Kwanini maeneo ya Mchikichini ilala, Sunna Magomeni na Hananasif Kinondoni jijini Dar es Salaam yasitumike kujenga makaazi mapya kwa watakaohamishwa toka bonde la mto Msimbazi jijini Dar es Salaam badala ya kuwalipa fidia ndogo wananchi serikali ibebe jukumu kuwajengea makaazi yaliyopangwa eneo la Mchikichini Sunna na Hananasif
ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI 2020 - 2025:
(c) Kuboresha maeneo hatarishi ikiwemo bonde la
mto Msimbazi jijini Dar
es Salaam ili kudhibiti mafuriko, kuhifadhi mazingira na kuyafanya
kuwa vivutio kwa watalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali;
(d) Kuimarisha utekelezaji wa Programu ya Taifa ya Kurasimisha Makazi
yasiyo rasmi katika mikoa 26 nchini ikiwa ni pamoja na kuwezesha
ujenzi wa miji ya kisasa na kupunguza makazi yasiyo rasmi kwa
kuandaa Mipango Kabambe 6 ya miji ya Mpanda, Njombe, Mererani,
Chato, Ifakara na Kahama; na
(e) Kusimamia na kuratibu upangaji upya maeneo yaliyochakaa (re-
development) katika miji mbalimbali nchini.
Nyumba na Makazi
75. Chama Cha Mapinduzi kinatambua kuwa nyumba ni rasilimali ya msingi
na hitaji muhimu kwa maisha ya binadamu. Katika kusimamia hilo, kwa kipindi cha mwaka (2015 - 2020), Chama kimeisimamia Serikali kutoa
huduma stahiki ya makazi bora na kupata mafanikio yafuatayo:-
(a) Kuendeleza uwezeshaji wa watumishi kwa kuwapatia mikopo ya....
TOKA MAKTABA :
29 April 2021
MASWALI BUNGENI
Dodoma, Tanzania
Mheshimiwa TARIMBA G. ABBAS Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza kazi ya ujenzi wa mradi wa Mto Msimbazi ambao umetajwa katika Bajeti ya mwaka 2021/2022?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) Alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tarimba Gulam Abbas Mbunge wa Jimbo la kinondoni kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali na Benki ya Dunia inatarajia kufanya majadiliano ya mapendekezo ya awali ya mradi mwezi Desemba 2021 na kusaini mkataba wa mkopo wa kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 120 ifikapo mwezi Machi 2022 na utekelezaji wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Julai, 2022 baada ya kukamilisha masharti yote ya kutekeleza mradi.
Mheshimiwa Spika, huu ni mradi wa kukabiliana na mafuriko katika bonde la Mto Msimbazi. Mradi huo kwa sasa upo katika hatua za maandalizi ambapo usanifu wa miundombinu husika pamoja na nyaraka muhimu kwa ajili ya masuala ya mazingira na fidia zinaandaliwa.
Mheshimiwa Spika, Kimsingi mradi huu utahusisha pia ujenzi wa daraja jipya la Jangwani lenye urefu wa mita 390; Upanuzi wa mto kwa upande wa chini kuanzia barabara ya Kawawa hadi daraja la Salander ili kuruhusu maji ya mvua kwenda baharini kwa haraka;
Mheshimiwa Spika, Uimarishaji wa kingo za mto msimbazi katika maeneo korofi kwa upande wa juu katika maeneo ya Tabata na Kinyerezi ili kuzuia mmomonyoko wa udongo;
Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa vitega mchanga na vituo vya kuhudumia mto kwa ajili ya kupunguza kiwango cha mchanga kinachotuama eneo la chini la Mto Msimbazi;
Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa matuta kwa upande wa chini wa mto Msimbazi (kuanzia Daraja la Selander hadi Barabara ya Kawawa) yatakayoruhusu matumizi mbalimbali ya ardhi ikiwemo
City Park eneo la Jangwani pamoja na maendeleo ya
makazi maeneo ya Mchikichini, Sunna na Hananasif; Program za kuboresha usimamizi wa takangumu katika Kata 18 zinazozunguka bonde la Mto Msimbazi; na Kurudishia uoto wa asili katika maeneo yenye mikoko, maeneo yenye ardhi oevu, pamoja na misitu ya Pugu na Kazimzumbu, Wilayani Kisarawe.
MHE. TARIMBA G. ABBAS aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Mto Msimbazi ambao umeainishwa katika
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020 – 2025?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira; kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Tarimba Gulam Abbas Mbunge Jimbo la Kinondoni naomba kutoa maelezo yafuatayo kuhusu Mto Msimbazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inatekeleza mradi wa kuendeleza Jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam Metropolitan Development Project) kwa
mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 300 kutoka Benki ya Dunia.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza DFID, inatekeleza programu ya Tanzania Urban Resilience Programme ambayo imelenga kuzisaidia halmashauri na Serikali Kuu katika kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi. Kwa kuanzia, programu itaanza kutatua changamoto zinazolikabili Bonde la Mto Msimbazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, tayari DFID imeshatenga kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 20 kwa ajili ya Bonde la Mto Msimbazi.
Pia Benki ya Dunia, kupitia mradi wa DMDP, imekubali mkopo wa nyongeza wa kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 100 kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za Bonde la Mto Msimbazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Abbas Tarimba Gulam Mbunge wa Kinondoni:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepanga kubadili eneo la bonde la Mto Msimbazi kuwa eneo la uwekezaji na fursa mbalimbali. Ili kufikia azma hiyo, usanifu wa mradi huo umekamilika. Utekelezaji wa mradi utaanza baada ya kupata idhini ya Serikali kuhusu matumizi ya fedha hizo za mkopo kupitia Wizara ya Fedha na Mipango.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, ili kupunguza athari za mafuriko kwa sasa, kipande cha Mto Msimbazi cha daraja la Jangwani kinafanyiwa usafi wa mara kwa mara na wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Source :
Bunge Polis
habarileo.co.tz
https://habarileo.co.tz › benki-ya-du...
Benki ya Dunia yatoa mabilioni Dar
6 Oct 2022 — BENKI ya Dunia imetoa mkopo wa Dola za Marekani milioni 200 (Sh bilioni 466.387) kugharamia mradi wa Bonde la Msimbazi ili kuepuka mafuriko ...