma kuwasaidia watumishi Kwa kigezo kuwa hawajapata taarifa kamili na utaratibu wa namna gani watumishi hao wataweza kuhama.

Je, serikali haijatoa utaratibu Kwa Maafisa Utumishi ili waanze mchakato wa kuwawezesha watumishi ili wapate uhamisho? Na je, huyu Afisa Utumishi anafanya haya Kwa lengo gani? na hili jambo haliharibu taswira njema ya serikali kuamua kuwasikiliza watumishi?.

TUNAIOMBA SERIKALI ISIKIE KILIO CHETU SISI WATUMISHI WA HALMASHAURI YA KARAGWE ILI TUPATE HAKI ZETU KWANI SIKU ZIMEBAKI CHACHE NA HAKUNA LINALOFANYIKA. ASANTE
 
Huyo anashida zake binafsi.

Ikiwa Waziri katangaza,

Katibu Mkuu akaandika na barua na hiyo barua ishatoka na ipo hata kwenye mitandao halafu yeye anasema Hana taarifa!!!!


- Anatengeneza Mazingira ya kula Rushwa.

- Serikali ipeleke afsa utumishi mwingine.
 
hr kwann hiwa na roho mbaya hiv. haya maisha tu.leonupo kesho haupo au upo kaburin
 
Back
Top Bottom