DOKEZO Serikali itusaidie, Dampo la Bakhresa ni hatari kwa Afya za Wananchi wa Kijiji cha Kazole

DOKEZO Serikali itusaidie, Dampo la Bakhresa ni hatari kwa Afya za Wananchi wa Kijiji cha Kazole

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nchi ndio haina mpango.
Azam waliona mbali wakachagua vikinduu kuwa ni dampo lao,nyie Wazaramo kwa kujifanya mnayafuata mapori mmelifuata.
Huwa nakerwa sana na huu utaratibu wa vijiji,ndio mnaanzisha kijiji halafu ndio mnaomba barabara za sogea nipite baadae maji baadae vichochoro vya bange pombe na mikojo.
Ndiovmnaotufanya tutembee na spidi 50 nchi nzima kisa kijiji.
 
Azam waliona mbali wakachagua vikinduu kuwa ni dampo lao,nyie Wazaramo kwa kujifanya mnayafuata mapori mmelifuata.
Huwa nakerwa sana na huu utaratibu wa vijiji,ndio mnaanzisha kijiji halafu ndio mnaomba barabara za sogea nipite baadae maji baadae vichochoro vya bange pombe na mikojo.
Ndiovmnaotufanya tutembee na spidi 50 nchi nzima kisa kijiji.
Bakhresa na utajri wote huo anashindwa kujenga ukuta wa dampo?
 
Aliyemfata mwenzake ndiyo ana tatizo na ndiye anapaswa hama.

Ni sawa na Wazo na Twiga Cement
 
Aliyemfata mwenzake ndiyo ana tatizo na ndiye anapaswa hama.

Ni sawa na Wazo na Twiga Cement
Wazaramo wanashida sana,kila leo wanaenda palipo pabaya.haya wapambane na jalala.
 
Subirini nyie wanakijiji wote muhamishwe huko ndiyo mtajua
Hamjui [emoji1]

Ova
 
Ngoja nimcheki Upendo Michael au Istabela Mallisa wa Azam Tv aje aripoti hiyo taarifa
 
View attachment 2725927
Muonekano wa sehemu ya Dampo Bakhresa ulivyo wakati wa msimu huu wa kiangazi.
Miaka zaidi ya 10 iliyopita wamiliki wa Makampuni ya Bakhresa, walifika katika Kata ya Vikindu, Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kununua eneo kwa ajili ya kutupa taka.

Kwa wakati huo asilimia kubwa ya eneo lilikuwa ni pori na hakukuwa na makazi ya watu karibu na eneo hilo la Dampo.

Miaka ilivyozidi kwenda, Vikindu na maeneo yake ya jirani (yaliyomo ndani ya Vikindu) yakawa yanakua, idadi ya watu ikaongezeka kutokana na mwingiliano wa shughuli mbalimbali.

Wakati huohuo, Dampo la Bakhresa lipo wazi, mvua ikinyesha maji yanatirirka kuelekea kwenye makazi ya watu hasa wa Kijiji cha Kazole ambacho ni moja ya vijiji vinachopatikana ndani ya Kata ya Vikindu.

Baadhi yetu Wanakijiji wa Kazole tukafanya mpango wa kukutana na uongozi wa Bakhresa kuwashauri kuwa wajenge uzio ili kuzuia maji yanayoenda kwenye makazi ya watu.

Hoja hiyo ikawa inapigwa danadana na imeendelea kupigwa danadana hadi leo, watendaji wa upande wa Bakhresa wakawa wanadai wao waliingia mkataba na Vikindu na sio Kijiji cha Kazole.

Ikumbukwe Kazole ilipewa hadhi ya kuwa Kijiji kinachojitegemea Mwaka 2014, lakini mikataba ya Dambo yote ilisainiwa Vikindu, hivyo hatuna cha kufanya.

Dambo ambalo ninalizingumzia hapa, sijui lina sumu gani au zinawekwa dawa gani kwa kuwa hakuna mdudu anayesogea kwenye taka hizo, zinaoza na kunuka lakini Wadudu hawasogei.

Sasa Watoto wa mtaani wanapita na kushikashika vitu kwenye Dampo hilo, hapo nadhani unaweza kufikiria kuhusu hatari kwa afya zao ikoje.

Kingine ni kuwa wakati wa msimu wa matunda kama maembe au machungwa au matunda mengine ambayo yanatumika zaidi kwenye viwanda, ndipo ambapo uchafu unakuwa mwingi, kuna wakati inafikia hadi lori 30 hadi 40 kwa siku zinazokuja kumwga taka hapo.

Maembe mabovu yanayotupwa huuzwa tena mtaani
Taarifa nyingine ni kuwa yale maembe na machungwa ambayo yanaonekana hayafai na kwenda kutupwa katika Dampo hilo, kuna baadhi ya watu ambao sio waaminifu wanayachukua yale ambayo yanaonekana kuwa na muonekano mzuri kisha kwenda kuuzwa mitaani kwa bei rahisi hasa mitaa ya Temeke.

Wito wetu
Wito wetu sisi Wananchi wa Kazole na maeneo ya Vikindu na jirani, tunaomba Serikali ifuatilie kinachoendelea, kwani tuna wakati mgumu wa afya zetu kutokana na Dampo hilo.

Pia wanaochukua matunda yanayotupwa na kwenda kuyauza mitaani Dar es Salaam na kwingineko wanahatarisha afya za walaji kwa kuwa matunda hayo si salama kwa afya na hayafai kuliwa.
Dampo ni fursa lichangamkieni likiondoka mtajuta, yaani gesi na mbolea mnaishitaki iondolewe!
 
Back
Top Bottom